Meneja wa Shoprite kizimbani kwa kuwafungia chumbani wafanyakazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Meneja wa Shoprite kizimbani kwa kuwafungia chumbani wafanyakazi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Feb 4, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,483
  Likes Received: 5,718
  Trophy Points: 280
  Meneja wa Shoprite kizimbani kwa kuwafungia chumbani wafanyakazi  RAIA wa Kizungu, ambaye ni Meneja Mkuu wa duka la kuuza bidhaa za kusindika maarufu kama Shoprite, amefikishwa kizimbani kwa tuhuma za kuwafungia katika chumba wafanyakazi wa duka hilo kinyume na sheria.
  Mtuhumiwa huyo ni Fredrick Skein [33] ambaye alitokea nchini Afrika ya Kusini, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala ya jijini Dar es Salaam kujibu tuhuma zinazomkabili.

  Alisomewa shtaka lake katika Mahakamani hiyo na Inspekta Msaidizi wa Polisi, Denis Mujumba mbele ya Hakimu Janeth Kinyage wa Mahakama hiyo.

  Mujumba alidai kuwa, mshitakiwa alitenda kosa hilo Novemba 12, mwaka jana, katika duka hilo lililopo barabara ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.

  Ilidaiwa kuwa mshitakiwa aliwafungia wafanyakazi hao katika chumba zaidi ya masaa kadhaa kwa sababu ambazo hazikuweza kuelezwa Mahakamani awali hadi kesi itakaposikilizwa.

  Wafanyakazi waliofungiwa katika chumba hicho walikuwa watatu na walitambulika kwa jina la Anna Temu, Juma Said na Hassan Kassim.

  Hakimu alimwambia mshitakiwa angeweza kuwa nje kwa dhamana kwa kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakaoweza kusaini milioni moja kila mmoja na kuwasilisha hati zake za kusafiria mahakamani.

  Hata hivyo mshitakiwa alitimiza masharti ya dhamana na kuweza kuwa nje kwa dhamana, na kesi iliahirishwa hadi hapo Machi 3, mwaka huu, itakapotajwa tena.
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hawa wawekezaji wakiwa TZ wana kiburi sana, hii yote hutokana na kujua kuwa hawatafanywa kitu. Nakumbuka wale jamaa wa NIDA Textile walivyompiga mfanyakazi na kumfungia ndani wakisema kuwa alikuwa anaiba majora ya nguo, sijui kesi yake iliishia wapi alipowashitaki. Pia muwekezaji wa Speke Bay Lodge iliyoko karibu na Kijiji cha Mwabulugu, Mwanza. Aliwahi kufungia raia sababu tu walikuwa wanapita na mitumbwi yao eneo la ziwa mbele ya Hotel yake, sasa mpaka eneo la ziwa ni lake?. Hivi viburi vya wawekezaji kuna siku vitawatokea puani.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,483
  Likes Received: 5,718
  Trophy Points: 280
  Hawa viongozi wetu wanatufanya kuwa watumwa mkuu mfumwa!!!
   
 4. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hii ndio bongo bwana. Bunge lilikaa chini na kutunga sheria ya kuvutia wawekezaji. What do you expect? Hawa watakuwa wanalindwa mpaka siku tutakaposema basi.
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,185
  Trophy Points: 280
  asante wawekezaji kwa kuturudisha zama za mijeredi ya wakoloni.
  mlipokuja kuomba nafasi ya kuwekeza mlikuja kwa heshima ,mikono uyenu ikiwa nyuma , na vichwa vimeinamishwa chini.
  Leo mmetugeuka, mmetukalia vichwani, mwatubebesha mizigo mizito inayozisononesha akili zetu na kuudhalilisha utu wetu.
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,483
  Likes Received: 5,718
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka kuna mmoja aliwatoa resi kamati ya bunge uko mbugani mpaka leo aijulikani alipewa adhabu gani
   
Loading...