Meneja wa redio ya Kagasheki ni balaa

Mutabora

Member
Apr 29, 2010
45
4
anaitwa Emmanuel Mbaule,kwa mwaka mmoja amefanikisha mkakati wa kuwatimua wafanyakazi tisa kwenye redio Kasibante inayomilikiwa na Waziri Khamis Kagasheki.Cv yake inasomeka eti alikuwa kiongozi mzuri hapo Redio Mlimani ya Dar es salaam.Kutimua wafanyakazi hovyo ni sifa au udhaifu ktk uongozi?
 
inategemeana pia na sifa za hao waliotimuliwa. Kila siku hapa JK watu wanamshangaa kwa kutomtimua Ngeleja,this is because anaonekana si mchapa kazi. kwahiyo yeye kama meneja kama aliona wanaleta uzembe alikuwa hana budi kwani redio ina goals zake kama anaona kakuajili kakupatia tageti zako nawe umelala afanyeje mkuu? Huyo anafaa sana kwenye hizi wizara za serikali yetu.
 
Aisee, bora umeleta hii habari jamvini:
Huyu dogo Mbaule hata mie nimeshindwa kuelewa ufahamu wake ktk maswala ya ADMINISTRATION amekua akiendesha ofisi kinyume na taratibu na misingi ya utumishi.

Bahati nzuri anaofanya nao kazi ni wastaarabu kinyume na hivyo balozi Kagasheki angekuwa nasuluhisha kesi kila kukicha, Redio kwa sasa imechukiwa na Watu kwasababu ya uongozi wake mbovu. Kuna haja ya kumvua cheo cha Umeneja hakimfai kabisa, Mbaule kuendelea kuwa Meneja ni kudhalilisha professional za watu.

Kama hataki kubadilika, atabadilishwa na umma muda si mrefu.
 
Hivi hii radio inasikika mpaka wapi? Maruku inafika au Katoma au Mugeza?
 
inategemeana pia na sifa za hao waliotimuliwa. Kila siku hapa JK watu wanamshangaa kwa kutomtimua Ngeleja,this is because anaonekana si mchapa kazi. kwahiyo yeye kama meneja kama aliona wanaleta uzembe alikuwa hana budi kwani redio ina goals zake kama anaona kakuajili kakupatia tageti zako nawe umelala afanyeje mkuu? Huyo anafaa sana kwenye hizi wizara za serikali yetu.

Katika kumwachisha kazi mfanyakazi kuna taratibu zake kisheria: hakuna cha kutimuatimua kama anavyofanya huyu dogo, anachofanya ni aibu na endapo anaowatimua wakijua wanavyotendewa ndivyo sivyo patachimbika.

Ushauri kwa waliotimuliwa:
Ebu nendeni muonane na Maafisa Kazi, wanapatika ktk Ofisi za Idara ya Kazi-Ofisi za Wizara ya Kazi na Ajira, kwa Bukoba ziko Kashai Road, kupita Soko kuu, karibu na Uwanja wa ndege, nyuma ya Shule ya msingi Bilele:

Ushauri mtakao pewa ufanyie kazi.
 
Mods napendekeza lianzishwe jukwaa la 'MKOA KWA MKOA' ili watu wajadili vizuri masuala ya majimboni kwao.
 
hiyo redio kazi yake kumsifia kagasheki,hata jina lenyewe 'kasibante' limekaa kimajungu. Kwa hiyo lazima matokeo yawe kama hivo,ingawa tunamshukuru kwa kuleta radio station wakwanza,na hiko fit kwenye burudani.
 
tunaweza kuisikia hiyo redio online? tupeni link maana wengine hatupo huko bukoba au ni redio ya kikabila?
 
Mods napendekeza lianzishwe jukwaa la 'MKOA KWA MKOA' ili watu wajadili vizuri masuala ya majimboni kwao.

Ili iweje weye inakusumbua nini kama hauna cha kuandika naona ukae tu kimya maana inaonekana hutaki watu waandike na wengine wasome

Unashauri kwingine ili aandike mikoa yake tofauti au?
 
hiyo redio kazi yake kumsifia kagasheki,hata jina lenyewe 'kasibante' limekaa kimajungu. Kwa hiyo lazima matokeo yawe kama hivo,ingawa tunamshukuru kwa kuleta radio station wakwanza,na hiko fit kwenye burudani.

Mkuu nyekundu maana yake nini? Kweli inabidi ianzishwe thread ya mkoa kwa mkoa kama alivyopendekeza Kakalende manake wakati mwingine watu wanataka tujadili mambo ya kijijini kwao badala ya mambo ya Taifa.
 
Ili iweje weye inakusumbua nini kama hauna cha kuandika naona ukae tu kimya maana inaonekana hutaki watu waandike na wengine wasome

Unashauri kwingine ili aandike mikoa yake tofauti au?

Mkuu hivi anaowashauri kwamba waende kwa maafisa kazi wako humu JF? Vinginevyo ushautri wake umemwagika chini
 
Back
Top Bottom