STRUGGLE MAN
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 8,638
- 16,566
Meneja wa kampuni kubwa Somalia auawa katika shambulio la droni la Marekani
Meneja wa shirika kubwa zaidi la mawasiliano nchini Somalia ameuawa katika shambulio la droni (ndege zisizo na rubani) za Marekani katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
Mtandao wa habari wa Military Times umeripoti kwamba, Marekani inadai kuwa inashambulia ngome za magaidi wenye mfungamano na mtandao wa al Qaida huko Somalia, lakini sehemu kubwa ya mashambulizi ya Marekani nchini humo yanaua raia akiwemo Mohamud Haji Sirad mwenye umri wa miaka 55 ambaye alikuwa meneja wa shirika kubwa zaidi la mawasiliano nchini Somalia. Meneja huyo ameuawa baada ya droni za Marekani kumshambulia kwa makombora mawili akiwa katika shamba lake wilayani Jilib.
Komandi ya Kijeshi ya Marekani barani Afrika AFRICOM ilidai kuwa imemuua kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa genge la kigaidi la al Ashabab na mkewe lakini shirika kubwa zaidi la mawasiliano la Somalia limekanusha madai hayo na kusema kuwa, aliyeuliwa katika shambulio hilo ni meneja wa kampuni hiyo, si kiongozi wa al Shabab na mkewe.
Jana Jumamosi, kundi la kigaidi na ukufurishaji la al Shabab ambalo limetangaza utiifu wake kwa mtandao wa kigaidi wa al Qaida lilisema kwamba, Marekani imekuwa ikiua raia wa kawaida kwenye mashambulizi yake nchini Somali kwa kutumia ndege zisizo na rubani (droni), na kisha kuhalalisha mashambulizi hayo kwa kusema kuwa imelenga ngome za magaidi
Taarifa hiyo iliyosainiwa na msemaji wa al Shabaab, Ali Muhamud Rageh 'Ali Dhere' imedai kuwa, asilimia 82.7 ya mashambulizi ya droni za Marekani ndani ya miezi 34 iliyopita nchini Somalia yamelenga raia wasio na hatia
Sent using Jamii Forums mobile app