Meneja Tanesco Arusha Matatani kwa kuwahonga wahariri Mamilioni

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Meneja wa Tanesco Mkoa wa Arusha, Herini Mhina huenda akajikuta matatani kufuatia matumizi Makubwa ya fedha za shirika hilo katika kuidhinisha malipo ya posho za wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ili wamsafishe na kumfagilia meneja huyo na shirika lake.

Hivi karibuni wahariri hao kutoka jijjni Dar walifika katika shirika hilo jijni hapa kwa mwaliko wa meneja huyo kwa ziara ya Siku kumi kwa ajili ya kutembelea miradi ya shirika hilo na kuacha kuandika mabaya .

Kwa mujibu wa taarifa za ndani meneja huyo aliidhinisha posho ya sh, milioni 2.5 kwa kila siku kwa mhariri mmoja kwa muda wa siku kumi walizokuwa katika ziara ya shirika hilo.

Wafanyakazi wa shirika hilo waliokerwa na ufujaji huo wa fedha hizo wamedai kuwa meneja wao amewaita wahariri hao ili walifagilie shirika hilo kwa Rais Magufuli ili lionekane lina fanyakazi vizuri mkoani Arusha, wahariri hao wakipewa jukumu la kumfagilia meneja huyo aonekane anachapa kazi na kupandishwa cheo.

Hata hivyo hivi karibuni mambo yameanza kumwendea kombo meneja huyo baada ya tume Maalumu kutua jijini hapa na kuwahoji baadhi ya wanahabari kuhusiana na malipo hayo na utafunaji wa kitita hicho cha fedha kwa wahariri hao na matumizi mengine yasiyosawa.

Baadhi ya waandishi wa habari waliokuwepo kwenye ziara hiyo ambao wamekiri kuhojiwa juu ya fedha hizo kutoka jijini Arusha wapatao watatu kutoka ITV akiweno mpiga picha na Mwananchi walijikuta wakiambulia kiasi cha sh,300 kwa siku huku katika dokezo la posho yao kila mmoja ikionyesha amelipwa sh,milioni 2.5 .

Hatua hiyo iliwafanya baadhi yao walalamike ndipo walipoitwa na kuongezew sh, 300,000 nyingine huku wakiambiwa wanyemaze kwani kazi ni nyingi na zinaendelea.

Baadhi ya wafanyakazi hao wameiomba serikali ya Magufuli kuchunguza matumizi ya shirika hilo kwani limeshindwa hata kutoa gawio la maana serikalini lakini fedha nyingi zinaishia kulipana posho kwa lengo la kuwanufaisha wachache waonekane wanachapa kazi.
IMG-20191126-WA0002.jpeg
 
Ukosefu wa ajira unaongeza wapika majungu. Mwandishi toka DSM muda wa siku kumi akilipwa TZS 2,500,000 kwa kuifanyia kazi shirika kuna hujuma gani? Hiyo si posho ya 250,000 kwa siku kwa ajili ya chakula na malazi?
 
Something went wrong somewhere...
Hebu weka taarifa sawa
Is it;
2,500,000 ×10=25,000,000 au
250,000×10= 2,500,000

Taarifa za namna hii ni za kutafutana ndani kwa ndani!!

Lkn ukweli utajulikana!!
 
Hii taarifa sio sahihi.

Waandishi 10x2,500,000x10days=250,000,000.
Bado posho na matumizi mengine, hii ni kama milioni 300, hii sio kweli.

Wafanyakazi kama mna shida na meneja muandike taarifa sahihi dhidi yake na sio uzandiki, fitina na roho mbaya juu ya mshikaji.
 
Back
Top Bottom