Mene Mene Tekeli na Peresi: CCM vipi mmekosa msomaji na mtafsiri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mene Mene Tekeli na Peresi: CCM vipi mmekosa msomaji na mtafsiri?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by fredmlay, Apr 19, 2012.

 1. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Upepo wa siasa Tanzania umeshika kasi na mageuzi yamepamba moto, mwenye macho anaona mwenye akili anajua tunakoelekea, hakuna maajabu kama viongozi wa ccm kujifanya wao niwajuzi sana wa mambo, hupenda kujibu majibu mepesi kwa maswali mazito, kucheka wakati wa kuhuzunika na hata kufungua champagne wakati risasi zinarindima..! Kweli hawa jamaa wamechanganyikiwa.

  Tangu wiki iliyopita siasa za Tanzania zimeshuhudia makada wa CCM wakikimbia chama hicho lakini ajabu ni kwamba viongozi wa chama hicho wamekuwa majasiri kama mfalme Belshaza wa Babeli, alikuwa kwenye sherehe wakati majeshi ya adui yamezunguka ngome yake, Mungu anamfunulia linaloenda kutokea kupitia maandishi ukutani lakini Daniel anapoyasoma na kutafsiri yeye bado anammegea ufalme wake.

  James Millya amekihama chama hicho, lakini ajabu viongozi wa CCM wanaibuka na kusema alikuwa mzigo, yeye ni gamba nk, bila kufikiri athari za lugha wanazotoa (maana watanzania wanatafakari) wameendelea kujichanganya kwa staili hiyo.. hebu tujiulize yawezekanaje wewe uliyepewa dhamana ya kutuongoza ushindwe kuwawajibisha viongozi wabovu, wezi, mzigo nk? Kisha kafuatia Katibu Mwenezi-Longido kujiuzulu na leo Mh Mawazo (Diwani-Sombetini Ar) naye kafuata mkumbo, lakini ajabu lugha za viongozi wa ccm ni zile zile tena ajabu zaidi ni pale katibu mwenezi mkoa wa Arusha leo aliposema Mh. Mawazo ni sawa na sisimizi kwenye mbuga ya Serengeti!

  Ndugu zangu CCM maandishi yapo ukutani nyie mwafanya mzaha? Kama mmeshindwa kuyasoma kwanini msimtafute Daniel akawasomea ili ikiwezekana muepukane na kikombe hiki?
   
 2. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mtu kama Daniel wa Nebukadneza hayuko CCM na kama yupo anakula na kipofu.
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,336
  Likes Received: 22,188
  Trophy Points: 280
  CCM haijalala, imezimia. Kwenye kuzimia hakuna maono, dira wala mwelekeo.
   
 4. M

  MalikwaMali Member

  #4
  Apr 19, 2012
  Joined: Mar 30, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Piano piano. Poko poko.
   
 5. d

  dada jane JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole zao waendelee tu kunywa mvinyo kwenye vyombo vya utakaso.
   
 6. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #6
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Walioko ndani ya CCM nao wanatakiwa kujiuliza,Je wao sio mizigo?
   
 7. M

  Mwonambali Member

  #7
  Apr 19, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "A wise man will make more opportunities than he finds"
   
 8. M

  Mchokozi JF-Expert Member

  #8
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa mtikisiko huu wengi watazidi kusepaa!!!!!!
   
 9. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #9
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Tayari mwingine kasepa leo tena ni diwani huko Mwanza.. tutaona mengi..
   
 10. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #10
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kwao kila anayetoka alikuwa mzigo sasa unajiuliza vipi wasimtoe mpaka wasubiri atoke? Mbona kama ndivyo wanatubebesha mzigo tusio stahili?
   
 11. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #11
  Apr 19, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,929
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  [​IMG]


  Unajua kuna kitu hapa naona kama vinafanana!

  Kwanza wakati wa yale maandishi yanaandikwa ... Mfalme Belshazzar alikuwa katikati ya KARAMU (feast) ambapo walikuwa wanakula na kunywa na kuponda raha ... mara wakiwa hawana hili wala lile ghafla maandishi yakaanza kuandikwa ukutani! ... Mene Mene Tekel Upharsin!

  CCM nayo wakati huu wapo kwenye KARAMU ya kula na kunywa na kusaza utajiri wa nchi yetu huku wananchi wakiwa wanalia kuwa hali ni mbaya ... jamani jitahidini kurekebisha maisha bora .... lakini hawa CCM wamekuwa kama enzi ya Mfalme Belshazzar ... wanakula tu! ... wapo KARAMUNI wanajichana! ... wala hawawajali wananchi wa kawaida... watu wakipiga kelele wanaambiwa aah .. hizo ni kelele za mlango! ...


  Haya ndiyo maneno yaliyoandikwa:


  MENE, MENE, TEKELI NA PERESI.


  Hii ndiyo maana ya maneno haya:


  Mene: (CCM?) Mungu amezihesabu siku za utawala wako na kuukomesha.


  Tekeli: (CCM?) Wewe umepimwa katika mizani na umeonekana umepungua.

  Peresi: (CCM?) Ufalme wako umegawanywa na kupewa Wamedi na Waajemi. ... (Wamedi & Waajemi - CDM & ????)
  .
  For more consult Daniel 5


  Soma maana hapo juu na ulinganishe na CCM?


  Labda maandishi haya! ... naona kuna similarity! ...


  .
   
 12. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #12
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,898
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  siku zimewadia
   
Loading...