Men Talk 4: Mwanaume usitongoze kila mwanamke aliyekaribu na wewe, hata kama anavutia kiasi gani. Some are meant to be just friends

Analyse

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
8,373
2,000
Kipindi nasoma, naishi home kwa wazee, mfanyakazi wa ndani aligundulika ana mimba. Ikabidi ahojiwe muhusika ni nani. Ile nyumba watoto wa kiume tulikuwa watano ( kuna mtoto wa baba mdogo nae alikuja kutembea maana alikuwa likizo chuo). Kulingana na mazingira ya pale home, sio rahisi yule dada kutembea na mtu wa nje ya nyumba, kwahiyo ilo swala lilimpa mzee hasira sana, maana ilikuwa wazi muhusika wa ile mimba ni kati ya sisi watano.

Kikao kiliendeshwa na yule broh wa chuo, alimhoji maswali magumu sana yule binti, binti kazungukaa weee mwisho wa siku akanitaja mimi. Nilikataa kata kata maana nilikuwa najua anaongopa. Majadiliano yalikuwa mengi na marefu, ila ukweli ukaja kugundulika, aliyekuwa anaongoza mjadala (jamaa wa chuo) ndio muhusika wa ile mimba.

Baada ya siku mbili, mzee jioni moja akaniita. Tukawa tumekaa nje, tunaongea huku tunakunywa chai. Mzee alianzisha mada ambayo sikuitarajia. Aliniambia "Katika maisha, ukiwa kama mwanaume hutakiwi kutembea na kila mwanamke aliyekaribu na wewe, vinginevyo unaweza jikuta unapoteza watu muhimu sana ambao wangeweza kuja kuwa msaada kwenye maisha yako".

Tuliongea mengi, na alinipa hints nyingi sana. Ila wakati tunamalizia maongezi, akaniambia nilifanya kosa kutembea na yule mfanyakazi wa ndani. Nikashangaa why kasema vile. Halafu nikamkazia macho kwa msisitizo, huku nikikataa zile tuhuma. Nilimwambia "Baba hadi wewe unaamini nilitembea nae?". Mshua alitoa tabasamu fulani hivi, ambalo naweza sema ni la huzuni, then akaniambia "MWANAMKE HAWEZI MSINGIZIA MIMBA MWANAUME AMBAE HAJALALA NAE". Nilijisikia aibu sana, nikaondoka.

Kiuhalisia, wanaume tumeumbwa na tamaa plus mioyo ya kutoridhika, hasa linapokuja swala la mapenzi na wanawake. Utaoa leo, ila kesho mate yatakutoka ukipishana na zigo jingine njiani

Ila from real life experience, naweza washauri sio kila mwanamke mzuri anayekuwa in your life circle lazima upite nae. Why nawaambia hivi??

Wote tunajua, ni nadra sana kukuta marafiki wa kawaida wa jinsia tofauti ambao hawana uhusiano wa kimapenzi wananuniana au kuchuniana. Ukitembea na rafiki yako wa kike, basi jua umegain mpenzi, ila umepoteza rafiki.

Ukitembea na co-worker, basi jua umegain mpenzi na umepoteza co-worker. Ukitembea na mfanyakazi wako, jua umepoteza mfanyakazi na umeongeza mpenzi.

Wote tunajua, palipo na mapenzi lazima vifuatavyo viwepo:

1. Wivu kupitiliza
2. Kununiana bila sababu

Mapenzi yanapunguza sana ufanisi wa utendaji kazi, hasa endapo utataka kufanya vyote kwa pamoja (Rejea mfano wa Ngoswe).

Kuna ile dhana kwamba, ukiwa na ukaribu sana na demu halafu usimtongoze, atakuona nyuki wa mashine. Hizi kauli zimelostisha wana wengi sana. Unamtongoza demu anayekupaga deals, mkishakuwa wapenzi then mkagombana usitegemee akupe tena zile deal.

Hata uwe unatembea na pisi mpya kila wiki, hutoweza wamaliza wote, maana on everage wapo wengi kutuzidi. Japo Opportunities are endless, ila ukianza kutongoza kila unayemuona, slowly you will be blocking your connections.

Nakumbuka kipindi nilipoamua kuondoka home baada ya kugoma kusoma HKL. Mshua badala ya kunisihi nisikimbilie Dar na umri ule mdogo, tena bila ya kuwa na ndugu, yeye alinikumbushia tena hili swala, then akaendelea na mishe zake (nilisota sana huko nilipoenda, ila nikanyooka).

Wakuu, kuwa mwanaume ni pamoja na kusimamia unachokipigania, kuweza kucontrol hisia zako.

Regards.

Analyse.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom