MLAU
JF-Expert Member
- Aug 23, 2007
- 4,726
- 3,354
Najua ni mwaka 11 sasa tangu tujiunge na Jamii Forum enzi hizo inaitwa Jambo forum iliyoanzishwa na vijana wawili na kubadilishwa jina baadaye na kuitwa Jamii Forum.
Najua ni mengi tumejifunza humu ndani kupitia mada mbalimbali na hata kujua kama familia.
Nadhani kwa sisi tuliojiunga 2007 ni muhimu kutoa maoni,mawazo,ushauri kwa wengine pia kuhusu namna Jamii Forum inavyosaidia jamii kwa ujumla wake hasa hasa katika kujua haki za binadamu,taarifa kuhusu mwenendo wa Taifa letu na fursa mbalimbali zinazopatika nchini na nje ya nchi.
Ni muhimu kuondokana na tabia ambayo ilianza kujitokeza ya lugha chafu na hata kuonekana kama JF ina makundi katika mada kiasi cha kuanza kuonekana ni cha chanzo cha watz kutengana kwasababu tu tofauti za kiitikadi wakati sisi wote tunalipigania Taifa letu katika ustawi wa watu wake na usawa wa haki kwa kila mmoja.
Nawatakia kila la heri members wote wa JF lakini kwa sisi wa mwaka 2007 tuwe mfano katika mijadala na mada mbalimbali kwasababu ya uzoefu wetu ndani ya Jamii Forum.
Karibuni wote tuifanye JF kuwa kimbilio lakila mmoja katika kutaka kujua mambo mengi na taarifa mbalimbali za nchi yetu na dunia kwa ujumla.