Membe: Tulikuwa tunagongana angani utadhani nyumbani kuna moto

Big Mo

Member
Jul 28, 2015
96
95


Kwa ufupi

Asema anaunga mkono katazo la Rais Magufuli kwenda nje kwa asilimia mia kwa mia mbili.

Dar es Salaam
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amempongeza Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwa kupiga marufuku safari za nje ya nchi, akisema mawaziri na watendaji wa Serikali walikuwa wakigongana angani na ndege utadhani Tanzania ilikuwa ikiwaka moto.

Mbunge huyo wa zamani wa Mtama alisema uamuzi huo utaokoa fedha nyingi za Serikali na kumtaka Rais kushusha rungu hilo hadi kwenye mashirika.

Wakati Membe akieleza hayo, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alisema kila safari ya nje ina gharama yake na kila safari itakayofutwa zitapatikana fedha kusaidia masuala mengine ya maendeleo katika jamii.

Juzi, Dk Magufuli alipiga marufuku safari za nje ya nchi kwa watendaji na kwamba shughuli ambazo wangekwenda kuzifanya, kuanzia sasa zitahitaji kibali kutoka kwake au zitafanywa na mabalozi wa Tanzania walioko katika nchi husika.

Jana Membe alisema: ?...Tulikuwa tunagongana huko hewani utadhani huku nyumbani kunaungua moto. Tunapobaki huku ndani tunaokoa hela nyingi na nina hakika (Dk Magufuli) ataingilia hata kwenye mashirika. Kuna wakuu wao wanasafiri kila siku, nina hakika wataguswa katika hili. Lazima kuziokoa pesa za kufanyia shughuli nyingine mimi naunga mkono mia moja kwa mia hili.?

Alisema kitendo cha Rais Magufuli kufuta safari za nje hakina maana kwamba uhusiano wa Tanzania na nchi hizo unakufa. ?Hajakataza wageni, wafanyabiashara wa dunia wala wawekezaji kuja Tanzania, hata wawekezaji hawawezi kukataa kuja Tanzania waache gesi, dhahabu, almasi au tanzanite.?

Alisema wapo watu wanaodhani kuwa kauli ya Rais Magufuli itamhusu hadi Waziri wa Mambo ya Nje ?... atakwenda nje maana ukishamuita waziri wa mambo ya nje lazima aende nje. Dk Magufuli hawezi kusema hivyo. Hutasikia amekatazwa maana ndiyo wizara yenyewe na inashughulika na dunia.?

Alisema kauli hiyo pia haina maana kwamba Wizara ya Mambo ya Nje imefutwa kwa kuwa balozi za Tanzania zilizopo nje zipo chini ya wizara hiyo.

CHANZO: Mwananchi

 

Bill of Quantity

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
1,236
1,250
Papa kaingia mtoni... Lazima kinuke tu.

Najaribu kuwazia kwa speed hii ya magufuli isipokata moto, je upinzani 2020 watatuambia nini wadanganyika?
 

MeinKempf

JF-Expert Member
Jun 11, 2013
11,117
2,000
Nimependa uungwaji mkono huo wa ndugu membe, huo ndio
ukomavu wa kisiasa na kidplomasia.
 

ze keke

JF-Expert Member
Aug 20, 2012
398
250
wanafki kazini! he was at ths post for ten years, alishindwa nn kumshauri JK
 

Big Mo

Member
Jul 28, 2015
96
95
/Kaka aliwaambia - Kule nje wanahela nyingi ni sisi tu kweda kuwaomba watupe -tule - wakawa wanatuma mpaka maafisa kwenda kuomba mikopo nje- sasa deni tr.45- sijui tutarudishe
 

H20

JF-Expert Member
Jun 4, 2013
341
170
Mbona Mapadlock alikuwa anaunga mkono safari za JK akisema zilikuwa na tija? Au alikuwa mnafiki? Kwanini hakupinga akiwa waziri?
 

sawabho

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
5,283
2,000
Papa kaingia mtoni... Lazima kinuke tu.

Najaribu kuwazia kwa speed hii ya magufuli isipokata moto, je upinzani 2020 watatuambia nini wadanganyika?
Mkuu, lakini hii ya kufuta safari za nje ilikuwa midomoni mwa Wapinzani muda mrefu tu. wamekuwa wakipigia kelele kuwa safari hizo hazina tija, hebu angalia viongozi wetu wanasafiri kila siku nje lakini hajui hata jinsi ya kupunguza foleni Jijini Dar, kwa hiyo Mhe. Magufuli ametekeleza ushauri wa muda mrefu kutoka kwa Wapinzan.
 

babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
4,527
2,000
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, BernardMembe amempongeza Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwa kupigamarufuku safari za nje ya nchi, akisema mawaziri na watendaji wa Serikaliwalikuwa ?wakigongana? angani na ndege utadhani Tanzania ilikuwa ikiwakamoto.


Fidelis Butahe, Mwananchi

Dar es Salaam. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe amempongeza Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwakupiga marufuku safari za nje ya nchi, akisema mawaziri na watendaji wa Serikaliwalikuwa ?wakigongana? angani na ndege utadhani Tanzania ilikuwa ikiwaka moto.

Mbunge huyo wa zamani wa Mtama alisema uamuzi huo utaokoa fedha nyingi zaSerikali na kumtaka Rais kushusha rungu hilo hadi kwenye mashirika.

Wakati Membe akieleza hayo, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefuealisema kila safari ya nje ina gharama yake na kila safari itakayofutwazitapatikana fedha kusaidia masuala mengine ya maendeleo katika jamii.

Juzi, Dk Magufuli alipiga marufuku safari za nje ya nchi kwa watendaji nakwamba shughuli ambazo wangekwenda kuzifanya, kuanzia sasa zitahitajikibali kutoka kwake au zitafanywa na mabalozi wa Tanzania waliokokatika nchi husika.

Jana Membe alisema: ?...Tulikuwa tunagongana huko hewani utadhani hukunyumbani kunaungua moto. Tunapobaki huku ndani tunaokoa hela nyingi na ninahakika (Dk Magufuli) ataingilia hata kwenye mashirika. Kuna wakuu wao wanasafirikila siku, nina hakika wataguswa katika hili. Lazima kuziokoa pesa za kufanyiashughuli nyingine mimi naunga mkono mia moja kwa mia hili.?

Alisema kitendo cha Rais Magufuli kufuta safari za nje hakina maana kwambauhusiano wa Tanzania na nchi hizo unakufa. ?Hajakataza wageni, wafanyabiashara wadunia wala wawekezaji kuja Tanzania, hata wawekezaji hawawezi kukataa kujaTanzania waache gesi, dhahabu, almasi au tanzanite.?

Alisema wapo watu wanaodhani kuwa kauli ya Rais Magufuli itamhusu hadi Waziri waMambo ya Nje ?... atakwenda nje maana ukishamuita waziri wa mambo ya nje lazimaaende nje. Dk Magufuli hawezi kusema hivyo. Hutasikia amekatazwa maana ndiyowizara yenyewe na inashughulika na dunia.?

Alisema kauli hiyo pia haina maana kwamba Wizara ya Mambo ya Nje imefutwa kwakuwa balozi za Tanzania zilizopo nje zipo chini ya wizara hiyo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom