Membe: Serikali haiwezi kurudisha kesi ya Ahmed Ghailan | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Membe: Serikali haiwezi kurudisha kesi ya Ahmed Ghailan

Discussion in 'International Forum' started by Pdidy, May 23, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,389
  Likes Received: 5,670
  Trophy Points: 280
  Membe: Serikali haiwezi kurudisha kesi ya Ahmed Ghailani [​IMG] Sadick Mtulya
  SERIKALI imesema, haiwezi kuiomba Marekani ihamishe kesi ya tuhuma za ugaidi inayomkabili raia wa Tanzania nchini humo, Ahmed Ghailani, kuja kuendeshwa nchini.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe aliiambia BBC jana kuwa suala hilo ni gumu kwa kuwa serikali haijawahi kufanya hivyo kwa Mtanzania yeyote.

  Alisema serikali ina takwimu ya Watanzania 101 walioko magerezani katika nchi mbalimbali duniani,lakini haijawahi kuziomba nchi husika ili kesi za Watanzania hao, zije kusikilizwa nchini.

  Ahmed Ghailani alikamatwa nchini Pakistani mwaka 2004 akihusishwa na ulipuaji mabomu katika majengo ya balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya mwaka 1998, kupelekwa katika kambi ya Guantanamo.

  Anatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya kirai ya jijini Newyork, Marekani siku yoyote kuanzia sasa kujibu mashtaka hayo.

  "Litakuwa jambo gumu kwa serikali kuomba mashtaka yanayomkabili Ghailani, yaje kuendeshwa nchini kwenye mahakama zetu kwa kuwa hatujawahi kufanya hivyo kwa Mtanzania yeyote," alisema waziri Membe.

  Kwa mujibu wa Waziri Membe, Tanzania inachoweza kufanya ni kuwasaidia Watanzania walioko magerezani, msaada wa kisheria kabla na baada ya kuhukumiwa.

  "Nchi yetu inaheshimu sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na nchi husika, na tunachoweza kufanya ni kumsaidia Ghailani na watanzania wengine waliokamatwa, kwa kuwapa msaada wa kisheria kama watakuwa wamekwisha hukumiwa au bado," alisema Membe.
   
 2. K

  Kjnne46 Member

  #2
  May 23, 2009
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Membe anayosema sio sahihi kwa sababu:

  1) Ghailani "anatuhumiwa" kuvunja sheria nchini Tanzania na Wamerika "wameshamtesa na kumfunga Guantanamo hata kabla hajahukumiwa". Eti sasa baada ya kelele za Wanaharakati wa Haki za Binadamu ndio anapelekwa mahakamani NY "kusikiliza kesi yake". Waache kuhadaa ulimwengu na wampe uhuru wake kijana wetu ameteseka vya kutosha!

  2) Hao Watanzania wengine 100 wamefanya makosa katika hizo nchi walizofungwa na ni kupotosha umma kusema wako kwenye kundi moja na Ghailani.

  3) Ile Sheria ya Ugaidi iliyotungwa Tanzania haraka haraka na Mhadhamu Ben Jamin Mkapa ina kazi gani kama si kuitumia kwa kesi kama ya Ghailani??

  "Usimwamshe aliyelala, la sivyo utalala wewe" - AL QAIDA ni wembe wa Marekani walioutumia kuwanyolea Warusi Afghanistan lakini baadae wembe ukawageukia na wanajifanya "sio mali yao"! NYUKI NA CHUKI WAMECHOKOZA WENYEWE NA SASA KULIKONI WANALALAMA??

  'Terrorism' is the hate we hate that created the hate we now hate !!!!
   
 3. B

  Bull JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2009
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwaiyo kama hawajawai kuwarudisha wa TZ waliomagerezani nje ya nchi ndo maana nikitu hakiwezi kufanyika? hawa ndo wale viongozi sikuzote nasema wamefubaa akili, tuanaitaji creative, innovative leader sio hawa wajinga wajinga wanaofanya mambo kwa kusukumwasukumwa. lo
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kuweza wanaweza. Angesema kwamba hawana nia ningeelewa. Lakini unategemea nini kutoka kwa kinara ambaye ameitaka Marekani ihakikishe Watanzania hawafi kwa njaa kana kwamba hiyo ni kazi ya Marekani badala ya serikali ya Tanzania?
   
 5. Mauza uza

  Mauza uza JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 2,050
  Likes Received: 744
  Trophy Points: 280
  Kweli bongo hatuna viongozi...kama hawajahi kufanya si huyu ndo angekuwa wa kwanza then waendelee na kwa wengine??Uk imechukua raia wake wote hata residents tu imewatetea warudishwe UK.Leo waziri mzima anasema hawajahi fanya kwa hio hawatofanya....mmm sielewi ni viongozi gani hawa tulionao...AIBU.:confused:
   
Loading...