Membe: Rais Mkapa alithamini sana matumizi ya akili kubwa katika uongozi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe amesema kuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa, alikuwa Kiongozi wa dunia, mshauri wa masuala ya Uchaguzi na kinara katika kulisaidia bara la Afrika kutatua migogoro bila kuchoka

Amesema siku zote Mkapa alikuwa anathamini akili kubwa, yaani kutumia maarifa katika kuongoza na alithamini sana nidhamu ya kazi na utekelezaji wa sera, sio mtu

Ameongeza kuwa "Tumezaliwa duniani lazima tufanye kazi kuwasaidia wananchi, Hayati Benjamin Mkapa alikuwa mtu wa dini sana na wazazi wake walitaka awe padri kama mimi wazazi wangu walivyotaka niwe padri lakini yalitushinda"

Membe amesema “Katika kipindi cha Uchaguzi kama hiki tumempoteza mtu aliekuwa ana-stabilize mambo ya Uchaguzi”
 
Back
Top Bottom