Membe ni muongo, Kikwete hakuvunja Baraza la Mawaziri: Raia Mwema 12-18/10 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Membe ni muongo, Kikwete hakuvunja Baraza la Mawaziri: Raia Mwema 12-18/10

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hossam, Oct 13, 2011.

 1. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,367
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  Nimesoma na kusikitika sana kauli ya membe kwenye gazeti la raia mwema la jana 12-18/10 kwamba eti namnukuu 'Unajua ili uweze kujibu swali hili lazima uangalie matukio ya mwaka 2008. Mwaka 2008 Rais Alivunja Baraza la Mawaziri, hadi Waziri mkuu, Lowassa, akaondolewa. Hakuna huruma hapo. Ameondoa mawaziri na waziri mkuu'. Hivi huyu ndio eti na yeye yuko mbioni kuusakanya urais wa Tanzania, kweli nchi hii ni ya vilaza kabisa.

  Mwaka huo huo, 2008 Lowassa alisema, 'Nimetafakari kwa makini suala hili na kwa niaba ya chama changu, nimemuandikia rais barua ya kuachia ngazi (kujiuzuru)'. Membe labda alikuwa kauchapa usingizi hapo.

  Kwa nchi kama Tanzania (URT) waziri mkuu akijiuzuru, cabinet nzima inakuwa imefikia tamati bila hata rais kupenda ama asipende. Kwa mujibu wa maneno potofu ya nachelea kusema huyo matamshi ya Membe yanadhihilisha ama Lowassa alilazimishwa kujiuzuru, ama aliambiwa afanye usanii kwa makubaliano fulani, ama wote hawaelewi nini kiliendelea.

  Nina wasiwasi ukimuuliza Membe hivi hii miaka 50 ya uhuru ni wa nchi gani, anaweza kukujibu harakaharaha 'Tanzania' badala ya Tanganyika.

  Miaka 50 ya umaskini, Tanganyika ya leo hata wembe inaagiza nchi za nje, kweli tunahitaji kusherekea miaka 50 yetu.

  Nafungua mjadala.
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Membe ni CCM kwanza kama JK na CCM lao .Membe ni waziri wa Nje mambo ya ndani kuyajua si rahisi labda alikuwa nje wakati Lowasa anaamua kumeza kaa la moto .Tanganyika ni Nchi gani ? Iko bara gani ? Yaanu hata wazanzibar wanatucheka kwa uhuni huu .Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania mh mshangao mkubwa .Hawa jamaa wana pupa then Lissu akisema juu ya Tanganyika wanasema Chadema wanataka kuuvunja muungano.Upuuzi mtupu .
   
 3. K

  Kasesela Member

  #3
  Oct 13, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwana JF, naungana na hoja yako mia kwa mia; hofu yangu ni weledi mdogo wa waandishi wetu. Hivi walio/aliye kuwa anamuoji hakuona upotoshaji wa Membe? Au ndiyo bahasha za kaki zinatumiwa kubomoana!
   
 4. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  karibu ndugu
   
 5. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Mhurumieni huyo Membe jamani si ajabu wakati Lowasa anajiuzulu alikuwa misele huko nje ya nchi..hivyo hakupata taarifa vizuri...teh teh heee
   
 6. Kitty Galore

  Kitty Galore JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  leo!!!
   
 7. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kazi kweli kweli..
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  Oct 13, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  URAIS MTAMU!!! Mtu anaweza kusema lolote ili mradi asafishe njia kuelekea magogoni!! Hivi pale magogoni na ile harufu ya soko la feri kuna raha gani?
   
 9. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #9
  Oct 13, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Jamani hebu kumbukeni vizuri, baada ya Mwakyembe kuwasilisha ripoti ya kamati ya richmond, kesho yake mtu wa kwanza kuchangia alikuwa Waziri Mkuu Lowasa, katika mchango wake akasema amemwandikia barua Rais ili ajiuzulu. Lakini kama kumbukumbu zenu zipo Rais hakumjibu Lowasa kumkubalia kujiuzulu na badala yake JK alivunja baraza la mawaziri na kubadilisha mawaziri. So ukweli ni kwamba Lowasa na mawaziri wengine walitimuliwa na JK wala sio kwamba alijiuzulu. Hata Karamagi aliyedai naye kaomba kujiuzulu ni kwamba walifutwa uwaziri. Membe yuko sahhi kabisa
   
 10. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  yale yale tu!!
  katibu mkuu anakuwa na kashfa, anastaafu kwanza ndo anapelekwa mahakamani.
   
 11. ipogolo

  ipogolo JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 4,090
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  rais anaweza kulivunja baraza lake la mawaziri endapo yafuatayo yatatokea:
  Kujiuzuru kwa waziri mkuu na mengineyo. kwa hiyo rais alivunja baraza la mawaziri. IF A=B,B=C THEN A=C FINITO.
   
 12. M

  Musharaf Senior Member

  #12
  Oct 13, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hizi ni siasa za kuchafuana tu na hazina mashiko yoyote. sasa mambo ya mwaka jana unatuletea leo?? hjata kama na sisi tukitaka kuona hiklo gazeti itakuwaje? ulikuwa wapi siku zote hizi kuyasema haya? au kwa sababu umetumwa kumchafua huyu? Je na mpuuzi mwingine akileta thread humu kwamba mwanahalisi la 2007 February, Lowassa alidanganya halmashauri ya Rungwe,, tuamini pia??acheni upuuzi nyie,, tuongee changamoto zilizopo na zinazokuja.
   
 13. B

  BMT JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  sipendi viongozi wanafki like membe,,,,,thread za leo kweli zote kali naomba na magogoni wazipate, ikiwezekana wachukue hatua kwa mtu kama mkulo aaaaaaaaaaaaaaaaachie ngazi
   
 14. M

  Musharaf Senior Member

  #14
  Oct 13, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hiyo tarehe uloiweka hapo 12/18/10 naamini kwamba unamaanisha December 18 siyo? Na sote tunajua kwamba Raia mwema hutoka kila siku ya jumatano. Sasa tarehe hiyo uloweka wewe mbona haikuwa Jumatano? hii tarehe ilikuwa jumamosi, wewe umetoa wapi hilo gazeti la Raia mwema la Jumamosi? N hata kama ulimaanisha kusema tarehe 12,, nayi haikuwa jumatano,, sasa kama si uongo na uzushi humu ndani kwa njaa zenu ni nini? N gazeti lenyewe ulifungiwa maandazi niini maana toka December hadi leo umelipekua ili ulisome utuletee upuuzi kuhusu Membe uliliweka wapi? Sote tunajua Raia mwema walikuwa hawako online by that time. Wewe ni mzushi,, MODs please toa hii thread ya majungu.
   
 15. M

  Musharaf Senior Member

  #15
  Oct 13, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wee nawe mbona unaingia kimugongo mugongo bila data wala taarifa zozote? unashabikia tu hata upuuzi. Kafanye utafiti ndipo ulete majungu yako hapa. Chundu kama nyie ndiyo mnalishushia hadhi jukwaa hili
   
 16. M

  Musharaf Senior Member

  #16
  Oct 13, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Waelimishe wabangubangu hawa wasio na data na vilaza wa katiba na sheria
   
 17. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2011
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,280
  Likes Received: 4,284
  Trophy Points: 280
  Naona hii ni wiki ya Membe
   
 18. M

  Musharaf Senior Member

  #18
  Oct 13, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ya nini kumhurumia kama kuna hoja ya ukweli?? Tatizo ni kwamba hakuna hoja hapa zaidi ya ushambenga tu. Watu hata tarehe wanazitunga haziendani na siku husika, na ninyi mnaojiita Great thinkers mnaamini tu na kushabikia kila upupu humu!! shame
   
 19. M

  Musharaf Senior Member

  #19
  Oct 13, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Cha msingi yaandikwe yenye ukweli na si umbeya na ushankumpe ambazo ni porojo tu za kupotezea muda. Zimejaa makandokando
   
 20. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #20
  Oct 13, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Mkuu unaangalia kalenda ipi? Yangu inaonuesha Jumatano. Jamaa yuko sahihi labda useme husomi sred sawasawa
   
Loading...