Uchaguzi 2020 Membe ni msafi sana, Lissu ana makandokando. Upinzani twende na Membe 2020

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,173
27,223
Habari zenu wana JF, leo ningependa kuzungumzia hawa watu wawili ambao wanaonekana wanaweza kupeperusha bendera ya upinzani.

Membe ni mtu mmoja msafi sana na hata umchafuaje hutaweza kwa kuwa ana utumishi uliotukuka na hii imepelekea kupata maadui wengi sana.

Upinzani kwa ujumla wake tunahitaji kuwa na Membe sasa kuliko wakati wowote ule, huyu ni mtu sahihi wa kutuvusha.

Membe sio mropokaji kama ilivyo Lissu, Membe ni msikivu sana na ana uwezo mkubwa sana wa kujenga hoja.

Lissu kwa sasa bado sana ana makandokando mengi sana ambapo ni ngumu kuaminika na kumnadi kwa wananchi, wengi mnakumbuka alivyochemsha kwenye sakata la mchanga wa madini na kusema Tanzania itashitakiwa MIGA kitu ambacho hakikuwa kweli.

Hivyo huyu sio mtu sahihi kabisa kwa upinzani wakati huu, hivyo ni bora na mara 100 tukamuunga mkono Membe.

Kwa pamoja upinzani tutashinda
#2020 upinzani twende na Membe#
 
Hapana, lengo ni kufika ikulu na tunahitaj mtu ambae atakuja na mtaji wa watu wa kutosha na mwenye ushawishi mkubwa. Hivyo mtu pekee wa kutupelema huko ni membe. Lissu bado sana
Sisi wapinzani asilia tunamhitaji mpinzani asilia ambaye ni Lissu. Huyo Membe ambaye ni mwanaCCM mpeleke Lumumba akashindane na Meko kwenye kura za maoni.
 
Mkuu kama uchaguzi ukifanyika bila tume huru basi wapinzani watachezewa rafu sana hatimae alieshindwa ndie atatangazwa mshindi, na kwa kuwa matokeo ya kura za Uraisi hayahojiwi mahakamani, basi huo ndio utakuwa mwisho wa mjadara.
 
Kwanini matokeo ya urais yasipingwe mahakamani?
 
Hapana, lengo ni kufika ikulu na tunahitaj mtu ambae atakuja na mtaji wa watu wa kutosha na mwenye ushawishi mkubwa. Hivyo mtu pekee wa kutupelema huko ni membe. Lissu bado sana
Ushawishi Upi Wa Kutangaza Maadui Na Kupishana Angani Na Kuikataa Katiba Ya Warioba?
 
Naomba ujivue hiyo ngozi fake ya kondoo uliyojivika plz.

Wewe siyo Mpinzani Bali Ni mpiga mapambio maarufu Sana kutoka pale Lumumba so toa unafiki wako hapa.
 
Habari zenu wana JF, leo ningependa kuzungumzia hawa watu wawili ambao wanaonekana wanaweza kupeperusha bendera ya upinzani.

Membe ni mtu mmoja msafi sana na hata umchafuaje hutaweza kwa kuwa ana utumishi uliotukuka na hii imepelekea kupata maadui wengi sana.

Upinzani kwa ujumla wake tunahitaji kuwa na Membe sasa kuliko wakati wowote ule, huyu ni mtu sahihi wa kutuvusha.

Membe sio mropokaji kama ilivyo Lissu, Membe ni msikivu sana na ana uwezo mkubwa sana wa kujenga hoja.

Lissu kwa sasa bado sana ana makandokando mengi sana ambapo ni ngumu kuaminika na kumnadi kwa wananchi, wengi mnakumbuka alivyochemsha kwenye sakata la mchanga wa madini na kusema Tanzania itashitakiwa MIGA kitu ambacho hakikuwa kweli.

Hivyo huyu sio mtu sahihi kabisa kwa upinzani wakati huu, hivyo ni bora na mara 100 tukamuunga mkono Membe.

Kwa pamoja upinzani tutashinda
#2020 upinzani twende na Membe#
Umetumwa?
 
Back
Top Bottom