Membe: Musiba na Mchange anayewatuma kunichafua kwanini hamnipeleki mahakamani? Kama mnaweza kunirekodi mmeshindwa nini kutoa huo ushahidi

ANAANDIKA MH. BENARD KAMILLIUS MEMBE, SIMBA WA RONDO.

Watanzania Wenzangu! Nawasalimia! Kwa siku tatu mfululizo magazeti ya makuhani wa fitina na
unafiki Musiba na Mchange na wenzao wamekuwa wakinishambulia kwa uchochezi wa sintofahamu
iliyotokea kuanzia Alhamisi tarehe 17 Octoba siku ambayo Mhe Rais ameondoka Lindi kuelekea Dar hadi Jumapili ya tarehe 20.

Mimi nipo Kijijini kwangu Rondo kwa mwezi mmoja sasa. Ni nini hicho nilichokisema au
kukiandika kwenye mitandao ya kijamii? Kwa kuwa mawasiliano yangu yote nayafanya kwa simu
yangu ambayo inasikilizwa na kudukuliwa, naviomba vyombo vinavyohusika vitoe hadharani
mazungumzo na maandishi yangu ili watu wasikie, wasome na wanihukumu.

Napenda niuhakikishie umma kuwa Mimi sikuwa mjinga! Nilijua kuwa nikisema au kuandika vibaya, wabaya wangu wataninyooshea vidole. Sikuingia kwenye mitego yao hiyo. Mimi kama Watanzania wote wenye akili za kawaida nilishangazwa sana na ukimya wa Serikali huku damage na rumours zikiwa zimetanda kote nchini bila kuzitolea maelezo kwa siku 3 mfululizo!
Mhe. Rais ni kiongozi wa Umma.

Inapotokea sintofahamu au upotoshaji wowote ule, ulikuwa ni wajibu wa Msemaji wa Ikulu au wa Serikali kukanusha na kuweka mambo sawa kama wanavyofanya siku zote. Vinginevyo wale wenye akili za mbilikimo na makuhani wa unafiki wanachukua mwanya huo kutunga ya kwao ili kumfurahisha Mhe. Rais.

Good governance requires quick response to rumours. Rumours left unattended damages governance! Narudia! Naviomba vyombo husika vitoe hadharani nilichokisema au kupost kwenye mitandao ili nihukumiwe na Wananchi wenyewe na sio na Wabwekaji wa Taifa. Ben Membe. Rondo- Lindi.

#NiguseNinuke2020
 
Membe arudishe tu mabilion ya Watanzania aliyopora kutoka libya

Jamhuri ikiamua kumshitaki atafilisika

Pia sio vizuri kuwatumia vijana kubweka mtandaoni kuisema serkali

Tuendelee kumuunga mkono mh Rais Kwa uchapa kazi
Mikocheni Junction ni boya tu mchimba chumvi
 
Hivi kiongozi mbobevu katika siasa za Tanzania kama huyu anaweza kuandika maneno ya kibaguzi na uzalilishaji wa watu kama huu? "Wenye akili za Mbilikimo". Kwani mbilikimo sio binadamu kama wengine? Unaweza kutumia udhaifu wa mwili wa mtu kumkashifu mwingine? Hii ni hatari. Siamini kama aliyeandika walaka huu ni yeye anayehusishwa kuuandika!! !
 
huyu ni "sizonji" aliyegoma kupeleka maendeleo kaskazini nani mbaguzi?
 
Ni kiswahili tu, nadhani alikuwa ana maanisha mbilikimo wa akili
 
huyu ni "sizonji" aliyegoma kupeleka maendeleo kaskazini nani mbaguzi?
Wachaga mna shida sana! Hivi hii nchi ni yenu pekeenu?

Alafu kwa nini wanaolalamika ubaguzi wa Rais ni wachaga tu,? Yani katika makabila zaidi ya 200 wachaga tu ndio wanalalamika mna nini nyie?
Acheni upumbavu bwana
 
Who is musiba kwenye determination zake yule sawa na debe tupu msaka tonge kwa jamii ya wasioelimika ndo wawezamuelewa
Sasa kama ni hivyo kwa nini huyu jasusi mbobevu anatapatapa kumjibu?

Yani Membe ndio wa kujibishana na kina Musiba?
Kweli dunia haijawahi kuwa Sawa aisee.
 
Back
Top Bottom