Membe: Magufuli anawafukuza watumishi kiurahisi kwakuwa hakuwateua yeye

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Asema Rais Anawafukuza Watumishi Kiurahisi Kwa Kuwa Hakuwateua Yeye

Wiki hii ilikuwa wiki ambayo waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ameeleza mengi yaliyoteka vichwa vya habari.

Kati ya mambo aliyozungumzia ni pamoja na uamuzi wa Rais John Magufuli kuwasimamisha na kuwafukuza kazi baadhi ya watumishi wa umma.

Membe ambaye aliwania nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, amekaririwa na gazeti la Mwananchi akieleza kuwa ni rahisi kwa rais Magufuli kufanya hivyo kwa sababu watu anaowasimamisha hakuwateua yeye kwa sababu hawafahamu.

“Ni rahisi kumshughulikia mtu usiyemfahamu, lakini sio rahisi kumshughulikia unayemfahamu. Kwake kufanya hivyo ni rahisi kwa kuwa pia ni rahisi kuwashughulikia watu usiowajua kuliko watu unaowajua, lakini hebu tuone kama atafanya hivyo pia kwa hao aliowateua mwenyewe,” Membe alisema.
 
membe kaongezeka kiakili anaongea point,hebu jiulize mbona jp hajaigusa wizara ya ujenzi inamaana ni takatifu?
 
Sasa labda tumuulize ye membe alikuwa anatakaje? Mbona mkwere kateua serikali ya kishkaji mpaka siku anaondoka ikulu? Huyu membe hataki magufuli nae aunde serikali yake?
 
tukii pata watu kama akina membe 1000 tutaendeleaa ..in life we need challenges kumbuka bila challenge hata magufuli asingekuwa raisiii.. namsapoti membe kwa sababu atamfanya magufuli asijisahau kama yule naniiiii alotoka juz ikul...........
 
Asema Rais Anawafukuza Watumishi Kiurahisi Kwa Kuwa Hakuwateua Yeye

Wiki hii ilikuwa wiki ambayo waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ameeleza mengi yaliyoteka vichwa vya habari.

Kati ya mambo aliyozungumzia ni pamoja na uamuzi wa Rais John Magufuli kuwasimamisha na kuwafukuza kazi baadhi ya watumishi wa umma.

Membe ambaye aliwania nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, amekaririwa na gazeti la Mwananchi akieleza kuwa ni rahisi kwa rais Magufuli kufanya hivyo kwa sababu watu anaowasimamisha hakuwateua yeye kwa sababu hawafahamu.

“Ni rahisi kumshughulikia mtu usiyemfahamu, lakini sio rahisi kumshughulikia unayemfahamu. Kwake kufanya hivyo ni rahisi kwa kuwa pia ni rahisi kuwashughulikia watu usiowajua kuliko watu unaowajua, lakini hebu tuone kama atafanya hivyo pia kwa hao aliowateua mwenyewe,” Membe alisema.
Lumumba hureeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Dah hiyo ni harufu ya ufisadi na wivu juu. Mbona haelezei juu ya uharibufu na upoteaji wa mali ya umma katika kipindi kilichopita. Wakina Lowasa wako wengi tu.
 
Jamani Membe tena!!!!!! Nahisi milembe ina mteja hivi karibuni. Kwani watumishi waliofukuzwa na waliobakishwa toka kwa mtangulizi wake wapi wengi? Najua wazi waliobaki ni wengi
Swali la kujiuliza ni kwa nini walifukuzwa? Ni wazi walikuwa na vi kashfa . Membe una bahati kwa kale ka kashfa ketu kuhusu dola za yule kanali mvaa kilemba lazima ungefukuzwa km hao wenzio na hakuna namna ya kubishi
 
Mimi ninacho jiuliza je Membe kajipima na kujiona
'anam mudu Magufuli'?

manake wengi wanatamani kumkosoa Magufuli hadharani lakini ujasiri tu hawana
wanabakia kusema 'Rais anafanya kazi vizuri tumuunge mkono'
wanaomsifia magufuli kwa kila kitu wanampotosha njia kwangu mimi amefanya makosa makuu 6 tangu aingie madarakani
 
Membe ni jasiri siku zote.
Anawajua mafisadi wote na anaona kuna wanaotumbuliwa na wengine wanaachwa kwa kujuana.
Yuko sahihi kukosoa.
 
Back
Top Bottom