Membe kufukuzwa uanachama wa CCM, je madai yake kuwa Katiba ya chama chake ilivunjwa ni ya kweli?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,177
2,000
Tumemsikia wenyewe aliyekuwa mwanachama wa CCM, Bernard Membe akidai kuwa katika kufukuzwa kwake CCM, Katiba ya chama chake haikuzingatiwa

Kwa maelezo yake, kikao pekee chenye uwezo wa kumfukuza mwanachama yeyote wa CCM, ni Halmashauri Kuu ya CCM, jambo ambalo haliikufanyika, badala yake ni kikao cha Kamati Kuu (CC) ya CCM kilichojitwalia mamlaka hayo ya kumfukuza yeye uanachama, jambo ambalo aliliita ni la kuvunja Katiba ya chama chao waziwazi

Kutokana na maelezo yake mwenyewe, Bernard Membe, alieleza kuwa mchakato wa kumfukuza kwenye chama hiko cha CCM, bado haujakamilika, kwa vile kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) bado hakijaketi ili kubariki uamuzi huo wa Kamati Kuu ya CCM.

Maswali ya kuwauliza wajumbe wa kikao hicho cha Kamati Kuu ni haya, je ni kweli madai ya Membe kuwa alifukuzwa uanachama wa CCM na kikao ambacho hakina mamlaka hayo kikatiba?

Kama ni kweli, ni kwanini kikao hicho cha chama kikongwe barani Afrika, kifanye kitendo hicho cha kuvunja Katiba yake yenyewe?

Je chama hicho kimeanza kuvunja Katiba ya Chama chake, kama "walivyozoea" kuvunja Katiba ya nchi waziwazi?

Baba wa Taifa hili, Mwalimu Nyerere aliwahi kutamka wakati akiwa hai kuwa mtu anayeanza kula nyama ya mtu hataacha kamwe!

Je ni kweli baada ya CCM kuanza "kuisigina" waziwazi Katiba ya nchi, sasa wameamua kuanza "kuisigina" Katiba ya Chama chao cha CCM?

Ningependa nijibiwe hayo maswali yangu machache.
 

Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
5,721
2,000
Mystery,
Katiba si ipo, nenda kaisome kisha utuletee majibu ikiwa ni kweli alichosema Membe ni kweli ama la. Sasa Membe analalama, wewe nawe unaendeleza hayo ila kwa mfumo wa swali. Huu ni uzembe, kasome katiba upate jibu, ingia google kisha tafuta katiba ya CCM.
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,177
2,000
Katiba si ipo, nenda kaisome kisha utuletee majibu ikiwa ni kweli alichosema Membe ni kweli ama la. Sasa membe analalama, wewe nawe unaendeleza hayo ila kwa mfumo wa swali. Huu ni uzembe, kasome katiba upate jibu, ingia google kisha tafuta katiba ya CCM.
Bill
Ubaya wenu nyinyi wana-ccm wa utawala huu wa awamu ya tano, ni kujimwambafai, kama alivyoeleza Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete

Hili ni Jukwaa huru la kujadiliana, sasa ni kwanini wewe hutaki majadiliano hayo tuyafanye hapa JF?
 

Tsitingile

Member
Sep 25, 2018
90
125
Mystery,
Katiba si ipo, nenda kaisome kisha utuletee majibu ikiwa ni kweli alichosema Membe ni kweli ama la. Sasa Membe analalama, wewe nawe unaendeleza hayo ila kwa mfumo wa swali. Huu ni uzembe, kasome katiba upate jibu, ingia google kisha tafuta katiba ya CCM.
Kama huwezi kujadili kaa kimya bloodfootball
 

Savimbi Jr

JF-Expert Member
Sep 23, 2011
4,818
2,000
Membe kilichomponza ni nia ya kugombea urais 2020 kuchuana na JIWE ndani ya chama chao.
 
Top Bottom