Membe kubali yaishe!

6 July 2020
Lindi, Tanzania

MEMBE baada ya kurudisha kadi ya CCM/tutajiunga na chama tutagombea uongozi wa juu tutashinda
Bernard Carmillus Membe akiwa kijijini kwake Rondo mkoani Lindi kusini mwa Tanzania aongea mazito baada ya kuiacha CCM kwa kurudisha kadi ya uanachama.


Alihudumu chini ya Rais Jakaya Kikwete kama Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania kwa miaka 10. Pia alipata kuwa mbunge wa CCM jimbo la Mtama mkoani Lindi. Alihudumu kama afisa mwambata wa ubalozi wa Tanzania kwa miaka 10 huko Canada ktk bara la Marekani ya Kaskazini. Pia alipata kuwa Afisa Mchambuzi wa ripoti ktk Kurugenzi ya Usalama na Intelejensia wa Taifa TISS katika Ofisi ya Rais.

Hali ya kisiasa mikoa ya Lindi na Mtwara na kwingineko Tanzania kwa ujumla inaonesha waTanzania wapo tayari kwenda na Bernard Membe ili kuweza kuweka sawa masuala ya kama kilimo, uvuvi, mifugo, gesi na Maendeleo ya Watu.
Source : Gilly Bonny Online TV
 
Lolote lawezekana kumbuka walioondoa vyama vingi Tanzania ndio hao hao waliovirudisha kwa kupenda au kwa kutokupenda.
Na ndio haohao WANAOWEWESEKA MAKADA WAO WAKIJIUZULU AU AKIENDA UPINZANI...
NI NINI KINACHOWATIA KHOFU?
 
Mwache atimize takwa la kidemokrasia
Vipi mzee Sumaye hakuutaka uenyekiti tena huko ccm, au aliutaka wa Chadema tu?!

Na vipi Mwambe alijaribu kugombea uenyekiti wa ccm taifa au naye alikuwa katumwa tu kujaribu kule Chadema?!

Watia nia urais Tanganyika 2015 walikuwa 42, mwaka 2020 mtia nia 1 ccm, lakini tizama majimboni unakuta jimbo moja watu 50 ccm, demokrasia inawashindaje?!
 
Back
Top Bottom