Membe: Kama Magufuli Angekuwa Hai 'Nisingerudi' tena CCM

Annunaki

JF-Expert Member
Dec 30, 2021
1,911
3,171
Membe ametoa kauli hiyo leo wakati akifanya mahojiano na mtangazaji wa DW katika kipindi cha kinaga ubaga.

Membe amesema kama Magufuli angekuwa bado yuko hai asingerudi CCM tena, huku neno 'nisingerudi' akilitamka mara tatu kwa msisitizo.

Membe amesema amerejea CCM baada ya kuombwa na sekretarieti ya chama arejee tena CCM, hivyo akaiandikia kamati kuu ya ccm barua ya kurejea ,huku akienda mbali zaidi na kuhisifu awamu ya sita akisema Rais Samia ameleta 'governance' katika uongozi wake.

Ameendelea kusema kuwa kilichomuondoa CCM wakati wa uongozi wa hayati Magufuli ni kuguswa kwa maslahi yake ya kisiasa.

Kuhusu namba ya kadi aliyopewa baada ya kurejea tena CCM, Membe amesema kwa sasa chama kinatoa kadi mpya za kielektroniki, hivyo hajabainisha wazi ni kadi namba ngapi amepewa.

Alivyoulizwa tena kuhusu ndoto yake ya Urais, Membe amesema kwa sasa hayupo tayari kwani muda umemuacha na 2025 Samia anatosha.

Ikumbukwe Membe amerejea CCM tena.
 
Aliwahi kusema "niguse ninuke" lakini alipoguswa hakunuka hata kwao Londo. Mwamba kalala walioufyata sasa wanasema. Kabla yake, Nap alitembea,kwa magoti ikulu kisha baadae alipohojiwa akasema amefurahi kuonana,na baba lakini juzi tumemsikia alichosema dhidi ya mtu aliyemsujudia na kumuita baba.
 
'governance'

AxVmM9o (1).gif
True!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom