Serikali imesema haijapata taarifa za Waziri wa Ulinzi wa Israeli, Ehud Barak, kutoa matamshi kwamba Tanzania sio nchi muhimu kwake. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu kauli hiyo jana kwa njia ya simu, alisema kwamba hajapata taarifa kamili kuhusu suala hilo.
Hata hivyo, alitaka apigiwe simu jana mchana, lakini alipopigiwa simu yake ya mkononi ili kueleza msimamo wa serikali, simu yake iliita bila kupokelewa. Kauli hiyo kwamba Tanzania si muhimu kwa Israeli ilitolewa na Waziri Barak alipofanya mahojiano na Radio Israel na kunukuliwa na vyombo vingine vya habari vya nchi hiyo wiki iliyopita. Waziri Barak alitaja nchi muhimu na zenye maslahi kwa Israel kuwa ni Ujerumani, Uingereza na Ufaransa na siyo baadhi ya nchi maskini, ikiwamo Tanzania.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa wa Chadema, John Mnyika, alisema kupitia kauli ya kiongozi huyo wa serikali ya Israel, inaiona Tanzania sio nchi muhimu. Tunamtaka Waziri wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa, Bernard Membe kuitaka serikali ya Israel kuomba radhi kufuatia kauli hiyo au kueleza wazi iwapo mazungumzo hayo ya Waziri Barak ni msimamo wa nchi hiyo kuhusu uhusiano wa kidiplomasia wa mataifa yetu, alisema Mnyika.
Chanzo: Nipashe
UPDATE
And the deputy minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Mr Mahadhi Juma Maalim, told The Citizen Tuesday that the government has taken the issue seriously and is holding consultations over recent derogatory remarks.
We are holding meetings to see how we can respond to Mr Baraks comments. We will let you know when we are ready, he said during a telephone interview. Mr Barak has refused to apologise to Tanzania after branding the country as irrelevant as far as Israels relations with other nations are concerned.
Source: Israel
Mkuu,
Asante kwa mkeka huu. Uelewa wangu mdogo wa masuala ya mambo ya nje na diplomasia unanifanya nielewe sababu ya Serikali yoyote makini kutokurupuka kutoa tamko kujibu kauli iliyotolewa na Ehud Barak. Kwanza yafaa tujiulize, Mauritania ambayo nayo imetamkwa na Bw. Barak nayo imetoa tamko? Kama haijato bas kuna fumbo.
Fumbo la kwanza ni kuwa, Serikali yoyote makini haiwezi kukurupuka kujibu kauli ya Waziri wa Ulinzi ambaye kimsingi hana mamlaka ya kutamka msimamo wa nchi yoyote. Katika nchi yoyote dniani kuna sera mbili kubwa, Sera ya Ndani inayojumuisha sekta zote ikiwemo Ulinzi na Sera ya Nje. Kauli rasmi juu ya msimamo wa nchi hutolewa na Waziri au Wizara ya Mambo ya Nje na si vinginevyo. Ni sawa na kwenye familia, kauli ya baba ndio kauli rasmi, hauwezi kuchukulia kaul ya mtoto kuwa sehemu ya familia ingawa huwezi kuipuuzia maana inawakilisha discontect ndani ya familia. Hivi ndivyo ilivyotokea Israel. Kauli ile ingetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje bila shaka Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ingejibu haraka na mapema iwezekanavyo ikiwemo kuchukua hatua;
Fumbo la Pili ni kuwa mahala kauli yenyewe ilipotolewa inawakilisha uzito wa kauli yenyewe. Kauli yenyewe ya Waziri Barak ameitolea kwenye kipindi cha radio ndani ya Israel akihojiwa na wala si kwenye Mkutano wa Kimataifa. Katika Mkutano wa Kimataifa, Waziri wa sekta yoyote anaweza kuiwakilisha nchi na kutoa msimamo wa nchi kwa niaba ya Serikali yake. Ndio maana wanapoenda kwenye mikutano ya kimataifa, mawaziri hupewa hati za uwakilishi(credentials) ambazo hutambulisha mawaziri hao kuwa ni wawakilishi halali wa nchi, hati hizo husainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje au Rais wa Nchi. Na kama kunahusisha kusaini Mkataba wowote wa Kimataifa, basi Waziri huyo kama ni Waziri mwingine tu (kwa maana si Waziri wa Mambo ya Nje )hupewa "Instrment of Full Powers" hati ambao humuwezesha kusaini Mkataba kwa niaba ya nchi. Hivyo, mazngira aliyotolea kauli Bw. Barak hayakidhi haja kuwa alikuwa akitoa msimamo wa nchi bali maoni yake.
Katika mazingira hayo, nchi yoyote makini itawasiliana rasmi na Serikali mwenzake kupitia Wizara ya Mambo ya Nje kuuliza ikiwa kauli hiyo ndio msimamo kamili wa Serikali au la kabla ya kuchukua hatua yoyote. Nci kurupuka na kuanza kujibu kauli kitakachotokea ni Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi ile kukushangaa na kusema kuwa kauli rasmi ingetoka Wizara yao na si Wizara ya Ulinzi. Hivyo ndivyo Diplomasia inavyofanya kazi. Na kwenye Diplomacy mambo humalizwa kupitia njia za kidiplomasia (diplomatic channels) kwa kuwamlengo la msimgi la diplomasia ni kuboresha mahusiano na kinyume chake ni vita.
Katika hili naamini Wizara ya Mambo ya Nje inalifanyia kazi suala hili katika levels za kidiplomasia. Haiwezekani ikawajibika kwa hisia zetu tu zinazotokana na uelewa wetu mdogo wa sekta hiyo. Ni kawaida yet kuingilia masuala ya kitaalamu na kuweka emotions. Mfano ni kawaida kwa Watanzania kukosoa madaktari, makocha wa mpira na wataalamu wengine. Hatuna sababu ya kuingiza siasa kila mahala. Naamini kauli ile ingetolewa na Waziri Mkuu wa Israel au Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel naamini Tanzania ingeshuka kama nyuki kama ilivyofanya dhidi ya Waziri Mkuu Cameroon wa Uingereza. Na hapa si Waziri Mkuu pekee, bali Waziri Mkuu mwenye Executive Powers.
Siamini kama kuna mtu mzima humu hata mmoja mwenye busara na hekima atakayekwenda kugombana na jirani yake kwa matamshi aliyoyasikia kutoka kwa mtoto wa jirani. Kama hii ndio busara basi tunatatizo vichwani mwetu.