Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,264
- 105,428
I personally heard the talks between our Minister (Membe) and the BBC this morning. He really showed the kind of diplomatic leaders we are currently having; very bad.
Nilijiuliza, hivi huyo Balozi wa Libya anapaswa kutii mamlaka ya nani? (Balozi) Anajua fika bosi wake wa zamani (Gaddafi) hayuko tena madarakani na order imetolewa na watawala wapya (waasi), japo hawajaapishwa, juu ya mambo mbalimbali yahusuyo taifa lao ikiwamo kwa balozi za nje kupeperusha bendera mpya; hivi ni mpumbavu gani angekuwa na ujasiri wa kukataa agizo kama hilo? Nani asiyependa maisha yake, potelea mbali kazi?
Kitendo alichofanya Membe ni kibaya mno kiasi kwamba kinahatarisha hata usalama wa raia wa Tanzania na waafrika wengine waishio Libya kwa sasa. Kuna taarifa kwamba waasi wanawalenga waafrika weusi kwa madai kwamba wanmuunga mkono adui wao Gadafi kama ilivyopostiwa hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/167969-libya-rebels-now-target-%91blacks%92.html
Hivi waasi wakisikia statement ya Membe unategemea watawafnyia nini watanzania wenzetu waishio huko? Busara zaidi zitumike kwenye suala hili badala ya kujuana na ubabe wa kijinga.
Waasi wenyewe wamechemsha kwa kufanya mambo shaghalabaghala.
Balozi wa nchi anapotambuliwa na nchi nyingine hupeleka credentials zake Ikulu, huyu balozi wa sasa wa Libya alipeleka credentials za Gaddafi Ikulu, hao waasi hawajaleta balozi wao na credentials zao, kwanza hawana hata serikali.
The Libyan situation exposes a lot of hypocrisy.Mijitu imefanya kazi na serikali ya Gaddafi miaka yote, imeua naye, leo imeona Gaddafi anapigwa, imemgeuka. Hawa ma rebel wana risk kupigwa dafrao style ya Shibuda CHADEMA. Kwa nini wasiunde serikali kwanza, kuondoa mabalozi wa Gaddafi, na kuchagua mabalozi wao wapya?
Hawa mabalozi wa Gaddafi wanaojifanya kuuona mwanga dakika ya mwisho wakiwa wanavujisha habari muhimu za kidiplomasia kwa Gaddafi hawa waasi watafanyaje? Hapa naona inexperience tu.