Membe: CCM inajimaliza

Kuhani umemcritisize Membe Bure juu ya mfano wake kwa KANU ya Kenya, infact yeye ametoa mtizamo wake wa kisiasa, siasa za vyama, na wala hajaicritisize serikali ya Kenya kwa lolote. mimi nadhani hajavunja kanuni za diplomasia kwa mfano wake huo
 
Imetolewa mara ya mwisho: 09.12.2008 0158 EAT

• Makinda: CCM iko pabaya

*Awataka vijana kuchagua viongozi walio makini

*Mwenyekiti Njombe adai CHADEMA inasumbua

Na Francis Godwin, Njombe

NAIBU Spika wa Bunge, Bibi Anne Makinda, ambaye pia ni mbunge wa Njombe Kusini, amewatahadharisha wanaCCM kuwa makini katika kuchagua viongozi wa jumuiya zake na kwamba sasa chama hicho kiko pabaya na bila kuwa madhubuti nchi itayumba.

Bibi Makinda alisema hayo jana katika ukumbi wa UWT wilayani hapa wakati akitoa salamu kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) mkoa wa Iringa.

Alisema awali hali ya chama hicho ilionekana kuwa shwari kutokana na kutokuwapo misuguano wa kisiasa kama ilivyo sasa na kwamba ili kiendelee kuwa imara, lazima wanachama wachague viongozi makini watakaonadi vizuri sera za CCM ndani ya mfumo wa vyama vingi vya siasa.

"Chagueni kwa makini watu wa kuongoza Umoja wa Vijana, kwani vijana ndio mnatarajiwa kukiwezesha chama kupata ushindi...nasema tuko pabaya na tunakokwenda ni kubaya sana," alisema.

Alisema Rais Jakaya Kikwete alikuwa miongoni mwa vijana walioonesha mafanikio katika kuongoza nchi hii na kila mmoja amekuwa akipongeza jitihada zake anazozifanya.

Hata hivyo, Bibi Makinda hakufafanua kuhusu kauli yake ya chama kuwa pabaya, ila aliongeza kuwa Jumuiya ya Vijana ni tegemeo kubwa kwa CCM na kama vijana watafanya mchezo katika kuchagua viongozi chama kitakuwa katika eneo baya zaidi.

Awali akifungua mkutano huo kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Bw. Deo Sanga, Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Njombe, Bw. Adam Msigwa, alisema CCM imejipanga vyema kupambana na vyama vya upinzani na kuwa bado ushindi wa CCM 2010 ni mkubwa iwapo uchaguzi ndani ya chama utafanyika kwa umakini mkubwa.

Hivyo aliwataka vijana kuepuka kuchagua viongozi kwa misingi ya rushwa na badala yake waangalie uwezo wa mgombea, bila kuangalia rushwa aliyoitoa katika kuomba nafasi hiyo.

Aidha, aliwataka viongozi wa CCM kuepuka kuficha ukweli kuwa jina la chama hicho kwa sasa liko pabaya kwani kuendelea kuficha ukweli ni kukimaliza kabisa chama hicho.

"Jina la CCM liko pabaya sana tusifichane hapa...mfano Iringa Mjini nimeona mwenyewe katika televisheni, hali ya Iringa Mjini si nzuri ....CHADEMA inasumbua sana huko ...nendeni mkaseme katika kata zenu uwa CCM tuko pabaya, lazima tupambane na wapinzani," alisema.

Kauli ya Mwenyekiti huyo imekuja siku chache tangu viongozi wa CCM wilaya ya Iringa Mjini na Mkoa walipomdanganya Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuph Makamba, kuwa hali ya kisiasa wilaya ya Iringa mjini ni shwari na kuwa CHADEMA akiwamo Naibu Katibu Mkuu wake, Bw. Zitto Kabwe katika ziara yao ya Iringa waliambulia wanachama watatu pekee jambo ambalo si la kweli.

Kauli ya Bibi Makinda inakuja siku moja tu baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Benard Membe, kusema CCM inajimaliza yenyewe kutokana na kuendekeza makundi ndani yake.
 
Huyu Membe ni msanii kama bosiwake; kwani hayo makundi ndio ameanza kuyaona kwenye uchaguzi wa vijana, wakati wa mchakato wa 2005 ambao yeye alikuwa kinara lile genge lao la "MTANDAO" halikuwa kundi? Huyo ndio waziri wetu wa mambo ya nje; Asha Rose hakuwa anasema utumbo kam huyu bwana!!!.
 
CCM ni chama kikubwa sana na kina matabaka...Unaambiwa CCM ina wenyewe...Sasa Membe analia lia nini?
Kwani ccm ikifa Taifa nalo limekufa?
Eti Kenya na sijui KANU...Kwani KANU ilipokufa Kenya ilikufa?
Aaache utani bana CCM ama bila CCM taifa litasonga mbele tena may be minus ccm tunaweza kuwa na mafanikio zaidi.

Maneno machache lakini muhimu sana!
 
Kuhani umemcritisize Membe Bure juu ya mfano wake kwa KANU ya Kenya, infact yeye ametoa mtizamo wake wa kisiasa, siasa za vyama...

malizia, vyama vya nchi nyingine...

na wala hajaicritisize

amecriticize migawanyiko...

...serikali ya Kenya

Serikali ya Kenya inajumuisha watu wa KANU. Ukiingilia na ku criticize siasa za chama cha nchi jirani unakuwa umeingilia siasa za ndani za Kenya. Sio lazima umtukane Mwai Kibaki!!!

mimi nadhani hajavunja kanuni za diplomasia kwa mfano wake huo

Kwa standard zetu za bora liende ambapo Membe kaiita Irani "shetani," na amepeta, yes you're right. Kwa viwango vya world class diplomacy hiyo ni text book example of a diplomatic gaffe.
 
Imetolewa mara ya mwisho: 09.12.2008 0158 EAT

• Makinda: CCM iko pabaya

*Awataka vijana kuchagua viongozi walio makini

*Mwenyekiti Njombe adai CHADEMA inasumbua

Na Francis Godwin, Njombe

NAIBU Spika wa Bunge, Bibi Anne Makinda, ambaye pia ni mbunge wa Njombe Kusini, amewatahadharisha wanaCCM kuwa makini katika kuchagua viongozi wa jumuiya zake na kwamba sasa chama hicho kiko pabaya na bila kuwa madhubuti nchi itayumba.

Bibi Makinda alisema hayo jana katika ukumbi wa UWT wilayani hapa wakati akitoa salamu kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) mkoa wa Iringa.

Alisema awali hali ya chama hicho ilionekana kuwa shwari kutokana na kutokuwapo misuguano wa kisiasa kama ilivyo sasa na kwamba ili kiendelee kuwa imara, lazima wanachama wachague viongozi makini watakaonadi vizuri sera za CCM ndani ya mfumo wa vyama vingi vya siasa.

"Chagueni kwa makini watu wa kuongoza Umoja wa Vijana, kwani vijana ndio mnatarajiwa kukiwezesha chama kupata ushindi...nasema tuko pabaya na tunakokwenda ni kubaya sana," alisema.

Alisema Rais Jakaya Kikwete alikuwa miongoni mwa vijana walioonesha mafanikio katika kuongoza nchi hii na kila mmoja amekuwa akipongeza jitihada zake anazozifanya.

Hata hivyo, Bibi Makinda hakufafanua kuhusu kauli yake ya chama kuwa pabaya, ila aliongeza kuwa Jumuiya ya Vijana ni tegemeo kubwa kwa CCM na kama vijana watafanya mchezo katika kuchagua viongozi chama kitakuwa katika eneo baya zaidi.

Awali akifungua mkutano huo kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Bw. Deo Sanga, Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Njombe, Bw. Adam Msigwa, alisema CCM imejipanga vyema kupambana na vyama vya upinzani na kuwa bado ushindi wa CCM 2010 ni mkubwa iwapo uchaguzi ndani ya chama utafanyika kwa umakini mkubwa.

Hivyo aliwataka vijana kuepuka kuchagua viongozi kwa misingi ya rushwa na badala yake waangalie uwezo wa mgombea, bila kuangalia rushwa aliyoitoa katika kuomba nafasi hiyo.

Aidha, aliwataka viongozi wa CCM kuepuka kuficha ukweli kuwa jina la chama hicho kwa sasa liko pabaya kwani kuendelea kuficha ukweli ni kukimaliza kabisa chama hicho.

"Jina la CCM liko pabaya sana tusifichane hapa...mfano Iringa Mjini nimeona mwenyewe katika televisheni, hali ya Iringa Mjini si nzuri ....CHADEMA inasumbua sana huko ...nendeni mkaseme katika kata zenu uwa CCM tuko pabaya, lazima tupambane na wapinzani," alisema.

Kauli ya Mwenyekiti huyo imekuja siku chache tangu viongozi wa CCM wilaya ya Iringa Mjini na Mkoa walipomdanganya Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuph Makamba, kuwa hali ya kisiasa wilaya ya Iringa mjini ni shwari na kuwa CHADEMA akiwamo Naibu Katibu Mkuu wake, Bw. Zitto Kabwe katika ziara yao ya Iringa waliambulia wanachama watatu pekee jambo ambalo si la kweli.

Kauli ya Bibi Makinda inakuja siku moja tu baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Benard Membe, kusema CCM inajimaliza yenyewe kutokana na kuendekeza makundi ndani yake.

Mama Makinda; huku ni kututukana. nchi haiwezi kuyumba eti tu kwa sababu ccm imekosa viongozi wazuri wa jumuiya zake! wako viongozi wengi toka vyama vingine wanaweza kuongoza vizuri na tutawapa nchi. kama viongozi wa jumuiya za ccm watakuwa wabovu itakayoyumba ni ccm.

mama Makinda na Membe mmeanza kukimbia vivuli vyenu wenyewe! ninyi wenyewe mko ndani ya hayo makundi. vyovyote iwavyo, yawepo makundi au yasiwepo ccm imeshakwisha - hizi ni siku za mwisho kabisa za ccm kumalizika.
 
Jamani hata mtoni Republicans wanagawanyika. Democrats wanagawanyika.

Hata TANU ilishawaigawanyika. Mgawanyiko sio mbaya. Na kwenye mgawanyiko ndipo tunapopata alternative views.

Sahau CCM yasasa ni imara zaidi.
 
Back
Top Bottom