Membe: CCM inajimaliza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Membe: CCM inajimaliza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Dec 8, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,480
  Trophy Points: 280
  Membe: CCM inajimaliza

  • Uchaguzi UVCCM Dar vituko

  na Mwandishi Wetu
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu

  WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinajimaliza chenyewe kutokana na kuendekeza makundi ndani yake.

  Alisema uzoefu alionao, unaonyesha kuwa vyama tawala haviondolewi madarakani na vyama vya upinzani, bali hujiondoa vyenyewe kwa kutokuwa makini na kuendekeza makundi, chuki, fitina, majungu na migogoro isiyo na tija.

  Alisema kwa sasa CCM inatafunwa na makundi na kusababisha mgawanyiko miongoni mwa wanachama, jambo ambalo likiachwa liendelee, linaweza kukimaliza chama hicho tawala.

  Membe alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Mkoa wa Dar es Salaam, uliofanyika jana katika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.

  Katika uchaguzi huo uliotawaliwa na vituko vya kila aina, mtoto wa Mbunge wa Viti Maalumu, Tatu Ntimizi, Said Ntimizi, aliibuka mshindi na kutangazwa kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, hivyo kupata nafasi ya kuingia katika Baraza Kuu la UVCCM.

  Alisema ndani ya CCM kuna makundi yanayokua kila kukicha, hususan ndani ya jumuiya za chama na kushusha heshima ya chama hicho.

  Mbali ya UVCCM, jumuiya nyingine za CCM ni Umoja wa Wanawake (UWT) na Jumuiya ya Wazazi, ambazo mwaka huu, zinafanya uchaguzi wa viongozi wao.

  Membe ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mkutano huo, uliofanyika kwa ajili ya kuwachagua viongozi wa UVCCM, Mkoa wa Dar es Salaam, alionyesha kutokufurahishwa na makundi ndani ya chama hicho, ambayo alisisitiza yamesababisha baadhi ya watu kutokukubaliana na matokeo ya uchaguzi ndani ya chama hicho na kuleta mgawanyiko.

  Aliwataka wana CCM kutambua kuwa maadui wa CCM wamo ndani ya chama na si nje ya chama hicho, kinachoongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.

  “Vyama tawala haviwezi kuondolewa madarakani au kuuawa na vyama vya upinzani ila vinajiua vyenyewe, angalia Kenya, KANU ilijimaliza yenyewe na hata CCM tukiendekeza makundi, tutajimaliza wenyewe,” alisema Waziri Membe.

  “Historia inaonyesha kuwa jumuiya za chama ndizo zina nguvu, lakini kama jumuiya hizo zinaanza kukitafuna chama kwa kukipinga au wanachama kutafunana wenyewe kwa wenyewe ni dhahiri kuwa chama hakiwezi kupambana na wapinzani,” alisema Membe.

  Alisema CCM ina changamoto kubwa mbele yake, ikiwa ni pamoja na wanachama kutokukubaliana na baadhi ya mambo ndani ya chama, ikiwemo majungu, chuki, kugeukana na makundi ambayo yanashusha heshima ya chama.

  “Wapinzani si maadui, maadui wamo ndani ya chama, ugomvi, chuki, majungu, kutukanana, kudhalilishana na kutokukubali kushindwa katika uchaguzi, hao ndio maadui wakubwa wa chama,” alisema Waziri Membe.

  Baada ya ufunguzi huo, uchaguzi huo ulifanyika chini ya ulinzi mkali wa polisi na maofisa usalama.

  Katika uchaguzi huo, wajumbe walipiga kura kumchagua Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa, Makamu wake pamoja na wajumbe watano wa Mkutano Mkuu wa Taifa.

  Wagombea katika nafasi ya Mwenyekiti alikuwa Glorius Luoga, Hamisi Kifimbo na Said Ntimizi.

  Kabla ya kutangazwa kwa matokeo kamili, Ntimizi ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Tatu Ntimizi, alikuwa na kila dalili za ushindi kutokana na kuungwa mkono na wajumbe wengi ambao hawakuweza kuficha hisia zao tangu mwanzo.

  Katika kuthibitisha hilo, baadhi ya wafuasi wake walianza kunywa bia nje ya Ukumbi wa Karimjee, kwa madai kuwa walikuwa wakishangilia ushindi wa Ntimizi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam.

  Moja ya vituko vilivyoonekana katika uchaguzi huo ni kurudiwa kwa kazi ya upigaji kura kwa nafasi ya mwenyekiti bila sababu za msingi kutolewa.

  Hali hiyo iliwafanya wafuasi wa Ntimizi na Luoga waliokuwa wakichuana vikali, kurushiana maneno makali na lugha chafu ndani ya ukumbi huo kiasi cha polisi kuingilia kati.

  Baadhi ya wajumbe waliiambia Tanzania Daima kuwa kura hizo zimelazimika kurudiwa baada ya kura za awali za Ntimizi na Luoga kugongana.

  Baada ya kumaliza kupiga kura za nafasi ya mwenyekiti kwa mara ya pili, wajumbe hao waliendelea kuwachagua wajumbe wa uwakilishi wa jumuiya mbalimbali.

  Hata hivyo, wakati wajumbe ndani ya ukumbi wakiendelea kupiga kura za wajumbe wawakilishi, nje ya ukumbi wajumbe wengine walikuwa wameanza kupiga kelele za kushangilia na kunywa bia, wakicheza kwa furaha kuwa wamemaliza kazi waliyokuja kuifanya ya kumtangaza Ntimizi kuwa mwenyekiti.

  “Mwenyekiti tunaye siku nyingi, tumekuja kumbatiza tu aitwe mwenyekiti, ameshashinda hata kabla kura hazijahesabiwa…tumefanya kweli…” walisikika baadhi ya wajumbe hao huku wakipongezana kwa kunywa bia.

  Hali iliendelea kuwa ya kushangilia nje ya ukumbi, makelele, na wengine wakitukana kuwa Luoga amewaletea polisi kuwasimamia kwenye uchaguzi wakati wao hawana vurugu.

  Wakati wajumbe wa mkutano huo wakipiga kura, Nape Nnauye aliyevuliwa uanachama wa UVCCM, hivyo kukosa sifa ya kugombea na kupiga kura, alisema hatua yake ya kusema ukweli kuhusu mradi wa jengo la UVCCM, ndiyo iliyomgharimu.

  Alisema kutokana na uamuzi huo na kuchelewa kutolewa uamuzi wa rufaa yake, kunamfanya ashindwe kutumia haki yake ya kupiga na kupigiwa kura katika uchaguzi huo.

  Nape alienguliwa na Baraza Kuu la UVCCM kwa madai kuwa alisema uongo kuhusu mradi wa jengo la makao makuu ya umoja huo, kwamba uligubikwa na harufu ya rushwa na kumtaka Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Dk. Emmanuel Nchimbi, Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamani la UVCCM, Edward Lowassa na Kaimu Katibu Mkuu wa umoja huo, Francis Isaac, kuwajibika.
   
 2. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,613
  Likes Received: 2,020
  Trophy Points: 280
  CCM ni chama kikubwa sana na kina matabaka...Unaambiwa CCM ina wenyewe...Sasa Membe analia lia nini?
  Kwani ccm ikifa Taifa nalo limekufa?
  Eti Kenya na sijui KANU...Kwani KANU ilipokufa Kenya ilikufa?
  Aaache utani bana CCM ama bila CCM taifa litasonga mbele tena may be minus ccm tunaweza kuwa na mafanikio zaidi.
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Mzee wa matamshi tata kaubuka baada ya kusema OIC ni halali kwa watanzania? Haya yangu macho kumbe na nyie mnaona kwamba mnakufa kifo cha kulamba sukari ?
   
 4. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Anazungumza mambo ya kweli. lakini je yeye hana kundi? Na amefanya nini kama yeye kuondoa makundi kabla ya kuwataka wengine kuondoa?
   
 5. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #5
  Dec 8, 2008
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  ndio matokeo ya dhambi ya "kula nyama ya mtu".

  makundi ndani ya ccm yalianza zamani tangu enzi za
  lugha ya "huyu ni mwenzetu".

  makundi yamewafikisha wengine kunako power sasa
  ndani ya ccm makundi yanaonekana dili na vigumu
  sana kuyaondoa.

  hata hivyo mh. membe amefanya vizuri kuitambua dhambi hiyo
  hadharani huenda hiyo ikawa moja ya hatua muhimu katika
  kujivua hii dhambi ya makundi.
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Dec 8, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hawezi kujivua ila anazuga tu kwa kuwa he is eying for presidency na hawezi ndani ya CCM bila ya kuwa wapambe ambao ndiyo makundi hayo .
   
 7. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #7
  Dec 8, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,613
  Likes Received: 2,020
  Trophy Points: 280
  Hawawezi eti kujivua dhambi ya makundi...Kwanza tujiulize makundi hayo yamesababishwa na nini halafu ndiyo tujuwe kama wanaweza ku overcome ama la.
  Kiutaratibu ili kuweza kujivua dhambi hizo ni lazima waondowe tofauti zao....Na kuondoa tofauti zao ina maana kukubaliana baina yao kwa jinsi mambo yanavyokwenda..Is that possible?
  Unless makundi hayo ni majungu,chuki na tamaa za madaraka..Lakini kama ni makundi ya dissatisfaction due to the country's direction,Ufisadi,kilio cha wananchi nk...Then ni lazima wameguke.
   
 8. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #8
  Dec 8, 2008
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  CCM sasa hivi has no direction. Hakina sera kiongozi ambayo wote wanatakiwa wawe wanaiamini, isipokuwa wanaunganishwa na madaraka tuu. Mwelekeo wa CCM ni kuongoza serikali tuu, kwenda wap? Mungu anajua. Hiki ndo kitu CCM imekuwa ikifanya kwa miaka yote na ndo walichozoea. Sasa hivi CCM is a way to power. Waliomo wengi hawaamini manifesto au sera za CCM. Wanaamini katika madaraka, that's why they are in CCM in the first place. Ikiwa hali ndo hivyo, tutarajie makundi, magenge, vijiwe, matabaka, n.k.
   
 9. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #9
  Dec 8, 2008
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  maana yangu si membe kujivua dhambi ya makundi bali ccm kama chama.
  kama nilivyosema awali dhambi ya makundi ccm immeanza siku nyingi
  tangu wakati wa chama kimoja (lugha ya huyu mwenzetu) ila imekuwa
  iki-evolve siku hadi siku mpaka kufikia hali tunayoiona leo hii.

  sasa kama ccm itatambua kwamba dhambi ya makundi inaweza kupelekea
  kunyang'anywa dola nadhani hiyo ni hatua muhimu (sijasema kwamba inatosha) kuishinda hiyo dhambi ya makundi.

  lakini suala la ccm kubakia kama chama tawala kwa muda mrefu mwengine
  naamini wanahitaji kufanya kazi ya ziada kuliko hii ya kukubali madhara ya
  makundi. jee uwezo huo wanao? kila mtu ana jibu lake
   
 10. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #10
  Dec 8, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Bernard Membe kafyatua tena!!

  Membe, kaa nje ya siasa za ndani za jirani.

  Nairobi wanaweza ku take umbrage kutoka kwenye jumbe kama hizo, hususan nyakati hivi nyeti za mahusiano yetu ambapo Dar-es-Salaam imekuwa ikiwakera kwa misimamo yetu dhabiti kuhusu mwelekeo wa EA Community. Wewe ndio diplomat in chief wetu, unawezaje kutojua hilo ?

  Hawa mawaziri vipi hawa? Mbona hata makalagabago wa mitaani kama mimi ambao hatujawahi kuwa wasemaji wa nchi hata kwa wiki moja tunajua kwamba that's a no no? Membe vipi huyu ?
   
 11. mbarikiwa

  mbarikiwa JF-Expert Member

  #11
  Dec 8, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 507
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nilisikia kuwa huyu Bernard Membe alisha slim akaitwa Jaffar Membe kama alivyofanya kaka yake John Malecela akaitwa Juma Malecela.

  Sasa kichwa maji anakisema chama chake mwenyewe ambacho ndicho alikuwa anakipigania kwa kuipeleka Tanzania OIC ili kiendelee kubaki madarakani.

  Sasa nimegundua kuwa ni afadhali CUF kuliko CCM
   
 12. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #12
  Dec 8, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,613
  Likes Received: 2,020
  Trophy Points: 280
  Ni janja yake ya ku underestimate kazi ya wapinzani kwa kudai eti ccm itajimaliza yenyewe...Ndio maana mwalimu kuna wakati lazima tutamkumbuka kiaina..At least yeye alitumia neno "mtikisiko" kwa maana kuwa kuna manufaa kwenye kutokuelewana huko...Nani asiyejuwa wanaoelewana ndani ya ccm ni wale powerfull na wenye pesa na connection?
  Ilikuwa kisirisiri wakati wa mwalimu lakini baada ya kuminywa mbavu na mabepari na kusalimu amri...Mwinyi alijitafsiria kivyake na the rest is history kwani Mkapa ndio kaja akamalizia mchezo kwani unafiki uliisha mara baada ya mwalimu kufariki.
  Anaposema kwamba ccm inajimaliza ni uongo kwasababu wale wenye kufanya ufisadi kama wakikaa pamoja na kuendelea kufanya ufisadi bila kupingwa si ndio umoja wenyewe huo ccm? Yani waziri anayejiita mtanzania haoni kuwa tuko kwenye wakati wa kihistoria kwenye Taifa letu na dunia kwa ujumla?
  Hivi hawa viongozi wetu hususan mawaziri huwa wana ratiba gani? Mbona kama si watanzania kabisa na wala hawajui kinachoendelea? Ama ni makusudi tu?
  Waziri mzima unathubutu kusema kuwa kutoridhishwa na hali ya ufisadi ni makundi na kujimaliza?
  Ama kweli siasa sihasa.
   
 13. J

  JokaKuu Platinum Member

  #13
  Dec 8, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,149
  Trophy Points: 280
  wandugu,

  ..yaani Membe anagundua leo kwamba mambo ya fitina,kuchimbana,kuzushiana,...hayafai ktk siasa? huyu si alikuwa kinara kwenye kundi la wana CCM-mtandao waliokuwa wakisifika kwa siasa zao chafu ndani ya CCM?

  ..siasa chafu na za makundi ndiyo zimewaweka Kikwete na Membe madarakani. Sasa hivi Membe anaogopa kwasababu wengine ndani ya CCM wasije wakatumia mbinu hizohizo[za kikwete,membe,mtandao] kuwaondoa madarakani.
   
 14. M

  Masatu JF-Expert Member

  #14
  Dec 8, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Jokakuu,

  Makundi ruksa wakati wa mchakato na kampeni za uchaguzi, baada ya hapo yanatakiwa yafe ili kutekeleza Ilani ya chama.
   
 15. J

  JokaKuu Platinum Member

  #15
  Dec 8, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,149
  Trophy Points: 280
  Masatu,

  ..makundi mazuri ni yale yanayopambanisha ideas za kuwakomboa wananchi. makundi kama mtandao yanayokumbatia siasa za kuchimbana na kuchafuana hayafai ktk siasa wakati wowote ule.

  ..halafu umesahau kauli ya Kikwete kwamba yeye na kundi lake wali-campaign kwa miaka 10? sasa hawa wakakujua kwamba kuna wakati wa campaign/uchaguzi na wakati wa kufanya kazi na kushughulikia matatizo ya wananchi?

  ..nakubaliana na mawazo yako, lakini nadhani Membe hana sifa za kuwahubiria wana CCM wenzake umuhimu kwa kutoendekeza makundi, fitina, uzushi, rushwa,kununua vyombo vya habari, na mambo mengine machafu ktk siasa.
   
 16. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #16
  Dec 8, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Je, ni tetesi yenye ukweli kuwa Membe ni mtoto wa dada yake mwenye kaya ?
  Kama ni kweli itasaidia kutatua mikanganyiko inayonikwaza katika baadhi ya matamshi na msimamo wa huyu mkulu kuhusu mahusiano yetu na dunia tambarara. Kama si kweli naomba msamaha mapema - si unajua tena sikio halina 'anti-spam'.
   
 17. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #17
  Dec 8, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Umedanganywa 100%, hao wawili ni marafiki wa kufa na kupona, urafiki wao una date tangu early 1980s, wakati huo JK akiwa mlala hoi na Membe akiwa ikulu.
   
 18. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #18
  Dec 8, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Jamani hata mtoni Republicans wanagawanyika. Democrats wanagawanyika.

  Hata TANU ilishawaigawanyika. Mgawanyiko sio mbaya. Na kwenye mgawanyiko ndipo tunapopata alternative views.
   
 19. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #19
  Dec 9, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Halafu ukija bongo mpelekee zawadi za nguo na vitabu na sanduku la zawadi badala ya ndugu zako wanaosota, watu wengine bwana hovyooo kweli kweli! Bwa! ha! ha! ha!

  rais asiyejiamini bwana kaaazi kweli kweeeeli!
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Dec 9, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mimi sioni jambo la kushangaza hapa...Jamani hizi chuki hata hapa JF vipi lakini!
  Membe kazungumza issue ndani ya chama chake inakuwaje jamani tunamshambulia yeye wakati maswala ya CCM hayatuhusu hivyo.. acheni wajimalize.
  Isipokuwa tu nitamsahihisha sehemu moja kuhusiana na usemi wake kuwa Chama Tawala hakiondolewi madarakani isipokuwa hujindoa chenyewe!...Mkuu hapa kachemsha na kachemsha kwa sababu hakufuata historia vizuri ya tawala zilizopita na zijazo zinaanguka vipi...

  Mfano wa KANU , pengine hakutazama undani wa Utawala wa KANU kuwa tatizo halikuwa wanachama wake kuweka makundi ya chuki isipokuwa tatizo lilianza kwa rais kiongozi mwenyewe MOI alipong'ang'ania madaraka kama ndugu yake Mugabe wa ZANU PF ndipo vyama hivyo vilipopoteza umoja wao..Kwa hiyo chanzo cha FITNA ama Majungu ndani ya KANU yalianza kutokana na viongozi wake..tamaa ya baadhi ya watu wasiotaka kuondoka ktk Uongozi hata kama Umri wao umepita... Kina NCHIMBI hao na UVCCM ndio chanzo na wapika fitna na majungu kwa sababu hawataki ushindani.. wao ni Miungu watu..
  Sababu ya pili kubwa ni Utajiri unaopatikana bila kutoka jasho!. Ukishika Uongozi ndani ya chama CCM hata kama uwe mwenyekiti wa vijana unapata heshima kuliko kiongozi wa chama pinzani, wewe ni mtu mkubwa tena mheshimiwa, Prince wa ufalme wa nchi ya Wadanganyika kwa nini kusiwepo na fitna!.. Nani anayependa kila siku kuvunja mbavu kupanda daladala!..
  Kwa hiyo Membe anachotakiwa kutazama ktk issue hii ya chama chake sio watu na hizo chuki, kuchimbana na kuzushiana isipokuwa chanzo cha yote haya ni kwamba CCM imejaa Ma -opportunist na nafasi zenyewe ni ndogo..CCM leo hii ni sawa na Rwanda ardhi ndogo, watu wengi.. Na hakuna mtu asiyependa kuonja Utamu wakati chama kimeshika hatamu..

  nani asiyetaka kuonja Utamu wa chama kinaposhika hatamu!
   
Loading...