Membe awavaa wanasiasa wanaojisafisha masikitini, mkanisani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Membe awavaa wanasiasa wanaojisafisha masikitini, mkanisani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sulphadoxine, Jan 13, 2012.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, amewataka viongozi wa dini kuwa macho na wanasiasa wanaotumia nyumba za ibada, kujisafisha kwa jamii ili kulinda maslahi yao binafsi.

  Membe aliyasema hayo juzi mjini Mtwara katika hafla fupi ya kuliombea Taifa, iliyoandaliwa na Mbunge wa Mtwara Mjini, Asnein Murji na kuwakutanisha viongozi mbalimbali wa dini za Kiislamu na Kikristu.

  Alisema amani ya taifa imo shakani na kwamba kama viongozi wa kidini wataruhusu nyumba za ibada kuwa kimbilio la wanasiasa na wao kutumika katika kuwasafisha, hali hiyo inaweza kusababisha mgawanyiko katika jamii.

  Alisisitiza kuwa kama viongozi hao wataruhusu hali hiyo, watakuwa wanaligawa taifa kwa sababu kila muumini atamfuata mwanasiasa wa mrengo wake.

  "Viongozi wa dini msipokuwa makini mtaliingiza taifa katika Machafuko, hakuna chama chochote cha siasa kinachoweza kuvuruga amani yetu, ila ninyi viongozi wa dini mkiamua mnaweza kuvuruga amani yetu,"alisema Membe.

  "Kuweni macho na wanasiasa wanaokimbilia kwenu,msikubali kutumiwa kwa kulinda maslahi ya wanasiasa, fanyeni kazi zenu za kuwajenga waumini wenu kwa mujibu wa mafundisho ya imani zenu, mkiruhusu kutumiwa na wanasiasa amani ya nchi mtaivuruga," alisisitiza.

  Alisema ni jambo la faraja kuona viongozi wa dini wanakutana na kuliombea taifa bila kujali tofauti za itikadi zao na kwamba ushirikiano huo unapaswa kuendelezwa kwa kutoruhusu kugawanywa na wanasiasa.

  Membe ambaye pia ni Mbunge wa Mtama, mkoani Lindi aliwataka wakazi wa mikoa ya kusini kuhakikisha kuwa wanakuwa na haki miliki ya ardhi ili kujihami dhidi ya uporaji unaoweza kujitokeza wakati mikoa hiyo itakapofunguka kiuchumi.

  "Upajikanaji wa gesi mkoani Mtwara ni jambo ambalo litaifanya Mtwara na hata Lindi kuwa sehemu ya mapinduzi ya kiuchumi,shauri wangu wa bure kwenu ni kuhakikisha kuwa mnakuwa na haki miliki ya ardhi, vinginevyo mtaporwa ardhi yenu," alishauri.

  Aliwataka maofisa ardhi katika mikoa hiyo, kuongeza kasi ya kupima viwanja na kuwapatia wananchi haki miliki.

  Kwa upande wake, Murji, alisema lengo la hafla hiyo ni kuliombea taifa ili liondokane na matatizo.

  Alisema hatua hiyo pia inalenga katika kuwawezesha viongozi wa dini kukutana na
  kubadilishana mawazo.

  "Nimeona ni heri kwetu kukutana viongozi wote wa dini na kuliombea Taifa ili liepukane na changamoto mbalimbali zinazolikabili, lakini pia ni vizuri kama viongozi wa dini watazingatia ushauri uliotolewa na Waziri Membe ili kunusuru uvunjifu wa amani' alisema Murji
   
 2. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Membe vs Lowassa again......hawa jamaa watauana naona before 2015! sie yetu macho..
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwanini WAPORWE ARDH,yaan membe anaongea kiurahis namna hii
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  karaha zote zinazoisakama tz wao wanang'ang'ani kwenda Ikulu?
   
 5. Kaliua urambo

  Kaliua urambo JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 606
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  big up bwana membe !
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kwa LiPi?
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  membe akiki yake iko diluted sana....
   
 8. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kwani ulikua unataka kusema nini labda tukusaidie?
   
 9. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Hivi Membe anadhani anaweza kuwa Raisi,hana personality hiyo,kumchagua inaweza kuwa janga kuu la kitaifa,wote na Sumaye na Lowasa hakuna Raisi hapo.Kwanza shangaa anaongelea wanasiasa wanaotumia taasisi za dini wakati naye yuko na hao hao,sasa which is which.
   
 10. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kuna jamaa huko nyuma alikuwa anakosoa mfumo wa chadema wa kutafuta mgombea urais.
  sasa hapa ccm membe na lowasa tutazika mtu kabla ya uchaguzi ujao.
  ccm pameanza kunuka miaka minne kabla.
   
 11. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  And for what I see, kilichomtokea Dr Mwakyembe, basi wa kuzikwa atakuwa Membe.
   
 12. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana kabisa na Membe. Hakika sasa ndio yale yale ya Kimbari na sasa yananukia Kongo DRC.

  Hongera sana Membe kwa kuona mbaaaali.
   
 13. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #13
  Jan 13, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  huu wa Membe ndo unafiki wa hali ya juu,yeye anawalaumu hao wengine kutumia dini kujisafisha wakati na yeye mwenyewe anatumia njia hiyo hiyo kujitangaza.Anatufanya watz hatuna akili sio? Au ameona spidi za wanzake zimekuwa kubwa kushinda yake?
   
 14. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #14
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Nyoka wa mdimu.......By Mudhihir wa Mudhihir(2008)

  [​IMG]
   
 15. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Huyu hawezi kuwa Rais hata afanyeje, angetulia zake, may be Rais wa 2015 angemfikiria hata ka uwaziri, ila anavyoendelea hivi ndo kifo chake kisiasa. Anafuata nyendo za Kigoda
   
 16. Ndetirima

  Ndetirima JF-Expert Member

  #16
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 60
  Membe hana mvuto ndiyo maana hawezi kuombwa kushiriki kwenye hafla za kuchangisha pesa za maendeleo mahali popote. Aache kulalamika aombe nayeye kushirikishwa na atoe michango yake, watu wanataka maendeleo sio maneno matupu. Asijione kwamba yeye ni msafi, atoe kwanza boriti kwenye jicho lake ndiyo aone kibanzi kwenye jicho la mwenzake.
   
 17. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #17
  Jan 13, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Membe ndio aliyeanzisha kujikomba Makanisani. Aache unafki.
   
 18. m

  mudavadi Member

  #18
  Jan 13, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamaa anadhani kwamba kwa kufanya hivyo anajitakasa, kumbe anachokifanya ni money laundering, tena kwa kutumia nyumba za ibada. Bila kutubu Mungu hawezi kumsamehe. Maskini urais unamuendesha mbio, anazunguka kama pia. Tayari amesha-book hafla hadi za mwakani aalikwe.
   
 19. w

  watenda Member

  #19
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii ni pin pointing na unatakiwa ujasiri wa namna hii ili watanzania waelewe kwamba viongozi wetu wa dini wakikubali kuyumbishwa kwa vipande 30 vya fedha basi amani wanaiweka rehani. Hivi hizi hela angewaendeleza wale wamasai waliopoteza mifugo na sasa wanafanya ulinzi na kusuka nywele za wanawake si angeacha legacy?
   
 20. n

  ndutu Member

  #20
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pigo moja, pigo lenye nguvu, pigo takatifu. Angalau kuna mtu amenyanyua mdomo kuwaambia ukweli viongozi wa dini. Lakini kwa ushabiki wetu uchwara kuna watu wataona kwamba mungu wao ametukanwa kumbe waliopewa live ni waponyaji wa roho zetu, na siyo huyu mwizi wa mali zetu anazozitapanya sasa hivi.
   
Loading...