MEMBE Awataka vijana kutetea Taifa kwa nguvu zote. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MEMBE Awataka vijana kutetea Taifa kwa nguvu zote.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jumakidogo, Nov 13, 2011.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kauli ya waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Bernard Membe, kuwataka vijana wapiganie haki kwa nguvu zote na kulitetea taifa kwa gharama yoyote. Inaashiria wapo viongozi ndani ya serikali na chama tawala CCM waliochoshwa na kukerwa na hali ya mambo ilivyo sasa hapa nchini. Membe aliyasema haya jana katika tamasha la Campus Night lililoandaliwa na kanisa la VCC Victory Christian Centre. Kanisa linaloongozwa na Mchungaji Huruma Nkone. Membe alisema Tamasha linapaswa kutumiwa na vijana kuitetea nchi kwa gharama yoyote pasipo hofu ya kuogopa jambo lolote. Alisema pia, vijana wengi hawana ajira. Kauli hiyo aliisindikiza na takwimu ambayo inaonyesha ni 10% ya vijana kati ya vijana laki moja ndio wamepata ajira. Tamasha hilo lilikusanya idadi kubwa ya vijana wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali jijini Dar es salaam. Kwa kauli ya Membe nashawishika moja kwa moja kuwaunga mkono CHADEMA katika harakati zao za kupigania haki ya wanyonge. Membe ameonyesha kupingana na misimamo ya viongozi wenzie kuwa harakati za CDM hazina tija kwa taifa.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hana lolote joka la mdimu hili
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Wakati hakuna kazi kwa Vijana? ni mabomu mtindo mmoja?
   
 4. Cathode Rays

  Cathode Rays JF-Expert Member

  #4
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,736
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Ukitaka kuwajua wanasiasa wenye malengo ya "kisiasa" shika hii kauli halafu subiri nyingine kwenye tukio jingine then linganisha

  Mark these words, then after few weeks ataalikwa pengine ataongea mengine....kama kawaida yao
   
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #5
  Nov 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Bila shaka atakuwa ameanza kuwashwa na mkunaji hakunaga humu aendelee kubaki na magamba atampata mwenyeji wake bila shaka!
   
 6. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #6
  Nov 13, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mwisho wa maneno yake alisahau kuwasihi polisi waache kutumia mabavu.
   
 7. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #7
  Nov 13, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  ukifanya editing ya Jina MEMBE
  Step 1

  M__EMBE

  Step 2
  .
  Kwenye hyo space utajaza mwenyewe.
   
 8. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #8
  Nov 13, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  anauchu na uprezidaa huyu? mpaka anajikuta anaropoka hovyo hovyo. Mpaka 2015 atakuwa chizi kabisa
   

  Attached Files:

Loading...