Membe atua usiku kikachero, ahoji Shibuda alimpinga Kikwete, mbona hakukuwa na nongwa?

Shibuda alifikia wadhifa ailkioufikia yeye. Shibuda anajua mambo ya chumbani mwa Taifa kama yeye anavyojua. Ajiulize kwa sasa anavyo endesha maisha yake yeye ni liability ima thamani kwa taifa?
Shibuda ni msukuma anayeongea ki-zanzibar hahah,sijui alijifunzia wapi kizenj.
 
Kuwa mpole ukitaka kujua hana jipya mpange Membe Vs JPM pawe na usawa, iwe nje au ndani ya CCM, au kwa kura za Watanzania, Membe anashinda kirahisi,..... Kama hana mvuto muache afu wawapambanishe na MAGU jibu utalipata na nadhani unalijua
Hapa ndipo Watanzania wengi tunapokosea, "Kulinganiasha tunayeona amekosea VS Tunayemtaka"

Tunayemtaka ni lazima asimame mwenyewe kwa vigezo vinavyoonesha kuwa anatufaa. Mambo ya kulinganisha walio hai na wafu ndio yametufikisha hapa tulipo.
 
Machadema yanacheza ngoma wanazopiga ccm!

Haya majamaa hata yawekewe kujifunza kwa picha hayajikuelewa kamwe!

Yani Tanzania Daima badala ya kuandika habari za mwenyekiti kuwa jela, nyie mnapoteza muda na Membe mkiamini kwamba kweli kuna mgogoro wa kuiyumbisha ccm hapo?
 
Hatimaye kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Bernard Membe, ambaye kwa takribani wiki mbili sasa limetikisa anga la ndani na nje ya nchi ametua nchini kikachero, Tanzania Daima limebaini.

Membe ambaye ameingia kwenye malumbano na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally, kurejea kwake kumekuwa kukivuta hisia za wengi wanaosubiri kujua hatma ya mwana diplomasia huyo kutokana na tuhuma dhidi yake kwamba anataka kumvurugia rais John Magufuli kuwania urais mwaka 2020.

Membe ambaye amepata kuwa Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa chini ya rais mstaafu, Jakaya Kikwete, amewasili jana saa mbili usiku kwa ndege ya Sheila la ndege la Kenya (KQ), akitokea nje kwa shughuli binafsi.

Mmoja kati ya watu wa karibu waliofika kumpokea Membe, aliliambia Tanzania Daima kuwa alifanya hivyo ili kukwepa baadhi ya makada wa CCM waliopanga kumpokea.

"Unajua Membe ana kesi kwa katibu mkuu, lakini pia CCM ilishaonya watakaokwenda kumpokea wasivae sare za chama, kwa hiyo kama wangejua anarudi leo wangekuja wengi na hiyo ingekuwa mbaya kwake", alisema kada huyo.

Chanzo, Gazeti la Tanzania Daima.
Upinzani na makuhadi wenu mnajisumbua sana kujaribu kuidhoofisha CCM. Kama mlishindwa wakati wa Lowassa, ambaye mpaka leo mnamwita Rais wa mioyo ya WaTz, leo hii mnafanya vituko na vichekesho kwenye vyombo vyenu vya habari na mitandao ya kijamii.

Ikumbukwe kuwa CCM siyo mtu ila ni chama cha Wakulima na Wafanyakazi tofauti na vyama vingine vilivyoanzishwa na watu binafsi kwa maslahi binafsi.

Mchango wa CCM kuleta uhuru na ukombozi wa Afrika ni nguzo moja kuu inayowaunganisha wanachama wake na wanachama wa vyama vingine vya ukombozi.

Kama upinzani una nia ya dhati kutawala nchi hii, itumie mbinu sahihi za kukonga mioyo ya wapiga kura kuliko kujaribu kuweka chuki ndani ya chama tawala. Moja ya mikakati sahihi ni kwa vyama hivyo kujitambulisha kama vyama vya wanachama na siyo vya kiongozi mmoja mmoja km Mbowe - CHADEMA au Maalim - CUF.
 
Shibuda ni msukuma anayeongea ki-zanzibar hahah,sijui alijifunzia wapi kizenj.

Shibuda naye anazurura huko nje akitafuta watakao muunga mkono kugombea urais 2020? Basi wamuangalie asije akauza siri za kujuakizenji ili kutunisha mfuko wa kununulia kura na wapiga kura. Na ndipo hatari kwa usalama wa Taifa ilipo. Kuuzwa siri za nchi ilikutunisha mfuko.
 
Hata wewe kuna watu hawakupendi mtaani kwenu au kazini kwako.Hatuongelei kupendwa hapa.Mimi nakwambia hivi acha NDOTO Membe hawezi kuwa raisi wa nchi hii.Ndio point yangu kubwa.Kumuondoa raisi aliyepo madarakani kabla ya mihura miwili kwa nchi yetu Tanzania haziwezekani.Nasisitiza haiwezekani,punguzeni NDOTO za mchana.Halafu watu sio wanaoamua, mfumo ndo unaamua ndo maana nikakwambia labda ahamie CHADEMA akagombee huko ila kwa CCM haiwezekani (NEVER).
Kuwa mpole mbona mnamuogopa sana Membe, uyu Jiwe ata akisimama na James delicious, lazima apigweee
 
Kweli mleta mada ni punguani wahed, yeye anakurupuka eti karudi kikachero wakati hajui alikuwa wapi na aliondoka lini. Na siyo mara ya kwanza Membe kusafiri nje ya nchi na kurudi bila mleta mada kujua.
Kaja na ungo?

Punguani wahed.
You're barking at the wrong tree.

IMG_20181207_091223.jpg
 
Yaani mimi sitarajii upinzani kuongoza nchi, ila wacha tusubiri
 
Kuwa mpole ukitaka kujua hana jipya mpange Membe Vs JPM pawe na usawa, iwe nje au ndani ya CCM, au kwa kura za Watanzania, Membe anashinda kirahisi,..... Kama hana mvuto muache afu wawapambanishe na MAGU jibu utalipata na nadhani unalijua
Mkuu tume yenyewe ya uchaguzi sio huru, kila idara ni ccm, sioni namna ya kumtoa ccm madarakani.
 
Hatimaye kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Bernard Membe, ambaye kwa takribani wiki mbili sasa limetikisa anga la ndani na nje ya nchi ametua nchini kikachero, Tanzania Daima limebaini.

Membe ambaye ameingia kwenye malumbano na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally, kurejea kwake kumekuwa kukivuta hisia za wengi wanaosubiri kujua hatma ya mwana diplomasia huyo kutokana na tuhuma dhidi yake kwamba anataka kumvurugia rais John Magufuli kuwania urais mwaka 2020.

Membe ambaye amepata kuwa Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa chini ya rais mstaafu, Jakaya Kikwete, amewasili jana saa mbili usiku kwa ndege ya Sheila la ndege la Kenya (KQ), akitokea nje kwa shughuli binafsi.

Mmoja kati ya watu wa karibu waliofika kumpokea Membe, aliliambia Tanzania Daima kuwa alifanya hivyo ili kukwepa baadhi ya makada wa CCM waliopanga kumpokea.

"Unajua Membe ana kesi kwa katibu mkuu, lakini pia CCM ilishaonya watakaokwenda kumpokea wasivae sare za chama, kwa hiyo kama wangejua anarudi leo wangekuja wengi na hiyo ingekuwa mbaya kwake", alisema kada huyo.

Kuhusu kugombea aliongeza kuwa, "Hakuna sehemu katika Katiba ya chama inayosema kuwa ni lazima rais aliyepo aendelee kwa miaka mingine mitano bila kupingwa, bali ni utaratibu tu waliouona waasisi wa chama hicho, kuwa pengine ni wa kiungwana kiongozi apewe kipindi kingine amalizie aliyoyaanza".

Alisema tangu utaratibu huo uanze, alipata kujitokeza kada mmoja tu wa CCM, Magare Shibuda ambaye aliomba kuwania urais mwaka 2010 wakati ambao rais Kikwete alikuwa akiwania muhula wa pili.

"Kwa maana hiyo, si jinai kwa mwanaccm kujitokeza kugombea urais katika kipindi ambacho rais aliyeko madarakani naye anataka kuwania apate miaka mingine mitano ya kuongeza". Alisema kada huyo.

Chanzo, Gazeti la Tanzania Daima.
Kwahiyo kuwasili usiku ndio kikachero? Too much hype and sensationalism, no iota of substance.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom