Membe atua usiku kikachero, ahoji Shibuda alimpinga Kikwete, mbona hakukuwa na nongwa?

Jamaa karudi.
Huko green house kwa sasa najua hapakaliki.
.
IMG-20170923-WA0114.jpeg
 
Whatever, ila Membe hawezi kuwa raisi,iwe kwa ubabe iwe vyovyote hata ikibidi kutumia njia nisizoweza kuzielezea hapa.Ndo maana nakuhakikishia 100% mnapoteza muda wenu bure kujadili Jambo lisilowezeka.Learn to accept the truth.Jifunze kuendana na mazingira yaliyopo, kumshabikia Membe hakutamfanya awe raisi wa nchi hii.Sio 2020 tu bali hata 2025. Watanzania hampendi kuambiwa ukweli ila ukweli ndo huo.
Tuliza kende wewe ni nani adi uwaamlie watu, 2015 lowasa alisumbua sana,sahv ndo kabisaaa Jiwe ni Shetani Mkubwa, me nilimpa kura ila 2020 simpi nashukuru mnajua kuwa Jiwe hapendwi
 
Tuliza kende wewe ni nani adi uwaamlie watu, 2015 lowasa alisumbua sana,sahv ndo kabisaaa Jiwe ni Shetani Mkubwa, me nilimpa kura ila 2020 simpi nashukuru mnajua kuwa Jiwe hapendwi
Hata wewe kuna watu hawakupendi mtaani kwenu au kazini kwako.Hatuongelei kupendwa hapa.Mimi nakwambia hivi acha NDOTO Membe hawezi kuwa raisi wa nchi hii.Ndio point yangu kubwa.Kumuondoa raisi aliyepo madarakani kabla ya mihura miwili kwa nchi yetu Tanzania haziwezekani.Nasisitiza haiwezekani,punguzeni NDOTO za mchana.Halafu watu sio wanaoamua, mfumo ndo unaamua ndo maana nikakwambia labda ahamie CHADEMA akagombee huko ila kwa CCM haiwezekani (NEVER).
 
Shibuda alifikia wadhifa alioufikia yeye. Shibuda anajua mambo ya chumbani mwa Taifa kama yeye anavyojua. Ajiulize kwa sasa anavyo endesha maisha yake yeye ni liability ima thamani kwa taifa?
 
Hatimaye kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Bernard Membe, ambaye kwa takribani wiki mbili sasa limetikisa anga la ndani na nje ya nchi ametua nchini kikachero, Tanzania Daima limebaini.

Membe ambaye ameingia kwenye malumbano na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally, kurejea kwake kumekuwa kukivuta hisia za wengi wanaosubiri kujua hatma ya mwana diplomasia huyo kutokana na tuhuma dhidi yake kwamba anataka kumvurugia rais John Magufuli kuwania urais mwaka 2020.

Membe ambaye amepata kuwa Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa chini ya rais mstaafu, Jakaya Kikwete, amewasili jana saa mbili usiku kwa ndege ya Sheila la ndege la Kenya (KQ), akitokea nje kwa shughuli binafsi.

Mmoja kati ya watu wa karibu waliofika kumpokea Membe, aliliambia Tanzania Daima kuwa alifanya hivyo ili kukwepa baadhi ya makada wa CCM waliopanga kumpokea.

"Unajua Membe ana kesi kwa katibu mkuu, lakini pia CCM ilishaonya watakaokwenda kumpokea wasivae sare za chama, kwa hiyo kama wangejua anarudi leo wangekuja wengi na hiyo ingekuwa mbaya kwake", alisema kada huyo.

Kuhusu kugombea aliongeza kuwa, "Hakuna sehemu katika Katiba ya chama inayosema kuwa ni lazima rais aliyepo aendelee kwa miaka mingine mitano bila kupingwa, bali ni utaratibu tu waliouona waasisi wa chama hicho, kuwa pengine ni wa kiungwana kiongozi apewe kipindi kingine amalizie aliyoyaanza".

Alisema tangu utaratibu huo uanze, alipata kujitokeza kada mmoja tu wa CCM, Magare Shibuda ambaye aliomba kuwania urais mwaka 2010 wakati ambao rais Kikwete alikuwa akiwania muhula wa pili.

"Kwa maana hiyo, so jinai kwa mwanaccm kujitokeza kugombea urais katika kipindi ambacho rais aliyeko madarakani naye anataka kuwania apate miaka mingine mitano ya kuongeza". Alisema kada huyo.

Chanzo, Gazeti la Tanzania Daima.
2020 CCM pasu kwa pasu tupa huko!
 
Back
Top Bottom