Hatimaye kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Bernard Membe, ambaye kwa takribani wiki mbili sasa limetikisa anga la ndani na nje ya nchi ametua nchini kikachero, Tanzania Daima limebaini.
Membe ambaye ameingia kwenye malumbano na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally, kurejea kwake kumekuwa kukivuta hisia za wengi wanaosubiri kujua hatma ya mwana diplomasia huyo kutokana na tuhuma dhidi yake kwamba anataka kumvurugia rais John Magufuli kuwania urais mwaka 2020.
Membe ambaye amepata kuwa Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa chini ya rais mstaafu, Jakaya Kikwete, amewasili jana saa mbili usiku kwa ndege ya Sheila la ndege la Kenya (KQ), akitokea nje kwa shughuli binafsi.
Mmoja kati ya watu wa karibu waliofika kumpokea Membe, aliliambia Tanzania Daima kuwa alifanya hivyo ili kukwepa baadhi ya makada wa CCM waliopanga kumpokea.
"Unajua Membe ana kesi kwa katibu mkuu, lakini pia CCM ilishaonya watakaokwenda kumpokea wasivae sare za chama, kwa hiyo kama wangejua anarudi leo wangekuja wengi na hiyo ingekuwa mbaya kwake", alisema kada huyo.
Chanzo, Gazeti la Tanzania Daima.