Membe atua usiku kikachero, ahoji Shibuda alimpinga Kikwete, mbona hakukuwa na nongwa?

MI
Hivi unatuaje Airport kikachero, nikajua labda kaingia na Parachute, maana kama katumia Airport kuingia hapa nchini hilo ni jambo la kawaida na hakuna ujasusi hapo. Acheni kukuza mambo.
nikajua katua kwa kutumia mwamvuli, kumbe kashuka kawaida tu
 
Tunaenda na Magu Mpaka 2025, Then tunamuongezea miaka 5, tukiona bado hajachoka tunampa kumi Mingine, Tukutane 2040
 
Kuwa mpole ukitaka kujua hana jipya mpange Membe Vs JPM pawe na usawa, iwe nje au ndani ya CCM, au kwa kura za Watanzania, Membe anashinda kirahisi,..... Kama hana mvuto muache afu wawapambanishe na MAGU jibu utalipata na nadhani unalijua

Ndio maana tumeanza kumshughulikia mapema. Kumbuka walimtuhumu Membe kuanza kampeni kabla ya muda hawatakiwi kuthibitisha tuhuma.
 
Nchi haina mashujaa ni vigumu kusonga mbele watazania wote kazi yetu ni kulaumu na kukosoa na mbaya tumekua waoga zaidi na wabinafsi hatukuumbwa ili kuthubutu
 
Whatever, ila Membe hawezi kuwa raisi,iwe kwa ubabe iwe vyovyote hata ikibidi kutumia njia nisizoweza kuzielezea hapa.Ndo maana nakuhakikishia 100% mnapoteza muda wenu bure kujadili Jambo lisilowezeka.Learn to accept the truth.Jifunze kuendana na mazingira yaliyopo, kumshabikia Membe hakutamfanya awe raisi wa nchi hii.Sio 2020 tu bali hata 2025. Watanzania hampendi kuambiwa ukweli ila ukweli ndo huo.

Fundi wa goli la mkono ameshaumizwa.
Kumbuka aliyoyasema alipotishiwa bastola
 
Ndugu yangu! Huyo Membe hana jipya. Kama angekuwa na ushawishi aliyokuwa nao Lowassa mwaka 2015, tungesema sawa. Lakini kwa sasa usitegemee lolote jipya kutoka kwa Membe. Hii ni kutafuta tu front page na kiki kwenye vyombo vya habari. Kamati ya maadili ya chama iliyomkata bwana Lowasa 2015, naamini bado ipo palepale hata huyo akiruhusiwa kuchukua fomu ya kuteuliwa ndani ya chama kugombea urais itafanya kazi yake tu. Hivyo, suala la Membe mimi naona kuwa watu wanapoteza muda wao tu kulijadili.
Ishu siyo ushawishi, ishu ni MKAKATI, ushawishi haukumuwezesha EL kuingia ikulu, na aliyeingia ikulu hakuwa na ushawishi bali mkakati ... the movie is very interesting ...
 
Kinyanganyiro cha kuanza kuomba ridhaa ya kuwania nafasi hiyo kwa mjibu wa kanuni za chama bado. Sasa yeye akianza harakati hizi mapema sana, yatamkuta yale yaliyomkuta ndugu LOWASA. Someni kanuni za chama nadhani ndiyo mtayajua haya. Lakini mkiwa mashabiki tu, hamtayajua.
Unajua stori zote hakuna mahali ambapo BM ameonesha kuwa ameaanza hicho kinacho semwa kuwa ameanza ... bora hata EL yeye zilikuwa wazi zilionekana lakini jamaa yupo kimya ni maneno tu anawekewa mdomoni ... ataitwa atakanusha then what ... 2020 imekuwa karibu kuliko ilivyofikiriwa....:D:D:D
 
Bwana Membe ana aiba ya uongozi nadhani ndicho kinachimponza maana wengine waliotajwa hatujasikia wakisumbuliwa sumbuliwa
 
Hatimaye kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Bernard Membe, ambaye kwa takribani wiki mbili sasa limetikisa anga la ndani na nje ya nchi ametua nchini kikachero, Tanzania Daima limebaini.

Membe ambaye ameingia kwenye malumbano na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally, kurejea kwake kumekuwa kukivuta hisia za wengi wanaosubiri kujua hatma ya mwana diplomasia huyo kutokana na tuhuma dhidi yake kwamba anataka kumvurugia rais John Magufuli kuwania urais mwaka 2020.

Membe ambaye amepata kuwa Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa chini ya rais mstaafu, Jakaya Kikwete, amewasili jana saa mbili usiku kwa ndege ya Sheila la ndege la Kenya (KQ), akitokea nje kwa shughuli binafsi.

Mmoja kati ya watu wa karibu waliofika kumpokea Membe, aliliambia Tanzania Daima kuwa alifanya hivyo ili kukwepa baadhi ya makada wa CCM waliopanga kumpokea.

"Unajua Membe ana kesi kwa katibu mkuu, lakini pia CCM ilishaonya watakaokwenda kumpokea wasivae sare za chama, kwa hiyo kama wangejua anarudi leo wangekuja wengi na hiyo ingekuwa mbaya kwake", alisema kada huyo.

Chanzo, Gazeti la Tanzania Daima.

View attachment 958723
Hivi ni kwanini CCM wanahangaika sana na membe badala ya kutumia nguvu hizo kuwaletea wananchi maendeleo? Naona Membe sasa amegeuzwa kuwa 'jimbo la uchaguzi'. MaCCM ni majitu ya ovyo sana.
 
Back
Top Bottom