Membe asijekuwa kama waziri wa mambo ya nje wa Misri! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Membe asijekuwa kama waziri wa mambo ya nje wa Misri!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kayumba, Mar 7, 2011.

 1. k

  kayumba JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nimemsikiliza Waziri Membe akihojiwa ITV na katika mahojiano hayo nimesikia maneno niliyoyasikia kwa waziri wa Mambo ya Nje wa Misri baada ya mapinduzi ya Tunisia. Akijibu hoja ya Katibu Mkuu wa umoja wa nchi za Kiarabu Amr Mussa kuwataadhalisha kuwa kilichotoka Tunisia kinaweza kutokea katika nchi zao.

  Wazari huyo alisema hivi "Yanayotokea Tunisia hayawezi kutokea Misri kwa sababu serikali yao ilikuwa tofauti na ya Tunisia"! Na Membe amesema yaliyotokea katika nchi za kiarabu hayawezi kutokea katika nchi yetu kwasababu hata nchi nyingine (UN, AU na jumuia nyingine) hazitaruhusu ukiukwaji wa demokrasia!!!!.

  Uenda hatukujifunza kutoka kwa wenzetu. Iili tuwe salama ni kutatua matatizo yaliyoleteleza maandamano katika nchi nyingine na si kukaa tukidhania sie hatuwezi kufikwa na yaliyotokea kwingine.
   
 2. M

  Mindi JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2011
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 1,393
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Alifanya kazi kubwa sana kuitetea serikali na ku-play down changamoto ya CHADEMA. hata hivyo kinachotakiwa ni kutafutia ufumbuzi wa uhakika matatizo yanayoikumba nchi yetu. hiyo nchi anayosema inaheshimika sana huko nje, imepata hard beating kwa mambo mengi ya kizembe. mpaka sasa "wadau wa maendeleo" wanasita kuichangia serikali kutokana na matatizo makubwa ya utendaji na upungufu mkubwa katika udhibiti na usimamizi wa matumizi ya serikali. kuna wikileaks walivyoanika kuhusu serikali kutokuwa na nia ya kweli kukabiliana na rushwa na ufisadi. ni nchi tofauti kabisa na ile ya zamani ambapo rushwa na ufisadi vilikuwa katika viwango vya chini sana.

  Hao wananchi waliolemewa na maisha bado wanatafuta namna ya kuonesha hasira yao. angalau CHADEMA wanatoa mwanya ku-organise protest hizi. bila hivyo bomu lingelipuka kwa vurugu zaidi. serikali isijisahau, there is no time to lose. vinginevyo hayo anayodai hayawezekani, yatawezekana na kauli ya wengi ni kauli ya Mungu. kitakachofanyika ni jumuiya ya kimataifa kuomba tu uchaguzi ufanyike basi! asidhani watakuja kumsaidia kuwarudisha madarakani wakiangushwa na popular upraising!
   
 3. k

  kayumba JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kifikiri jumuia ya kimataifa itawaokoa wakati ufisadi wanaufumbia macho hizo ni ndoto za mchana kweupe!
   
Loading...