Membe adaiwa kusaidia kampuni ya wanandugu (MEIS) kuchota bilioni 54

Membe hapo anachokitaka ni gawio.....hana kingine ndio maana analilia hiyo deal......na huyo Mo hadi amemlipua unaweza kukuta wana mgongano wa kimasilah

Mo naye ni mnufaika wa hicho kiwanda cha saruji kilichowekewa kauzibe na Membe, sasa hapa mshindi itategemea ukaribu wake na jk maana siku hizi ili ufanikiwe mambo yako ni muhimu kujinasibisha na jk ama ikulu.
 
Kama hao jamaa wanawekeza kwenye kiwanda cha saruji na haki imefuatwa wapewe wao. Hawa akina Mo pamoja na kuzaliwa na kuishi Tanzania kote huko lakini mpaka leo wanandoto za Canada na Uingereza, it is pitty lakini ni tatizo kubwa la Wahindi!
Tatizo hapo ni Urais 2015, Rostam anajaribu kumchafua Membe. Membe kwa kujisafisha aseme kila kitu wazi wazi! Lakini bila shaka hizi ni siasa zile za Urais kwa CCM 2015.
Kama deni liliuziwa au walipewa MEIS basi lifanye kazi iliyokusudiwa kwa wananchi wa Tanzania. Hawa MEIS naona wameamua kuingia kwenye saruji hata kiwanda cha Mukuranga ni cha kwao!!!
 
Kama pia swala lina Rushwa ndani yake liangaliwa kwa uangalifu na hatua kuchukuliwa!!!!!!!!!!
 
Kama pia swala lina Rushwa ndani yake liangaliwa kwa uangalifu na hatua kuchukuliwa!!!!!!!!!!
Nani wa kuchukua hiyo hatua? HOSEA hua hahusikagi na marushwa makubwa makubwa kama haya, hua anayapotezeaga tu kama alivyofanya kwenye Richmond, Deep Green, Kagoda, Meremeta, Tangold n.k.
 
hapa mpango wa kumchafua Membe na kumsifia Asha Rose Migiro umeanza
I support you! Hapa pana ujinga tu wa kumchafua waziri, halafu hivi watu wana fikra za aina gani?? Huyu mama Migiro hana uzoefu wowote wa wizara nyeti humu nchini anaweza kuwa Rais? Nadhani akisimama Slaa na Migiro, nitampigia Slaa.
 
Umenena......hosea hahusiki kabisaaaa na wala sheria haimruhusu kuchunguza marushwa haya MAKUBWA
Nani wa kuchukua hiyo hatua? HOSEA hua hahusikagi na marushwa makubwa makubwa kama haya, hua anayapotezeaga tu kama alivyofanya kwenye Richmond, Deep Green, Kagoda, Meremeta, Tangold n.k.
 
Suala hapa si Membe kuchafuliwa au Migiro kufagiliwa,lililopo mbele yetu ni moja tu nalo ni kuhakikisha 2015
Magamba wote wanaondoka,hata aje nani kutoka chama cha magamba hawezi kuleta mabadiliko.
 
I support you! Hapa pana ujinga tu wa kumchafua waziri, halafu hivi watu wana fikra za aina gani?? Huyu mama Migiro hana uzoefu wowote wa wizara nyeti humu nchini anaweza kuwa Rais? Nadhani akisimama Slaa na Migiro, nitampigia Slaa.
leo nimepita mtaani Dar es Salaam nimeona exchange rate ya US $ inakaribia sh. 1,590/- (1600) ambao itakuwa rekodi katika historia! Kama hamuoni faida za 'mitandao' yenu hiyo inavyofilisi na kuporomusha uchumi wa nchi yetu, na hapo hamjafikiria kuporomoka kwa maadili, endeleeni tu!
 
Mtanzania at it again! Lakini bahati nzuri sana na safari hii, gazeti hili "lililojijengea umaarufu na heshima ya kuwabeba mafisadi na kuwachafua maaduai zao" wameibuka na goof ya mwaka. Issue ya conflict of interest hapa inaingiaje? Watch this space! tutawasambaratisha kwa hoja na umma wa watanzania utapata ukweli very soon, siyo hizi malicious porojo!
 
sijui kama ni mimi tu ndio siewlewi, hivi hizo hela zinazogombewa chanzo chake ni nini?
 
hapa mpango wa kumchafua Membe na kumsifia Asha Rose Migiro umeanza
Hapa mchezo umeanza ule wa 1995 (mtandao) ninaamini hawa jamaa watamchafua kila mmoja toka chama cha magamba ili mradi siye yule wanaye muunga mkono. Wakifanya mchezo njia nyeupeee kwa wanamageuzi
 
Suala siyo kwamba membe anachafuliwa au hachafuliwi. Hilo sisi hatuwezi kujua ukweli wake. Suala ni yeye kujisafisha na tuhuma zinazoelekezwa kwake. Uzuri ni kwamba hata huyo membe hana ubavu wa kupambana na Chadema.
 
Mtanzania at it again! Lakini bahati nzuri sana na safari hii, gazeti hili "lililojijengea umaarufu na heshima ya kuwabeba mafisadi na kuwachafua maaduai zao" wameibuka na goof ya mwaka. Issue ya conflict of interest hapa inaingiaje? Watch this space! tutawasambaratisha kwa hoja na umma wa watanzania utapata ukweli very soon, siyo hizi malicious porojo!

Hapa hakuna suala la siasa wala 2015, kinachogamba hapa ni maslahi ya kiuchumi na hoja zinazojengwa hazielezei ukweli wote kuhusu sakata hili. Ukweli ni kwamba,miaka ya nyuma Serikali ya Libya iliikopesha Serikali ya Tanzania mafuta . Deni hilo ni sehemu ya madeni ya nje ambayo serikali imekuwa ikidaiwa.

Kwakuwa deni hili ni moja ya yale madeni yaliyokaa muda mrefu bila mwenye fedha zake kudai, likaingizwa kwenye mpango wa DEBT SWAP- ambao Serikali au taasisi zisizo za kiserikali zimefanya mazungumzo na MDAI kuomba asamee deni kwa ahadi kwamba fedha hizo zitakazosamehewa zitatumika katika miradi ya maendeleo yenye kusaidia kuwaondoa wananchi kwenye umasikini.


Kwa kesi ya deni la Libya, METL ilikuwa ni moja ya makampuni kadhaa yaliyojitokeza kufanya mazungumzo na Serikali ya Libya kuomba deni hilo lisamehewe, ili sehemu ya fedha za msamaha wazitumie kuwekeza katika mradi wa maendeleo nchini.


Harakati za METL hazikuzaa matunda,kwani baadhi ya watendaji katika serikali ya Libya walifikiria badala fedha hizo kupewa kampuni ya Tanzania, bora ziwekezwe kwenye hoteli ya Bahari Beach ambayo inamilikiwa na Serikali ya Libya kupitia kampuni ya Libya Investment Authority (Sovereign Fund)
http://www.libyaninvestmentauthority.com/ .

Uamuzi huo ulichukua muda mrefu kuwa executed....kwasababu wanazojua wao walibya (pengine kwakuwa hawakuwa na interest ya uwekezaji kwenye miradi iliyopo sub-saharan Afria-kwani Sovereign Fund hii imejikita zaidi kwenye uwekezaji katika mafuta, na bishara nyingine za mabenki etc barani Ulaya.


METL (mohamed enterprises) baada ya kuona bado fedha hizo zipo nchini na hazijachukuliwa na Libyan Investment Authority kuwekezwa katika hotel ya bahari beach....wakaamua kufanya ‘uchakachuaji’ kwa kushirikiana na AFISA WA UBALOZI WA LIBYA na baadhi ya watendaji wa Benki kuu, ili walipwe fedha hizo (kama deals za EPA zilivyokuwa zikifanyika). Mchakato wao wa kuchakachua ulifika mbali....lakini kwa bahati mbaya kwao, kuna mtu aliyeistua Serikali ya Libya kupitia BALOZI wao...wakazima jalibio hilo. Vile vile Afisa huyo wa Libya alisimamishwa kazi na kurejeshwa kwao Libya. Juhudi za Mohamed Enterprises kumshtaki afisa huyo hazikuzaa matunda kwakuwa alikuwa na kinga, na alishakuwa recalled kwao.

In the meantime, Balozi mpya wa Libya ambaye yupo well-connected na Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Libya na CEO wa Mfuko wa Libyan Investment Authority, aliwashawishi Serikali yake.....waruhusu fedha zao ziwekezwe nchini kwa kuipatia local company. Wazo la Balozi huyo lilikubalika kwao, na yeye akapewa jukumu la kutafuta local company ambapo yeye aliipendekeza kampuni ya MEISE (ya hao ndugu watatu wanaoongelewa). Balozi aliichagua kampuni hiyo kwasababu yeye alikuwa na mahusiano ya karibu na Mmoja wa wenye kampuni hiyo Bw. Islam ambaye ni Balozi wa Heshima wa Nchi ya Comoro hapa Tanzania. Mahusiano yao ya kibalozi ambayo baadaye yalikuwa cemented zaidi na ushirikiano wa Comoro na Libya katika harakati za Libya kuisaidia Serikali ya Comoro kukikomboa kisiwa cha Anjuan, yalipelekea AUTHORITIES kule LIBYA kuafiki moja kwa moja pendekezo la Balozi wao kwamba fedha zile ipewe kampuni ya BW Islam kwa ajili ya uwekezaji katika UJENZI wa kiwanda cha kutengeneza CEMENT kule LINDI. Kampuni ya MEISE iliamua kuwekeza kwenye kiwanda hicho Mkoani Lindi katika jimbo la Mchinga, kwakuwa eneo lile kuwa limestone kwa wingi sana, vile vile walikuwa na uhakika wa kupata umeme wa uhakika kutoka SONGAS. Lengo lao lilikuwa ni kuuza cement hiyo nchini na nyingine ku export nchi za jirani hasa Zambia na Msumbiji ambako kuna mahitaji makubwa ya CEMENT.
Benard Membe, kama Mbunge wa kutoka Mkoa wa Lindi, amekuwa very supportive kwa mradi huo,kwani ungetoa ajira kwa wananchi wa mkoa wa Lindi na kuuinua mkoa wao kiuchumi. Si ajabu kama katika mikutano yake na Walibya ali express support ya mradi huo na kuwapa confidence Serikali ya Libya kwamba mradi huo unakwenda mahala salama na faida zake zi wazi.

Mpaka leo Mohamed Enterprises, hawajasema fedha hizo walitaka kuzifanyia nini? Na faida za mradi wao zingekuwa ni zipi? Lakini Pamoja na hayo, MWENYE FEDHA ZAKE, akiamua kumpatia mtu mwingine.....wao kwanini wawe na NONGWA....kwani waliwekeza mpaka waone ni haki yao? Katika historia ya DEPT SWAP nchini Mohamed Enterpirses wamekwishawahi kupewa pesa nyingi sana toka enzi za awamu ya pili....watueleze wamewekeza wapi? Matunda yake ni nini?
Kwa maoni yangu.....haya makampuni yanayopigana leo nani apewe fedha hizo....yanachelewesha maendeleo kwa wananchi...iwe wa Lindi au pengine ambao Mohamed Enterpirses alikuwa anafikiria kuwekeza.......Tuache kupigania maslahi binafsi...tufikirie wananchi wengi masikini wanaosubiria ajira....
NA kwa gazeti la Mtanzania hili linajulikana kwa siasa za majitaka dhidi ya watu wanaowadhania wanaingilia kati ndogo za mabosi wao za 2015....
 
Back
Top Bottom