Membe asaidia kampuni ya wanandugu kuchota bilioni 54 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Membe asaidia kampuni ya wanandugu kuchota bilioni 54

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bajabiri, Jun 20, 2011.

 1. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hatimaye MEMBE amekiri kuwa ana uhusiano wa karibu na ile kampuni ya MEISS ambayo anataka iende jimbon kwake ikajenge kiwanda cha saruji......membe amesema kua kampuni hiyo ana uhusiano nayo kwa kua ni rafiki zake.....
  My take:sakata hili liliibuka last weekend ambapo gazet la mtanzania liliripoti na inaendelea hukohuko kwenye gazeti la mwanamagamba(mtanzania)
   
 2. e

  emrema JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani hii issue sio ndogo kiongozi kuwa na interest kwenye kampuni na kuwatukana wawekezaji wenginew na wanasiasa?what is behind this?
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ukiona hivyo ujue wamemshika katikati ya miguuu....ndo maana kaamua kutukana
   
 4. v

  vivimama Member

  #4
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hawa ndo viongozi tunaowachagua hawajua hata mipaka yao.
  AIBU SANA.

  mapenzi yangu
   
 5. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  KAMPUNI ya Mohamed Enterprises (MeTL), kupitia Mahakama Kuu, imekwamisha malipo ya dola milioni 34 za Marekani (Sh bilioni 54.4)bil- ambazo zilikuwa zichukuliwe na kampuni ya MEIS Industries katika mazingira yenye utata.

  Kampuni ya MEIS Industries inamilikiwa na wanandugu watatu ambao ni Islam Ally Saleh, Merey Ally Saleh na Saleh Ally Saleh.

  MEIS ilikuwa imeamriwa ichukue fedha hizo mali ya Serikali ya Libya, ilhali kukiwa na kesi ya msingi namba 110/2010 iliyofunguliwa na MeTL dhidi ya Serikali hiyo. Kumekuwapo msukumo mkubwa wa kisiasa na kidiplomasia wa kutaka MEIS ilipwe mabilioni hayo, ilhali ikiwa haina haki hiyo kisheria.

  Duru za kimahakama zinaonyesha kuwa MeTL walifungua kesi hiyo na kupeleka samansi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa iliyo chini ya Waziri Bernard Membe, ili kupitia kwake, afikishiwe Balozi wa Libya nchini. Hata hivyo, Wizara ya Membe katika namna ya kushangaza ilipokea samansi hiyo, lakini ikakataa kuiwasilisha kwa Balozi wa Libya.

  Imebainika kuwa, wakati kesi ya MeTL ikiwa inaendelea siku chache badaye MEIS Industries ilifungua kesi namba 124/2010 dhidi ya Serikali ya Libya ikitaka ilipwe dola milioni 20 za Marekani na gharama za usumbufu za dola milioni 14.

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ilitoa ushirikiano kwa kuhakikisha samansi inapelekwa kwa Balozi wa Libya nchini, tofauti na ilivyokuwa imeikatalia kampuni ya MeTL inayowakilishwa na wakili wa kujitegemea, Dk. Masumbuko Lamwai.

  Kesi hiyo ilisikilizwa upande mmoja wa walalamikaji na hukumu ikatolewa na Mahakama Kuu kwa kuamuru Benki ya TIB iilipe MEIS dola milioni 34 za Marekani.

  Katika namna ya kustaajabisha, Balozi wa Libya hapa nchini akijua wazi kwamba kuna kesi katika Mahakama Kuu dhidi ya Serikali ya Libya, hakuweka wakili wa kuitetea Serikali, na matokeo yake ndiyo yaliyowezesha kesi isikilizwe upande mmoja na kutolewa hukumu.

  Duru za uchunguzi zimebaini kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ilikuwa bega kwa bega na MEIS Industries pamoja na Balozi wa Libya nchini kuhakikisha kesi hiyo inaendeshwa na kufikia tamati kama ilivyotokea.

  MEIS Industries inamilikiwa na watu wanaotajwa kuwa na uhusiano wa karibu mno na baadhi ya maofisa waandamizi kabisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Imebainika kuwa TIB baada ya kuamriwa ilipe kiasi hicho cha fedha, ilikataa kulipa kwa maelezo kwamba haikuwa na ruksa ya kuzitoa.

  Kutokana na msuguano huo, MeTL walilazimika kuweka zuio mahakamani ili TIB wasiilipe MEIS Industries. Aidha, utata wa namna fedha hizo zinavyotaka kuchukuliwa umejitokeza pia kwenye mchakato wa kisheria ambapo wakili Joseph Thadayo ndiye mwanasheria wa MEIS, ndiye wakili wa Membe na amekuwa pia akilipwa na TIB kwa kazi za kisheria anazowafanyia. "Hapa kuna maswali mengi ya kuuliza juu ya uhusiano wa MEIS, Membe na Thadayo," kimesema chanzo chetu cha habari.

  Wakati baadhi ya vyombo vya habari vikiripoti kuwa MeTL inataka ilipwe
  fedha hizo kinyemela, imebainika kuwa MeTL ndiyo inayojitahidi kuzuia malipo hayo ambayo MEIS wanahaha kuhakikisha wanalipwa.

  Wakati Membe na Balozi wa Libya wakinukuliwa wakisema Massoud Mohamed Nasr, hatambuliki, MTANZANIA imefanikiwa kupata waraka unaoonyesha kuwa Nasr ndiye anayetambuliwa kwa nyaraka rasmi za Serikali ya Libya kukusanya madeni ambayo Serikali hiyo imekuwa ikiidai Serikali ya Tanzania tangu Februari 12, 1983. Uhalali wa Massoud upo hata kwenye nyaraka ambazo zipo katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  Nasr alishalipwa dola milioni nne za Marekani kama kamisheni kwa kazi hiyo, jambo ambalo Ubalozi wa Libya hapa nchini unalifahamu, na hivyo kuondoa dhana kwamba hatambuliki. Dk. Lamwai amemwandikia barua Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akimpa tahadhari juu ya kutowajibika kwake katika suala la kesi iliyofunguliwa na MeTL.

  Amemwandikia pia Balozi wa Libya juu ya uamuzi wake wa kutotaka kufanya mipango ya kuitetea Serikali yake katika kesi namba 124/2010.

  Katika kesi nyingine namba 110/2010 walalamikaji MeTL wamewasilisha mahakamani pingamizi dhidi ya wakili Kamara na kampuni ya The Crest Professional Attorneys kwamba hawana sifa ya kuiwakilisha MEIS Industries, kwa vile mwaka 2009 walitoa ushauri wa kisheria kwa suala hilo hilo lililo mahakamani.

  Shauri hilo halijatolewa uamuzi na Mahakama. Katika kesi namba 124/2010, MeTL pia imewasilisha pingamizi kama hilo kwa Kamara na kampuni hiyo na Jaji amemtaka Kamara asiwajibike kwa shauri kati ya MeTL na MEIS Industries.

  Katika hatua nyingine kampuni ya MeTL imelalamikia kitendo cha baadhi ya magazeti kumhusisha Mbunge wa Singida Mjini, Mohamed Dewji kwenye sakata hili. Ofisi ya Mwanasheria wa MeTL, imesema Mohamed si Mkurugenzi wala mwanahisa katika MeTL, bali mhusika ni Ghulam Dewji ambaye ni baba yake.

  "Mohamed kuwa na uhusiano na Ghulam kwa sababu ni baba yake haina maana kwamba ni Mkurugenzi au mwana hisa wa MeTL, tena habari zinazoandikwa zinamhusu Ghulam, lakini kwanini iwekwe picha ya Mohamed? Huu ni mpango wa kuchafuana.

  "Hatutaki suala hili liingiliwe kisiasa, kirafiki au kidiplomasia, Mahakama iachwe iwe huru kuamua, vyombo vya habari visitumiwe kupotosha ukweli," imesema taarifa ya mwanasheria wa MeTL.

  source:Mtanzania

   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  wao hawajali aibu....wanaandaa pesa za 2015,we unadhan hiyo kampun isingempa pesa MEMBEEEEE????
   
 7. M

  Marytina JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hapa mpango wa kumchafua Membe na kumsifia Asha Rose Migiro umeanza
   
 8. z

  zamlock JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  kazi kweli kweli
   
 9. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #9
  Jun 20, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mbopo aka Assah Mwambene uko wapi, amsha vijana wako waanze kazi huku maana mgombea wetu wa urais 2015 anaanza kusakamwa hapa.
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Atuambie mapema kama ana Power of Attorney ya hiyo kampuni.
   
 11. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #11
  Jun 20, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,246
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Hakuna aliyemsafi ndani ya club ya magamba!
   
 12. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #12
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Yupo london anakula BATA......
   
 13. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #13
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Mudhihir alipenda kutumia misemo na methali huku akinukuu kauli za wanafalsa na vitabu mbalimbali, mbali ya misemo yake kufurahisha, pia Mudhihir alikua fundi wa kufikisha ujumbe aliokusudia katika lugha nyepesi. Moja ya misemo itakayokumbukwa alipokuwa bungeni ni ule wa nyoka wa mdimu alioutumia akimlaumu waziri mmoja kuwa ndiye anayetaka kiwanda cha saruji kijengwe kilomita 35 kutoka eneo lenye malighafi ambalo ni Mchinga.
Alisema mtu huyo, anafanya hivyo kwa roho mbaya kwa kuwa hatanufaika lolote na msimamo wake kuhusu kujengwa kwa kiwanda hicho na kumfananisha na nyoka anayeishi kwenye mti wa ndimu ambaye hali majani yake wala ndimu, lakini anayekwenda kuchuma ndimu kwenye mti huo humng'ata.- Mwanachi,Novemba 2010
   
 14. Mzalendo

  Mzalendo Senior Member

  #14
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndio maanake, siasa za majitaka at its best nasinto shangaa kuona alhamisi jarida mama sijui dada la mtanzania (rai) nalo linaweza kuja na makala za kuuzunisha kuhusu mchezo mzima ulivyochezwa na membe,hila mara nyingi san haya majungu ya Mtanzania huwa yana backfire nakuwa marketing campaign ya bure kwa niaba mchafuliwa
   
 15. m

  mkuliakg New Member

  #15
  Jun 20, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sin hakika kama haya madai ni ya kweli au lah, ila kinachonitia wasiwasi ni gazeti ambalo limeripoti habari hii. sote tunajua kuwa gazeti la mtanzania linamilikiwa na Rostam na kazi yao kubwa ni kumsafisha Lowasa na kuwachafua watu wanaoonekana kuwa ni tishio kwake. Membe ni mmoja kati ya watu wanaonekana ni tishio kwa Lowasa since anatajwa kuwa na nia ya kugombea urais mwaka 2015. Sisemi kama ni habari za uongo ila nadhani uchunguzi wa kina unahitajika juu ya swala hili.
  nawasilisha
   
 16. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #16
  Jun 20, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  dawa ni kuing'oa serikali ya ccm madarakani. vinginevyo kila siku tutakuwa tunajadili ufisadi ufisadi ufisadi.
   
 17. W

  We know next JF-Expert Member

  #17
  Jun 20, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Na hawa wanasheria wa Tanzania credibility yao inakuwa question as well. Hivi huyu Joseph Thadayo si ndiyo aligombea ubunge wa CCM kura za maoni na Prof Maghembe kule Usangi (Mwanga)? Unajua nchi hii watu wamejisahau kuwa siku moja hayo magorofa na mashangingi yao ndiyo yatakuwa makaburi yao.
   
 18. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #18
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Membe hapo anachokitaka ni gawio.....hana kingine ndio maana analilia hiyo deal......na huyo Mo hadi amemlipua unaweza kukuta wana mgongano wa kimasilah
   
 19. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #19
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,094
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Mara membe anachafuliwa,mara ritz1 anamchafua january makamba,mara asha rose migiro anaandaliwa.duu,tutasikia mengi hadi kufikia 2015,Mungu atupe uzima! chadema jiandaeni kuchukua nchi,huku magamba wananyukana nyie nendeni kwa wananchi kuwaelezea sera zenu...by the time wanamalizana,watamkuta mwana sie wao,hvyo wataishia kueleka jiwe!
   
 20. K

  Kinto Senior Member

  #20
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 109
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Waache kugombana kwa ajili ya fedha zisizo zao, wafanye kazi watafute hela zao
   
Loading...