Uchaguzi 2020 Membe anaweza kutuvusha upinzani kuliko Lissu

Hapo ndio unaona umetuchota mawazo na akili zako za kiccm! Hata kama umeleta huu uzi kwa kejeli, kwanini usimkejeli huyo Membe aanzishe chama chake ili huo ubobezi wake uonekane? Au yeye ubobezi wake unaweza kuonekana kwenye vyama vya wanaume wenzake tu?
Tuache "double standard" Mbona EL hakuambiwa aanzishe chama?Si Mbowe wala Zitto anayeweza kukataa pesa kisa nyinyi wafuasi hamumtaki BCM
 
Nimefuatilia na kumsikiliza kwa makini sana Mh. Membe (jasusi mbobezi) na nimekubaliana nae kuwa anaweza kuwa mtu sahihi sana kuliko wagombea wengine wa upinzani.

Membe ana uwezo wa kujenga hoja na ikakubalika hii ni kutokana na ujasusi wake hivyo ni faida kubwa sana kwa Upinzani
Membe ana utumishi uliotukuka ukilinganisha na wagombea wengine wa upinzani, hivyo kuna faida nyingi kuwa mgombea wetu wa upinzani.

Membe ni mwanadiplomasia nguli na anaweza kuirudisha Tanzania mahali ilipokuwa kimataifa.

Membe ni karata turufu sana kwa wakati huu kwa kuwa ameshajimbambanua kupambana na Magu, hivyo ameshajiandaa na urais.

Upinzani tumpe nafasi membe apeperushe bendera yetu kuliko kuwaachia wengine ambao sidhani kama wana ushawishi kama Membe

#2020upinzani na jasusi mbobezi#
Atuambie kwanza faida tuliyopata kama nchi kutokana na safari nyingi sana za JK nje ya nchi alipokuwa Rais. Alituahidi.
 
Tuache "double standard" Mbona EL hakuambiwa aanzishe chama?Si Mbowe wala Zitto anayeweza kukataa pesa kisa nyinyi wafuasi hamumtaki BCM

Kwa taarifa yako mimi simsemei mtu, ila mimi nilipinga since day 1 huyo EL alipokuja cdm. Wanaweza kuchukua hela kweli maana wao ndio wenye maamuzi, lakini ni at the expense of their parties. Sisi wafuasi ndio nguzo yao ya kweli ya muda mrefu, na sio hizo hela za hao wazee wahuni.
 
Tuliza akili bro, huyu jamaa ni jasusi na ana mbinu zote za kuwezesha upinzani kushinda uraisi mwaka huu. Ni karata turufu
Kwenye mada hii naendelea kuona jinsi wale wanaojiita wasomi walivyokuwa na uwezo mdogo wa kufikiri...

Pia kitendo cha kuamini tu kwamba kiongozi bora anapatikana kwa kupiga kura peke yake ni uzumbukuku mkubwa sana.
 
Sina wasiwasi na Membe bt wasiwasi wangu upo kwa mtangaza matokeo je atakuwa tayari kutangaza matokeo kuwa Membe kashinda?
 
Alishindwa kutumia ujasusi wake wakati Swahiba wake JK akiwa Rais na mwenyekiti wa chama hataweza wakati huu mpinzani wake akiwa ameshikilia vyote viwili.
Tuliza akili bro, huyu jamaa ni jasusi na ana mbinu zote za kuwezesha upinzani kushinda uraisi mwaka huu. Ni karata turufu
 
Back
Top Bottom