Membe anapofanya kazi ya mwenguo

That's why Tanzania is very poor country in the world,and will still be poor forever and ever.I can't just imagine Minister for foreign affairs anaenda kumwaga sijui nani miss tanganyikeni kwenda china,huu ni utupu wa hali ya juu,yeyote anayetetea utumbo huu,ajiulize swali moja tu,why our nation is fuc.king poor?Nchi nyingine zipo busy kuleta maendeleo katika jamii zao,si manyangema tunarukaruka tu,mara miss,mara real madrid ije bongo,uzuzu huu.Halafu mambo ya kutoleana mifano ya US,naona hiyo haina maana kabisa,let Americans do whatever they can,lakini sio kila jambo mbona white house wanafanya nasi tufanye.Mbona basi bajeti yetu iwe tegemezi kwa 40%,Tanzania ililaaniwa na nani?Halafu ukitaka ujue tumelaani nenda kwenye sehemu za starehe,watu wanajigamba utafikiri tunaishi mwezini,kumbukeni tupo mkiani mwa dunia katika maendeleo,nani wa kufuta hii aibu?
 
Sikujua kama Membe kwenda kumuaga Richa kunakwamisha maendeleo....
Kama ni kweli basi nimejua ni kwa nini hatujaendelea maana hatujui hata ni nini kinachotufanya tusiendelee
 
That's why Tanzania is very poor country in the world,and will still be poor forever and ever.I can't just imagine Minister for foreign affairs anaenda kumwaga sijui nani miss tanganyikeni kwenda china,huu ni utupu wa hali ya juu,yeyote anayetetea utumbo huu,ajiulize swali moja tu,why our nation is fuc.king poor?Nchi nyingine zipo busy kuleta maendeleo katika jamii zao,si manyangema tunarukaruka tu,mara miss,mara real madrid ije bongo,uzuzu huu.Halafu mambo ya kutoleana mifano ya US,naona hiyo haina maana kabisa,let Americans do whatever they can,lakini sio kila jambo mbona white house wanafanya nasi tufanye.Mbona basi bajeti yetu iwe tegemezi kwa 40%,Tanzania ililaaniwa na nani?Halafu ukitaka ujue tumelaani nenda kwenye sehemu za starehe,watu wanajigamba utafikiri tunaishi mwezini,kumbukeni tupo mkiani mwa dunia katika maendeleo,nani wa kufuta hii aibu?

Hebu kuwa objective, kwani ni lazima kila kitu uwe against? Sioni umasikini unaletwaje hapa kwa Membe kwenda kwa ma miss. That is not logical. Nyie ndiyo mnaoleta umasikini kwa ku complicate hoja zisizo za msingi
 
Mimi sioni ajabu,kama kikwete mwenyewe ameamua kuingilia kazi za membe,je kwanini na yeye asiwaingilie wengine?ila isitafsiliwe vibaya!!!!!!!

Mr President is doing his work, Membe naye ili asipokee mshahara bure wacha afanye chochote aonekane yupo busy....
 
Membe ataka mashirika ya ndege yaajiri warembo

na Khadija Kalili
Tanzania Daima

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe, ametoa wito kwa wamiliki wa mashirika mbalimbali ya ndege kutoa ajira kwa warembo wanaomaliza muda wao ili kuienzi fani ya urembo hapa nchini.
Membe alitoa wito huo jana katika hafla ya kumkabidhi bendera ya taifa, Miss Tanzania 2007, Richa Adhia, ambaye anatarajiwa kuondoka nchini kesho kwenda China kwa ajili ya kinyang'anyiro cha kumsaka mrembo wa Dunia ‘Miss World' kitakachofanyika Desemba mosi mjini Sanya.

"Nachukua fursa hii kuyaomba mashirika yote ya ndege yaliyopo na yatakayokuja, kuwaajiri warembo, bila kuvisahau vituo mbalimbali vya televisheni na hoteli za kitalii, waongeze kigezo cha urembo kuwa kimojawapo katika utoaji ajira," alisema.

Membe alisema kuwa, lazima waajiri waongeze kigezo cha urembo na kutoa mfano wa mashirika ya ndege ya nje ambayo yameajiri wasichana warembo ambao wamekuwa kivutio kikubwa katika sekta ya biashara na kuvutia wateja.

Aliipongeza Kamati ya Miss Tanzania kwa kuendesha mashindano ya urembo bila kujali dini wala rangi na kutambua kuwa wote ni taifa moja, hivyo kwa pamoja waweke mikakati ya kuienzi fani ya urembo nchini kwa kuwatumia ipasavyo warembo.

Katika kile alichoamini kuwa kitawatangaza warembo na kuwaenzi, Waziri huyo aliahidi kuwa picha zao zitawekwa katika jalada la jarida la wizara yake litakalotoka kwa mara ya kwanza Desemba mwaka huu, litakalofahamika kama ‘Foreign Affairs Journal'.

Naye Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Emmanuel ole Naiko ambaye pia ni mlezi wa Miss Tanzania, alisema kuwa kituo chake kitampa DVD, VCD na vielelezo vingine vitakavyoitangaza nchi.
 
jamani mkiona hivyo mjue kazi hana...as bosi wake anafanya kazi zake za mambo hayo nje...so let him do that ila hachohofia hatukawii sikia jk siku ya mashindano akaenda na mkewe kuwawakilisha watz kumuangalia miss tz live..sio wazo la mbole jamani hili??
 
Back
Top Bottom