Membe ana ubavu wa kuyatangaza hadharani majina ya vigogo waliowekewa mabilioni Uswisi?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Huyu waziri ambaye inasemekana ni ndugu wa mbali wa mkuu wa kaya ni magumashi kabisa, kama alivyo huyo jamaa yake. Wote wawili ni mafundi wakubwa wa kupasia mipira, hawataki kukaa nayo.

Mpira wa sakata la meli kisha upasia kwa UN na EU. Kuina mengine bado anatafuta namna ya kupasi kama vile lile la hela za Libya.

Lakini kuna hili la vigogowaliowekewa mabilioni katika mabenki ya Uswisi ambayo mamlaka za nchi hiyo ya Ulaya inayo majina ya vigoigo sita wa hapa TZ. Kwa kuwa yeye ni waziri wa nje tunaomba alichangamkie hili, kama vile alivyolichangamkia la hela za rada -- si katika kutaka hela zirejeshwe hapa -- kwani hizo hela si mali ya wananchi wa TZ, ni mali ya makampuni ya nje waliowawekea vigogo wetu.

Kitu tunachotaka kutoka kwa Membe ni kupata hayo majina ya vigogo na kuyatangaza hadharani. Bila shaka hayo majina yameshakabidhiwa serikali ya TZ kwani itakuwa haina mantiki kwa mamlaka za benki za Uswisi kutangaza kuwepo kwa majina ya wala rushwa hao halafu iyakalie majina isiyakabidhi kwa nchi husika. haitaingia akilini hii!

Jee, Membe anaweza kuonyesha 'umahiri' wake na ubavu kwa kuitisha waandishi wa habari na kuyatangaza majina hayo? Sana sana atafanya danadana tu kwamba bado majina hayajapatikana.

Hawezi kabisa!!! na hapo ndiyo umagumashi wake utadhihirika.
 
Akiweza kuichangamkia kashfa hiyo na kuyaweka hadharani majina mimi nitamsapoti kugombea urais 2015. Sitanii!!!
 
membe alisahalizungumzia hilo, lakini katika kuhakikisha hela zinarejeshwa, na siyo kuwabaini akina nani vigogo hao na kuwashitaki mahakamani.
 
Membe ni mbabaishaji tu, tuone hayo majina. kama unavyosema, nadhani serikali yetu tayari inayo.
 
75.jpg

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar,Othman Masoud Othman amesema Zanzibar haikuwahi kutawaliwa baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964, akimshangaa Mbunge wa Singida Mashariki(CHADEMA) Tundu Lissu kudai Zanzibar imejitangazia uhuru,kauli hiyo sio sahihi.



“Mimi nimepata kusoma na kuangalia hiyo hotuba ya Mhe Tundu Lisu, lakini pia nimeona majibu ambayo yalitolewa na Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha(Waziri wa Ulinzi) aliyesema maeelzo ya Mbunge Lissu yamejaa hadaa na upotoshaji naungana naye” Aliliambia Baraza Mwanasheria Mkuu.


Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Othman alisema marekebisho 10 katika katiba ya Zanzibar yalifanywa baada ya hoja nyingi zisizojibika katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyokuwa ikieleza Zanzibar ni sehemu ya Muungano.
 
Ya Uswisi kama ya EPA, sana sana tutaambiwa wameambiwa warudishe na kusadikishwa kuwa wako katika mchakato wa kurudisha halafu ndiyo mwisho tena
 
Back
Top Bottom