Membe Amlipua Wenje

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,367
Wakati Bunge likipitisha bajeti ya makadirio ya matumizi Sh191.91 bilioni ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka wa fedha 2014/15 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, alitumia nafasi hiyo ‘kumchana' Ezekiel Wenje na kusema kuwa anatumiwa na mataifa ya nje.

Mbali na hivyo aliwaita watu wanaotoa kauli za uchonganishi kuwa ni wapumbavu na akataka waache tabia za kipumbavu kwani hawatavumiliwa hata kidogo.

Membe alitoa kauli hiyo jana jioni wakati akitoa majumuisho katika michango ya wabunge kwenye hotuba ya mapato na makadirio ya wizara hiyo kwa mwaka 2014/15.

Wenje ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa jana asubuhi katika hotuba yake, alimshambulia Membe kuwa ni waziri mzigo ambaye hajui wajibu wake.

Sakata hilo liliibuliwa kwenye uhusiano baina ya Tanzania na nchi ya Rwanda ambalo Wenje alilizungumzia zaidi.

Akijibu hoja hizo Membe, alisema: "Kwanza nikubaliane na kauli ya wabunge wengi kuwa uhusiano wa Tanzania na Rwanda siyo mzuri kwani kila upande haumuamini mwenzake," aliema Membe.

Alisema kinachowaumiza pande zote ni kuwa kila upande unapozungumza na mahasimu wa mwenzake, wanahisi kuwa anataka kuipindua Serikali yao hivyo bado hawajakubaliana kwa jambo lolote lakini akasema yote yatakwisha salama.

"Huwezi kusimama hapa mtu na macho yakakutoka halafu unaanza kulizungumzia taifa lingine ambalo siyo lako, hivi unatoa wapi ujasiri huo au wanakulipa,"alihoji Membe na kuongeza.

"..Mimi naweka rehani uwaziri wangu hapa kwamba ukileta vielelezo kamili mimi nitakuwa tayari kuachia nafasi yangu, je na wewe nikitoa vielelezo utakuwa tayari kuwajibika."

Alimtaja Wenje kwa jina kuwa alichokifanya hakifai kuwa alitoa kauli ambayo siyo nzuri kwa siri za taifa na akasema mtu kama huyo akipata nafasi hata kama nchi itakuwa vitani, yuko tayari kutoa siri.

Aliyataja makundi ya ya M23 kuwa ni moja ya kundi ambalo linaundwa na Banyamulenge waliokuwa chini ya Laurent Nkunda pamoja na kundi la FDLR ambalo liliua watu wengi kwamba linaundwa na Wahutu bila ya ubishi.

Membe alimpongeza mbunge Alli Keissy kuwa alichokizungumza jana asubuhi kuhusu Rwanda na DRC Kongo ni sahihi na ndiyo maana alimshangilia kwa nguvu zote.

Source: Mwananchi
 
Kwa upuuzi alioongea awenje jana, nitashangaa kama kuna chombo cha habari makini kitamtetea
 
P4P ie "Pay for Performance" and BRN "Big Results Now" huwa zinaendana na kulandana... naona strategists wa Lumumba wame merge P4T (pay for threads) na Big mashuuZ-el-LemutuZ Now" BMN... So P4T & BMN ndo mpango mzima ee...
 
Wenje ni mvuta bangi muhuni wa kule Igogo ya juu, kazi yao ni kuvuta bangi na kukaba watu kule Igogo.
 
P4P ie "Pay for Performance" and BRN "Big Results Now" huwa zinaendana na kulandana... naona strategists wa Lumumba wame merge P4T (pay for threads) na Big mashuuZ-el-LemutuZ Now" BMN... So P4T & BMN ndo mpango mzima ee...
Pole sana Mkuu.taarifa hiyo imeandikwa na Gazeti la Mwananchi
 
membe haaminiki.leo M23 wakichukua madaraka congo membe atakuwa wa kwanza kuwaalika Tz kuzungumzia kuimarisha uhusiano!
 
P4P ie "Pay for Performance" and BRN "Big Results Now" huwa zinaendana na kulandana... naona strategists wa Lumumba wame merge P4T (pay for threads) na Big mashuuZ-el-LemutuZ Now" BMN... So P4T & BMN ndo mpango mzima ee...

za masiku! nilijua umeacha bangi kumbe ndo unazichanganya na viroba.
 
wenje mara nyingi haongei kama kiongozi anaongea kama mvuta bangi.dunian kuna watu.

hivi wewe,kesy na wenje nani mvuta bangi? kesy ndio mvuta bangi na diplomasia haijui. wewe ni kanjanja na hufuatilii bunge. kama ulisikiliza bunge wenje aliongea vitu vya msingi visivyo fungamana na nchi yoyote lakini huyu kichaa mwenzako kesy ndio sifuli kabisa kwa kuishambulia rwanda wazi wazi. lakini sishangai maana siku hizi ccm mmeanza kunywa pombe za kienyeji
 
membe haaminiki.leo M23 wakichukua madaraka congo membe atakuwa wa kwanza kuwaalika Tz kuzungumzia kuimarisha uhusiano!
Tanzania runaheshimu matakwa ya wananchi wa nchi nyingine. Hatuna budi kuunga mkono na kuwakubali viongozi wanaoteuliwa kidemokrasia. Ila Mkuu, sahau kabisa M23. Kama mlikuwa na ndoto za M23 kutwaa madaraka nchini DRC, hizo ni ndoto za Alinacha
 
hivi wewe,kesy na wenje nani mvuta bangi? kesy ndio mvuta bangi na diplomasia haijui. wewe ni kanjanja na hufuatilii bunge. kama ulisikiliza bunge wenje aliongea vitu vya msingi visivyo fungamana na nchi yoyote lakini huyu kichaa mwenzako kesy ndio sifuli kabisa kwa kuishambulia rwanda wazi wazi. lakini sishangai maana siku hizi ccm mmeanza kunywa pombe za kienyeji
Wenje ni mvuta bangi na ukichanganya kuwa si raia wa Tanzania hapo unapata picha kamili. Kessy havuti bangi ila ni fyatuuu ile mbaya
 
WEJE SI MTANZANIA SI MAAJABU KUKOSWA UZALENDO NA TANZANIA,hajui chochote kuhusu nchi,nazan hata huo uwaziri kivul kapewa kwa sababu anatoka nje ya tanzani.,MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
tusiwe wapumbavu kushabikia ujinga, kwenye ukwel tunasema, pumba tunasema bla kujari pande zetu, utaifa do gunzo yetu,hvi weje aliyo wasilisha kwel mazur,weje mbuge wangu nanmpenda ila leo katereza akili,AU SABABU SI RAIA WA KUZALIWA,NDO MAANA HANA MCHUNGU NA NCHI,maana mda wowote anaweza kwenda kwao kenya TZ pakichafuka
 
wenje apimwe DNA yake kuthibitisha kama ni mtanzania halisi - lakini pia hii njaa ya viongozi wa juu wa chadema itaipeleka nchi pabaya - inaelekea wapo kwenye payroll ya kagame!! watu wenye madeni lukuki na watu walioihujumu ATCL kwa kuirundikia madai feki lazima watafute njia haramu za kupata kipato kwa kuwa makuwadi wa watu kama kagame - hapa namlenga mbowe aliesema ugoro wa wenje ni kauli ya chadema
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom