Membe "akiri" nia ya kikwete kuendeleza hoja tata akichaguliwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Membe "akiri" nia ya kikwete kuendeleza hoja tata akichaguliwa?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtaka Haki, Oct 24, 2010.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika Hali ya kushangaza na kushtusha. Membe ameenda mkoani Mwanza kwa nia ya kukanusha "uvumi" anaosema unaenezwa na walioshindwa kupata urais ndani ya CCM.

  Uvumi aliosema unaenezwa na wapinzani wa Kikwete ni kuwa eti ameendeleza udini kwenye serikali na pia ameshindwa kuwashughulikia mafisadi.

  Kilichoshangaza hapa ni kuwa badala ya kuthibitisha madai hayo kuwa ni ya uongo alichofanya ilikuwa ni kuthibitisha kuwa ni kweli.

  Suala la mafisadi sio uvumi ni jambo ambalo kila mtu analielewa na hata watoto wadogo kuwa serikali imeshindwa na sio kushindwa imeamua kulikumbatia kwa nguvu zote. Niliwahi kusema tena kuwa kama unasema unapambana na ufisadi na kutoa mfano kuwa umewapeleka mahakamani kisha unarudi na kuwasemea wale uliowapeleka mahakamani kuwa ni watu safi na wanatakiwa kuchaguliwa waje wakusaidie serikalini, hiyo ni nini?
  Hapo ni kutoa ushahidi kwa majaji na mahakimu na wananchi kuwa mimi rais siamini kuwa watu hawa wanaweza kupatikana na hatia. Ni WASAFI.

  Suala la udini ndilo ambalo wengine wangekuwa hawalielewi vizuri. Kwa bahati nzuri ila kwa kushangaza Waziri Membe ameonyesha kukiri kuwa bado mpango wa Kikwete ni kuendeleza hoja hizi tata na bila aibu Membe anajaribu kuwaandaa viongozi wa dini. Soma habari hii hapa chini penye rangi nyekundu.
  Je Rais wetu bado anajitakia mema? Je anaitakia mema nchi hii.
  Kama kitu kina utata kuhusu udini kwa nini tusiache?
  Hakuna wenye shida na ndugu na ukristo au uislamu. Swali ni kuwa hatukuwa na matatizo bila OIC na hata mahakama ya kadhi. Huu umuhimu unaojitokeza wakati wa utawala wa JK ni wa nini mkubwa hivyo? Je kama ni pesa hizo tunazowaachia EPA na RICHMOND na RADA na MEREMETA nk . Je sio pesa. Ingekuwa kama hizo nyingine zinatafutwa kwa bidii kukusanywa na kulindwa basi yungejua kweli shida ni pesa. Watanzania huu ni wakati wa kufanya maamuzi ya kuliponya taifa hili.

  Membe atetea serikali kwa maaskofu
  Saturday, 23 October 2010 19:07
  Source Mwnanchi:

  Frederick Katulanda, Mwanza
  WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema CCM imegawanyika makundi mawili, moja likiwa ni lile la viongozi walioshindwa kuupata urais na lingine likiwa ni lile la Kikwete na serikali yake.

  Alisema kundi lililoshindwa na Kikwete kupata urais ndilo limekuwa likisambaza ujumbe na taarifa za kumchafua Kikwete na serikali yake kuwa ameshindwa kuwashughulikia mafisadi na kuigeuza nchi hii kuwa ya kidini kwa kuteua viongozi wengi wa ngazi za juu nchini waislamu.

  Membe alijikuta akieleza hayo wakati alipokuwa akijibu maswali ya viongozi wa dini na madhehebu ya kikristo kuhusu masuala mbalimbali aliyoyazungumzia kuhusu ufisadi, udini na serikali kujiunga na IOC .

  Alisema kutokana na uvumi huo kuenezwa zaidi wakati huu wa kampeni ameanza ziara ya kupita mikoani nchini kuzungumza na viongozi wa dini kusafisha hali hiyo ya hewa.

  Katika kikao hicho kilichofanyika Hoteli ya G and G jijini Mwanza juzi na kuhudhuriwa viongozi wa madhehebu ya kikristo zaidi ya 100, Membe alisema alikuwa na mambo manne ya kufafanua ambayo ni tuhuma za kuwepo kwa udini, ufisadi, suala la Tanzania kutaka kujiunga na OIC na pamoja na kuanzishwa ka mahakama ya Kadhi nchini.

  “Wakristo wanaonekana kujitenga wakidai kuwa Kikwete kaonyesha mpasuko kwa kupendela waislamu katika serikali yake na kuwa ifikapo mwaka 2015 Tanzania itakuwa imejiunga na OIC na kuanzishwa kwa mahakama ya Kadhi na mengine yakidai kuwa ameshindwa kushuhgulikia ufisadi hapa nchini, mambo haya siyo kweli.” alisema

  Ingawa Membe alikanusha Tanzania haijafikia uamuzi wa kujiunga na OIC aliwataka viongozi hao kukubaliana na suala hilo kwa vile zipo faida nyingi ambazo nchi itapata na kutaja mojawapo kuwa jumuiya hiyo inazo fedha nyingi hivyo itawasaidia kutatua matatizo waliyonayo.

  Membe alizitaza baadhi ya nchi akidai kuwa zimenufaika na OIC na kusisitiza kuwa kujiunga nayo hakuna masharti ya kuigeuza nchi kuwa ya Kiislamu bali ni kuwa na idadi ya waislamu wasiopungua asilimia 60.

  Alikaririwa akidai kuwa serikali haina udini na kwamba kuanzishwa kwa mahakama ya Kadhi hakutaibadili nchi kuwa ya kidini na kubainisha kwamba katika utawala wa Kikwete amekuwa akipambana na ufisadi kinyume na inavyoelezwa na watu.

  Kutokana na maelezo hayo ya Membe, kilifika kipindi cha viongozi hao kueleza ya kwao ambapo mchungaji mmoja alianza kuzungumza kwa kutumia msemo wa Biblia kuwa kauli anayoitoa Membe kumsemea Kikwete wakati huu wa uchaguzi ni sawa na ‘Sauti iliayo nyikani’ na kutoboa kuwa Membe hakupaswa kuyaeleza yeye bali Kikwete.

  “Hapa tunasikia sauti inalia nyikani, sasa hatumuoni mtu anayelia, wakristo tunataka kumsikia yeye mwenyewe na siyo kutuma mtu bali aseme yeye kwa kinywa chake hadharani kuwa Tanzania hakuna udini na nchi haitajiunga na OIC.” alisema mchungaji mmoja akimueleza Membe.

  Kwa upande wa mafisadi mmoja wa viongozi hao wa dini walikaririwa akimuuliza iwapo ana dhamira ya kupambana na ufisadi ni kwa nini ameweza kusimama hadharani na kuwashika mkono akiwaombea kura baadhi ya watuhumiwa, ambao serikali yake imewafikisha mahakamani huku akitolewa mfano wa nchi ya Malawi ambako waziri mmoja amefilisiwa na kukamatwa kutokana na ufisadi.

  Mmoja wa viongozi hao wa dini alimtahadharisha Membe kuwa anapaswa kutambua kuwa Watanzania wa sasa siyo sawa na wale wa zamani na kwamba sasa anapaswa kuwajibu vyema wapouuliza.
  Walisema iwapo anasema faida ya kujiunga OIC ni kwa ajili ya kupata fedha za kusaidia taifa na kuhoji taifa limeshindwa vipi kunifaika na raslimali zake kama madini kiasi cha kuhitaji fedha za OIC.
  “Membe alisema mambo yote ambayo ameyazungumzia na kwao yamezushwa wakati huu wa uchaguzi na kubainisha kuwa wanaozusha ni kundi la waliokosa uongozi ndani ya CCM.

  Hata hivyo, nje ya hoteli hiyo Membe alipotakiwa na waandishi wa habari kuzungumzia kikao chake na viongozi wa dini, alikataa na kuwakimbia ambapo alijikuta akiliacha gari lake na kuingia gari la mkuu wa mkoa wa Mwanza ambaye alimkumbusha kuwa hilo halikuwa gari lake na kurudi kuingia gari lake na kuondoka.
  Naye Mwenyekiti wa Umoja wa dini na Madhehebu ya Kikristo, Charles Sekelo ambaye ni Askofu wa Kanisa la CECT, alipoulizwa kuhusuna na kikao hicho alikiri kuzungumza kwa mambo hayo na kueleza kwamba Membe alidai alikuwa akimsafisha Kikwete kutokana na kuvuma kwa mambo machafu.

  “Kwa maneno yake Membe alisema maduhumuni ya kikao chake nasi ilikuwa ni kusafisha juu ya mambo hayo, alidai yameuwapo mambo mengi mchafu ya kumchafua Kikwete na CCM, na kumbe alikuja kusafisha.” alieleza Askofu Sekelo.

  Kwa upande wake Mwakilishi wa Kanisa la Anglikana katika kikao hicho, Geoffrey Salum alisema, Membe alikuwa akijaribu kuwashawishi viongozi hao kujenga imani na serikali.
  “Membe hajafanikiwa kutokana na msimamo wa viongozi wa dini ulivyokuwa ndani ya ukumbi huo, kwani ameshindwa kukidhi haja ya maswali yao na diyo maana wengi wamemweleza wazi kuwa wanataka Kikwete mwenyewe akiri hakuna udini nchini,” alieleza Salum.

  Hata hivyo, Mchungaji David Emanuel wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, alisema katika kikao hicho wametoa dukuduku lao na kueleza wazi kuwa hawaafikiani na serikali yake.
   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Kuna hoja za maana hapa. Serikali ya awamu ya nne inayumbusha Taifa, na mmoja wa wayumbishaji ni mawaziri. It does not make any sense kusema uombe misaada wakati una uwezo wa kujitegemea? NI kweli kujiunga na OIC ni kwa ajili ya misaada? Since when Membe ameanza kuendekeza kuomba misaada? How can we advocate umatonya?
   
 3. coby

  coby JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2010
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 342
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndio dawa yao wapuuzi hawa, yaani wametufanya kila mtu hana akili.
   
 4. coby

  coby JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2010
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 342
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndio ubaya wa wasomi wengi waliopewa position za juu kila kitu ndio mzee. Shame upon you Membe!
   
 5. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni CCM ninayoijua, la ajabu lipi?
   
 6. T

  TumainiEl JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 2,895
  Likes Received: 1,649
  Trophy Points: 280
  Lipo tatizo na mwisho wake moto utawaka..
   
 7. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  siku zote huwa nafikiri Membe anabusara ,kumbe ni kazi bure!
  duh ni aibu sana hata kusimama mbele ya wazee na maaskofu kutoa pumba kama hizo.
  Halafu huyo Kiwete hivi bado mnataka kujiunga na OIC???
  Kikwete mbona hutaki kuelewa? unalazimisha mambo??
  ngoja tusubiri tuone:embarrassed1:

   
 8. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  I think the last thing to do litakuwa ni kumvua madaraka,
  anachotaka huuyu ni kupigiwa kura na wabunge ya kutokuwa na imani naye,
  and of course we are going to do that kama akiendeleza sera zake hizo za udini.
  mnataka kutuingiza kwenye migogoro ya dini kisa ni misaada?
  je tumeshapokea misaada mingapi tanzania? je kuna mabadiliko gani?
  bora hata tungewekewa vikwazo kama nchi zingine labda tungeweza kuwa na akili,maana sasa nchi na viongozi wote wanategemea tu misaada,hii ni aibu ndio maana wanahubiri neti kila siku kumbe hiyo ndio waliyokuwa wanatembea na mamilioni ya walipakodi ili kuwaletea neti.
  kama hizo safari wangeziacha je wasingenunua neti wao wenyewe bila kutegemea kusaidiwa?
  hivi tutabadilika sisi lini?
   
 9. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Wanajiona wamesoma sana na wanaijua sana nchi hii kuliko sisi
  mbona hawazijui kura zetu na wanakuja kuziomba? si wangetumia usomi wao wa KISHETANI kuchukua hizi kura zetu???

  Safari hii wameumia
  napadwa hasira mpaka nawatukana kwamba ccm ni WASHENZI kuliko tunavyowafahamu. Wapo tayari kuwaga damu zetu ili wapate uhalali wa kutawala na sio kuongoza
   
 10. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata waislamu wenyewe na busara zao wengi hawaoni ni kwa nini kama siku zote wameishi bila matatizo kwa nini umuhimu uwe mkubwa leo.
  Kuna mliosema labda itabidi bunge limpigie kura ya kutokuwa na imani nae.
  Kura ya kutokuwa na imani nae inatakiwa ipigwe jumapili ijayo kusema hatuna imani na wewe. Uongozi umekuwa mzigo na tunakupenda na tunakutakia mema hivyo ondoka ili yasikukute mabaya yatakayowahusisha na watanzania wengine waio na hatia.
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Yaelekea JK na CCM yake wana mambo yao ya usiri ambayo wametuficha wapigakura na kuwaamini haha mafisadi siyo rahisi hata kidogo..
   
 12. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  NI MUHIMU MNO rAIS Kikwete aendelee kubanwa athubutu kutamka kuwa hana ajenda za siri ZA oic na mahakama ya kadhi.
  Akidhani atasifiwe na waislamu. ALIWADANGAANYA WAISLAMU AKAWEKA MPAKA KWENYE ILANI SASA ANAKATAA KUWAJIBIKA ANATAKA KUSINGIZIA KUWA WABAYA NI WAKSTO. NASIKITIKA MNO MNO KUONA VIONGOZI WANAOCHEZEA MASUALA YA IMANI.
  Waislamu wenye busara hawawezi kukubali ujinga wa DIVIDE AND RULE KATIKA ULIMWENGU HUU WA LEO.
   
 13. DCONSCIOUS

  DCONSCIOUS JF-Expert Member

  #13
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Hivi ni asilimia ngap ya wakristo Tanzania? Mbona wanashikwa maskio sana?
   
 14. DCONSCIOUS

  DCONSCIOUS JF-Expert Member

  #14
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Hivi ni asilimia ngap ya wakristo Tanzania? Mbona wanashikwa maskio sana?
   
 15. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #15
  Oct 24, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  kuna uwezekano mkubwa kuwa idadi ya waislamu Tanzania ni kubwa. Kwanza kwa sababu ya rate ya kuzaana ya waislamu ni kubwa zaidi. Kwa kuwa kuna baadhi wana wake hata wanne wakati si wakristu wengi wenye haki kama hiyo, na wapagany wanaopractice polygamy wanaapungua. Lakini idadi ya wakristo si ndogo kiasi cha kuifanya Tanzania ikubali kiurahisi kuwa nchi ya kiislamu au kuwa part ya dunia ya kiislamu. Na idadi ya waislamu pia ni kubwa kiasi cha kuifanya Tanzania isiwe part ya dunia ya kikristo na kuwa kama Uingereza yenye state religion. Kuna wapagani wengi tu, wanadini hewa (non-practicing Christians and muslims) ambao wanaona ni bora tukiwa kama tulivyo sasa.
   
 16. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #16
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  NI UKWELI USIOPINGIKA kuhusu mambo ya UDINI KAMA Inavyozungumzwa ktk kipindi hiki cha uchaguzi basi wa KULAUMIWA NI SERIKALI YA CCM ya AWAMU YA NNE ambaye kiongozi wake ni JK. Kwa mtu analytical hupati shida kupambanua hilo. Mathalani, katika awamu tatu zilizopita kama Udini ulikuwepo (of which I believe otherwise) basi ulikuwa contained kwa maana ya utawala kutoa leadership. Kwa msingi huo tunachoona sasa ni failure ya leadership ktk nchi ndio maana tunayasikia haya. Serikali ingekuwa responsible kusingekuwapo na swala kama Mahakama ya kadhi kupelekwa bungeni period. Serikali ilishindwa kutoa leadership ili hilo swala lijadiliwe ndani ya cycles za dini husika na siyo bungeni.
   
 17. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #17
  Oct 24, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,993
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Membe kwa sasa hivi(hapo kwenye nyekundu) tunaweka kwenye faili mpaka 2015 utueleze kwa nini unaamini misaada ndio itatuondoa kwenye umaskini na sio rasilimali lukuki tulizo nazo.
   
 18. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #18
  Oct 24, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,827
  Likes Received: 10,128
  Trophy Points: 280
  Mungu tuokoe baba
   
Loading...