Membe akiri kuwa Magufuli ni dhaifu (ni sawa na timu dhaifu)

MNYAMU ZE KB

Senior Member
Nov 17, 2014
149
64
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amefunguka kwa mara ya kwanza na kuweka wazi kilichotokea mjini Dodoma na kusababisha ashindwe katika uteuzi wa kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Membe amekuwa kada wa tatu kueleza hadharani jinsi uteuzi huo ulivyoendeshwa ambao Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, aliibuka kidedea kati ya makada 42 waliojitokeza kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa.

Makada wengine waliojitokeza hadharani kuelezea mchakato huo ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya, ambao kwa nyakati tofauti walieleza sababu mbalimbali zilizosababisha kushindwa kwao

Membe akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika kongamano la pili la Watanzania waishio ughaibuni (Diaspora), alisema mchakato huo ulikuwa ni sawa na timu mbili za mpira wa miguu zilizokuwa zinapambana uwanjani.

Alisema unaweza ukapata timu nzuri sana ya mpira kwenye ligi na ikashinda michezo yote bila kufungwa goli hata moja. Aliongeza kuwa lakini mwishoni timu hiyo inapotoka sare na timu nyingine ambayo ni dhaifu kwenye fainali, timu hizo zinakwenda kwenye penalti kwa kuwa mshindi lazima apatikane.

Membe alieleza kuwa wakati wa upigaji penalti timu hiyo ambayo ilitarajiwa kuibuka na ushindi kwa kuwa ilicheza mpira safi ikafungwa penalti zote tano na hiyo timu ambayo haikutegemewa ikashinda mabao yote.

Alisema kuwa kwenye ‘football jargon' kitendo hicho cha timu iliyocheza mpira vizuri na kudhaniwa ingeibuka na ushindi,lakini ikashindwa kwenye penalti,
timu hiyo imekufa kifo cha ghafla.

Membe aliendelea kueleza kuwa timu hiyo itakuwa imepigwa kifo cha ghafla na kueleza kuwa inapopigwa kifo cha namna hiyo timu hiyo haiwezi kutegemewa isimame na ielezee kilichotokea. "Naomba leo nitumie nafasi hii kwa mara ya kwanza kuelezea kilichotokea mjini Dodoma katika uchaguzi wa nafasi ya urais kwa Chama Cha Mapinduzi na nadhani sitaulizwa tena," alisema Membe.

Mfano huo huenda ukahusishwa na wanachama wa CCM waliokuwa wanamuunga mkono Membe kama timu iliyokuwa inatumainiwa ingeshinda mchakato huo, huku Dk. Magufuli akielezwa kama timu ambayo haikudhaniwa kushinda kinyang'anyiro hicho kutokana na kutokuwa na makundi yaliyokuwa yanamuunga mkono. Membe alikuwa na kundi kubwa.
 
Mwenyekiti dhaifu na legelege.... chama kimekuwa dhaifu na legelege...
Yaani chama cha zamani hakiwezi kukwepa utabiri wa Hayati Mwl. JK Nyerere...!!
 
Kikwete aliwaeleza kuwa, ikitokea CCM akashndwa ni sawa tu.Kuna vyama vingne,nı vya Watanzania na wao wana haki ya kuongoza.Nionacho kwa Lowasa si mvuto wa asili bali wa Uchawı kutoka kwa TB JOSHUA.
 
Mleta mada ana hang over ya viroba vya jana alivyokunywa mkutanoni Mbeya. Hata heading kakurupuka nayo tu, "mafufuri" ndio yupi? Si tunayemjua ni kipenzi cha watu Dr John P. Magufuri.
 
Mleta mada ana hang over ya viroba vya jana alivyokunywa mkutanoni Mbeya. Hata heading kakurupuka nayo tu, "mafufuri" ndio yupi? Si tunayemjua ni kipenzi cha watu Dr John P. Magufuri.

Sema kipenzi chako mkuu siyo kipenzi cha watu wengine ata awamjui
 
Jamani atarudi vp mtama alishaligawa jimbo na kama angetaka angekwenda lindi mjini palikuwa tupu na angeshinda ila kaamua kupumzika afanye yake msikurupuke tu kumjadili mtu bila ushaidi
 
nadhani huo udhaifu anaousema membe angeuweka wazi hapa kwani naona vitu viwili hapa ambavyo anaongelea ndugu membe. moja ni udhaifu wa timu moja ambayo inafahamika ya kuwa siku zote inapocheza inapoteza mchezo kutokana na kiwango kidogo cha wachezaji wa timu hiyo, pili inaonekana ni udhaifu wa kutokuwa na makundi ambayo kwa mujibu wa membe ni kuwa ndugu pombe magufuli hakuwa na makundi ya kumusaidia katika harakati za kuibuka kidedea, suala la msingi hapa ni kuwa kama kweli huyu pombe hakuwa na makundi ya kumsaidia kuvuka katika kinyang'anyiro hicho, aliwezaje kuibuka kuwa mgombea wa urais? pia napata shida katika kauli ya kwanza ya kuwa ndugu pombe anafananishwa na timu dhaifu ya mpira na hili kwa uelewa wangu lipo kiutendaji zaidi, je leo hii tukilinganisha utendaji wa membe serikalini na magufuli kwa vipindi vyote ambavyo wamekuwa katika sekta zao ni nani ambaye anaweza kulinganishwa na timu dhaifu ya mpira? ukweli utaendelea kubakia ukweli hata kama utapindishwa namna gani nadhani ndugu membe angetafuta maneno mengine ya namna ya kumsema pombe na siyo kumfananisha na timu dhaifu ya mpira, ni yangu tu maoni najaribu kungalia uhalisia wa hili jambo unasimama wapi, nafikiri pia tunapokuwa tunaleta maada kama hii tuwe tunajaribu kuangalia katika sehemu zote mbili na kutoa hitimisho mwishoni ili wasomaji waweze kuelewa na kulinganisha pande zote kwa uelewa zaidi
 
Membe alishindwa kidemokrasia kabisa..sioni hicho kifo cha ghafla kinatoka wapi.
 
Asiyemjua Magufuri, labda hajawahi kupita barabarani.

Barabara nyingi ziko chini ya kiwango mfano mzuri ni kilwa road imejengwa ndani ya miezi sita imeshafumuka wa
naweka viraka sasa.

Tazama sasa wanajenga barabara feki kwa pesa za mikopo ,deni la taifa limefika trilion 36 toka 9 za mkapa!!!

CCM ni mfumo hovyo yatosha sasa..
 
There was no sudden death. There were no penalties. Mfano wake hauna mantiki na ufafanuzi uliotoa pia hauna mantiki. Mfano aliotskiwa kutoa ni wa mbio za farasi au hata wa mbio za marathon. . Kwenye mbio hizo watu wanakuwa wamegawanyika katika makundi yanayounga mkono mshindani fulani. Lakini mwisho wa mbio anaweza kutokea mshindi ambaye hakutarajiwa na wengi.
 
Back
Top Bottom