Mema ya awamu ya tano ni matokeo ya dhamira njema ya Rais na sio kelele za upinzani

jaruri

JF-Expert Member
Jul 16, 2014
716
459
Ndugu zangu watanzania nimekuwa nikisikia kelele nyingi kwenye vyombo vya habari kutoka vyama vya upinzani.
Nipende kutumia fursa hii kuwakumbusha watanzania wenzangu kuwa haya mema tunayo yaona katika serikali ya awamu ya tano ni matokeo ya dhamira safi ya rais wa awamu ya tano.Rais anatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kwa vitendo na ilani hii imeainisha kabisa kipi kinatakiwa kifanyike lini,wapi na kivipi.

Rais huyu amekuwa tofauti na marais walomtangulia,kafanya mengi mema tena makubwa.Kama vile:
  1. Elimu bure
  2. Nidhamu ya watumishi
  3. Kudhibiti rushwa na kuanzisha mahakama ya mafisadi
  4. Kulinda madini yetu na kuleta miswada mipya yenye lengo la kuleta maendeleo
  5. Ndege mpya
  6. Reli ya kisasa
  7. Upatikanaji wa madawa hospitalini
Huko nyuma upinzani ulikuwepo,jiulize kwa nini matokeo makubwa chanya tumeyaona katika awamu hii? Hapo ndipo ninapojenga hoja yangu kuwa Mema yote unayo yaona sasa katika awamu ya tano ni matokeo ya udhubutu,uzalendo na dhamira ya njema ya Rais wa awamu ya tano.

Niwakumbushe tu wapinzani kuwa ifike mahali wamuunge mkono Rais katika yale yalokuwa mema;watafute namna nzuri ya kutoa ushauri.Kupinga kila kitu sio njia nzuri ya kujenga nchi bali ni namna ya kutafuta umaarufu tu.Watanzania wanahitaji maendeleo sio siasa.
 
hiyo namba moja, kuna mtu mmoja yatima leo alikuwa anasema bila elimu bure sijui zile ada za tsh 20,000 kwa sekondari za kutwa wadogo zake wangezitoa wapi...
leo anamshukuru Mungu kwa maamuzi ya Rais yanayosababisha mdogo wake kumaliza form four mwezi ujao.
hiyo naiita orphan based development
 
Ubaradhuli uliokubuhu huu. Fisadi aliye Ikulu apambane na mafisadi,

Ndugu zangu watanzania nimekuwa nikisikia kelele nyingi kwenye vyombo vya habari kutoka vyama vya upinzani.
Nipende kutumia fursa hii kuwakumbusha watanzania wenzangu kuwa haya mema tunayo yaona katika serikali ya awamu ya tano ni matokeo ya dhamira safi ya rais wa awamu ya tano.Rais anatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kwa vitendo na ilani hii imeainisha kabisa kipi kinatakiwa kifanyike lini,wapi na kivipi.

Rais huyu amekuwa tofauti na marais walomtangulia,kafanya mengi mema tena makubwa.Kama vile:
  1. Elimu bure
  2. Nidhamu ya watumishi
  3. Kudhibiti rushwa na kuanzisha mahakama ya mafisadi
  4. Kulinda madini yetu na kuleta miswada mipya yenye lengo la kuleta maendeleo
  5. Ndege mpya
  6. Reli ya kisasa
  7. Upatikanaji wa madawa hospitalini
Huko nyuma upinzani ulikuwepo,jiulize kwa nini matokeo makubwa chanya tumeyaona katika awamu hii? Hapo ndipo ninapojenga hoja yangu kuwa Mema yote unayo yaona sasa katika awamu ya tano ni matokeo ya udhubutu,uzalendo na dhamira ya njema ya Rais wa awamu ya tano.

Niwakumbushe tu wapinzani kuwa ifike mahali wamuunge mkono Rais katika yale yalokuwa mema;watafute namna nzuri ya kutoa ushauri.Kupinga kila kitu sio njia nzuri ya kujenga nchi bali ni namna ya kutafuta umaarufu tu.Watanzania wanahitaji maendeleo sio siasa.
 
hiyo namba moja, kuna mtu mmoja yatima leo alikuwa anasema bila elimu bure sijui zile ada za tsh 20,000 kwa sekondari za kutwa wadogo zake wangezitoa wapi...
leo anamshukuru Mungu kwa maamuzi yanayosababisha mdogo wake kumaliza form four mwezi ujao.[/QUO
Umenena vyema mkuu;hawa watu sio wazalendo kabisa.Rais kafanya mengi mazuri ya kumshukuru kwayo
 
Mwenye dhamira njema hawezi kuwa mwizi, fisadi, muongo na muuaji.

Huyu Ndiye Pombe Magufuli:

- Wasema nyumba 8,000 kauza kwa mkono wake mwenyewe
- Apuuza maonyo ya wataalamu- Mafaili ya Sundi na Musa aliyabeba kwapani

ALIYEKUWA Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, katika Serikali ya awamu ya tatu, aliteka madaraka na kuwa mwenyekiti wa zoezi la kuuza nyumba za serikali ambazo hadi sasa, zimeshauzwa 8,288 imefahamika.

Habari zilizopatikana ndani ya wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), zimethibitishia Rai wiki hii kwamba Magufuli alihakikisha anashiriki kama Mwenyekiti katika zoezi zima la kuuza nyumba, ambalo kimsingi lilistahili kusimamiwa na Mtendaji Mkuu wa TBA.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari ndani ya TBA, Magufuli alifanya kila aina ya ‘fujo’ katika zoezi la kuuza nyumba hizo, wakati mwingine akibatilisha maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya TBA ya kuuza nyumba hizo, akiwapangia watu nyumba kwa utashi wake na wakati mwingine akiwakemea wale wote waliomshauri kinyume na matakwa.

Ni chini ya utaratibu huo, habari zinaeleza kwamba Magufuli, aliyabeba yeye mwenyewe mafaili ya ndugu zake; Musa Magufuli ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo ambaye ni mzazi mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao.

Habari hizo zinaeleza kwamba awali Mtendaji Mkuu wa TBA alimshauri Magufuli kwamba suala la mauzo ya nyumba kwa ndugu zake ni kinyume cha utaratibu. Hata hivyo, imeelezwa kwamba Magufuli alilazimisha huku akisema mdogo wake hana tatizo kwa sababu alikuwa tayari mfanyakazi wa Serikali.

Musa aliajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu, baada ya mwezi mmoja akauziwa nyumba na baada ya miezi miwili akaacha kazi.

“Kwa upande wa Sundi, kwanza ilikuwa Sundi auziwe nyumba moja kwa moja. Lakini Magufuli alipoonywa akashtuka na kusema suala hilo aachiwe yeye mwenyewe. Na ndipo akaibuka na jina la Stanley Manongi kwamba ndiye mnunuzi halisi na baba yake Sundi,” vinasema vyanzo hivyo vya habari, vingine ambavyo vilishiriki moja kwa moja katika mchakato wa uuzaji nyumba hizo.

Habari hizo zinaendelea kueleza kwamba baadaye, Sundi alishtuka akitilia shaka uaminifu wa Manongi, kwamba angeweza kumdhulumu nyumba hiyo.

“Ndipo Magufuli aliibuka na mpango wa Sundi kuwa mtoto wa Manongi na mrithi wake na kisha kwa kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote, mtoto wa Sundi naye akarithishwa na kama mrithi wa pili,” chanzo hicho cha habari kinaeleza.

Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa Serikali.

Sheria hiyo inaipa mamlaka ya kipekee ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.

Chini ya sheria hiyo, Waziri anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

Hadi Machi mwaka huu, wajumbe hao walikuwa ni J. Kijazi, E. Lipambila, E. Lugwisha, Msangi, E. Mwakalinga, D. Kisasi, P. Ncheye, F. Werema na A. Bukuku.

Hata hivyo, sheria haitoi nafasi yoyote kwa Waziri kusimamia shughuli za uuzwaji au upangaji wa nyumba za serikali.

Mtendaji Mkuu wa TBA Togolayi Makumba Kimweri, alipoulizwa kupitia kwa Katibu Muhtasi wake, alimwambia mwandishi wa Rai aandike maswali kisha asubiri kuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi.

Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa muda wa saa moja, mwandishi alipokwenda kuuliza akaambiwa kwamba Kimweri tayari alikwishaondoka ofisini kupitia mlango wa nyuma na asingeweza kurudi ofisini.

Lakini baadhi ya wafanyakazi wa TBA wameiambia Rai kwamba kinachoandikwa kwenye magazeti kuhusu ushiriki wa Magufuli kuuza nyumba za Serikali ni kidogo mno kuliko hali halisi.

Kama ilivyokuwa kwa mdogo wake Musa, waziri Magufuli alishinikiza mtoto wa dada yake anayeitwa James Doto Mgosha auziwe nyumba za serikali kwa kumtengenezea ajira ya muda mfupi katika TANROADS.

Tofauti na Musa, Doto ameuziwa nyumba hiyo kwa jina la mtu mwingine lakini anaishi katika nyumba hiyo, namba 64 iliyopo Kinondoni Flats.

Habari kutoka TBA zinaonyesha jina la mtu mwingine (tunalihifadhi) kuwa ndiye aliyeuziwa nyumba hiyo mtu huyo alipata kupitia utaratibu wa Magufulikupeleka jina lake kwenye wakala wa majengo na kulazimisha apewe nyumba.

Alipoulizwa kwa njia ya simu, Doto alisema suala la ajira na nyumba waulizwe waliomwajiri na kumpa nyumba. Akakata simu.

Mfanyakazi mwingine alieleza Rai kwamba msichana mwingine (jina tunalihifadhi) akiwa na miezi minne tu kazini alipelekwa na Magufulikatika Wakala wa Majengo akilazimisha auziwe nyumba hata kabla ya kuthibitishwa kazini. Nyumba hiyo iko Block A, Ocean Road.

Hata hivyo, habari hizo zinaeleza kwamba msichana huyo ambaye hadi sasa anaishi na wazazi wake, ameipangisha nyumba hiyo kwa mfanyakazi mmoja wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na analipwa kwa dola za kimarekani.

“Kuuza nyumba za serikali sawa, lakini kweli katika mtindo huu? Sisi tunaoshiriki kuzikagua na kuziratibu tukiomba hatupati, lakini wengine wanaingia serikalini miezi miwili wanapata nyumba. Na wengine hata si wafanyakazi, wanapata, hii si sahihi, alilalamika mfanyakazi mmoja aliyeandikia Rai kwa njia ya barua pepe.

Hadi Machi mwaka huu Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) walishauza nyumba 8,288 ambazo hata hivyo zilitakiwa kuuzwa kwa watumishi wa serikali.

Katika mauzo hayo, Serikali ilitarajia kupata jumla ya shilingi 60,016,556,439.00. Hata hivyo hadi sasa Serikali imepata shilingi 22,684,108,115.08.

Kwa sasa, Serikali imebakiwa na nyumba 1,098 zinazosimamiwa na TBA. Kati ya hizo, nyumba 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa Serikali, nyumba 675 kama tied quarters, nyumba 111 zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40 zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama ofisi na nyingine 29 ni kama karakana na bohari.

SALVA RWEYEMAMU
RAI
 
Mabutu Sseseko alijenga uwanja wa ndege mkubwa kijijini kwao Cheto..ooh sorry Kijijini kwao Lisala ila sasa hivi ile runway ya uwanja wanakijiji wanaanikia udaga
uwanja wa ndege unaweza jengwa popote,kama ambavyo kuna mikoa ina reli na mingine hakuna.Kujengwa chato isiwe nongwa,kwani watu wa chato hawalipi kodi? hakuna utalii unaoweza fanyika huko? hata utamaduni nao ni utalii,,wazungu wanaweza fika Chato na kujifunza utamaduni wa native people.
 
basi sawa sukari ilikuwa kilo 5000 sasa imeshuka.. kwa maelezo yako najua ndio walewale Ma Dac wapya
 
Ndugu zangu watanzania nimekuwa nikisikia kelele nyingi kwenye vyombo vya habari kutoka vyama vya upinzani.
Nipende kutumia fursa hii kuwakumbusha watanzania wenzangu kuwa haya mema tunayo yaona katika serikali ya awamu ya tano ni matokeo ya dhamira safi ya rais wa awamu ya tano.Rais anatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kwa vitendo na ilani hii imeainisha kabisa kipi kinatakiwa kifanyike lini,wapi na kivipi.

Rais huyu amekuwa tofauti na marais walomtangulia,kafanya mengi mema tena makubwa.Kama vile:
  1. Elimu bure
  2. Nidhamu ya watumishi
  3. Kudhibiti rushwa na kuanzisha mahakama ya mafisadi
  4. Kulinda madini yetu na kuleta miswada mipya yenye lengo la kuleta maendeleo
  5. Ndege mpya
  6. Reli ya kisasa
  7. Upatikanaji wa madawa hospitalini
Huko nyuma upinzani ulikuwepo,jiulize kwa nini matokeo makubwa chanya tumeyaona katika awamu hii? Hapo ndipo ninapojenga hoja yangu kuwa Mema yote unayo yaona sasa katika awamu ya tano ni matokeo ya udhubutu,uzalendo na dhamira ya njema ya Rais wa awamu ya tano.

Niwakumbushe tu wapinzani kuwa ifike mahali wamuunge mkono Rais katika yale yalokuwa mema;watafute namna nzuri ya kutoa ushauri.Kupinga kila kitu sio njia nzuri ya kujenga nchi bali ni namna ya kutafuta umaarufu tu.Watanzania wanahitaji maendeleo sio siasa.
Umewasikia takukuru wanavyobweka?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom