Mema ya awamu ya tano ni matokeo ya dhamira njema ya Rais na sio kelele za upinzani

uwanja wa ndege unaweza jengwa popote,kama ambavyo kuna mikoa ina reli na mingine hakuna.Kujengwa chato isiwe nongwa,kwani watu wa chato hawalipi kodi? hakuna utalii unaoweza fanyika huko? hata utamaduni nao ni utalii,,wazungu wanaweza fika Chato na kujifunza utamaduni wa native people.
Naa kweli wakienda kujifunza viubongo vya watu wale inaweza kutuingizia kipato.
Punda wanawekewa trafikilaaaiti!!

Lazima utalii ukue teh teh teh teh
 
Mwenye dhamira njema hawezi kuwa mwizi, fisadi, muongo na muuaji.

Huyu Ndiye Pombe Magufuli:

- Wasema nyumba 8,000 kauza kwa mkono wake mwenyewe
- Apuuza maonyo ya wataalamu- Mafaili ya Sundi na Musa aliyabeba kwapani

ALIYEKUWA Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, katika Serikali ya awamu ya tatu, aliteka madaraka na kuwa mwenyekiti wa zoezi la kuuza nyumba za serikali ambazo hadi sasa, zimeshauzwa 8,288 imefahamika.

Habari zilizopatikana ndani ya wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), zimethibitishia Rai wiki hii kwamba Magufuli alihakikisha anashiriki kama Mwenyekiti katika zoezi zima la kuuza nyumba, ambalo kimsingi lilistahili kusimamiwa na Mtendaji Mkuu wa TBA.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari ndani ya TBA, Magufuli alifanya kila aina ya ‘fujo’ katika zoezi la kuuza nyumba hizo, wakati mwingine akibatilisha maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya TBA ya kuuza nyumba hizo, akiwapangia watu nyumba kwa utashi wake na wakati mwingine akiwakemea wale wote waliomshauri kinyume na matakwa.

Ni chini ya utaratibu huo, habari zinaeleza kwamba Magufuli, aliyabeba yeye mwenyewe mafaili ya ndugu zake; Musa Magufuli ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo ambaye ni mzazi mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao.

Habari hizo zinaeleza kwamba awali Mtendaji Mkuu wa TBA alimshauri Magufuli kwamba suala la mauzo ya nyumba kwa ndugu zake ni kinyume cha utaratibu. Hata hivyo, imeelezwa kwamba Magufuli alilazimisha huku akisema mdogo wake hana tatizo kwa sababu alikuwa tayari mfanyakazi wa Serikali.

Musa aliajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu, baada ya mwezi mmoja akauziwa nyumba na baada ya miezi miwili akaacha kazi.

“Kwa upande wa Sundi, kwanza ilikuwa Sundi auziwe nyumba moja kwa moja. Lakini Magufuli alipoonywa akashtuka na kusema suala hilo aachiwe yeye mwenyewe. Na ndipo akaibuka na jina la Stanley Manongi kwamba ndiye mnunuzi halisi na baba yake Sundi,” vinasema vyanzo hivyo vya habari, vingine ambavyo vilishiriki moja kwa moja katika mchakato wa uuzaji nyumba hizo.

Habari hizo zinaendelea kueleza kwamba baadaye, Sundi alishtuka akitilia shaka uaminifu wa Manongi, kwamba angeweza kumdhulumu nyumba hiyo.

“Ndipo Magufuli aliibuka na mpango wa Sundi kuwa mtoto wa Manongi na mrithi wake na kisha kwa kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote, mtoto wa Sundi naye akarithishwa na kama mrithi wa pili,” chanzo hicho cha habari kinaeleza.

Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa Serikali.

Sheria hiyo inaipa mamlaka ya kipekee ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.

Chini ya sheria hiyo, Waziri anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

Hadi Machi mwaka huu, wajumbe hao walikuwa ni J. Kijazi, E. Lipambila, E. Lugwisha, Msangi, E. Mwakalinga, D. Kisasi, P. Ncheye, F. Werema na A. Bukuku.

Hata hivyo, sheria haitoi nafasi yoyote kwa Waziri kusimamia shughuli za uuzwaji au upangaji wa nyumba za serikali.

Mtendaji Mkuu wa TBA Togolayi Makumba Kimweri, alipoulizwa kupitia kwa Katibu Muhtasi wake, alimwambia mwandishi wa Rai aandike maswali kisha asubiri kuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi.

Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa muda wa saa moja, mwandishi alipokwenda kuuliza akaambiwa kwamba Kimweri tayari alikwishaondoka ofisini kupitia mlango wa nyuma na asingeweza kurudi ofisini.

Lakini baadhi ya wafanyakazi wa TBA wameiambia Rai kwamba kinachoandikwa kwenye magazeti kuhusu ushiriki wa Magufuli kuuza nyumba za Serikali ni kidogo mno kuliko hali halisi.

Kama ilivyokuwa kwa mdogo wake Musa, waziri Magufuli alishinikiza mtoto wa dada yake anayeitwa James Doto Mgosha auziwe nyumba za serikali kwa kumtengenezea ajira ya muda mfupi katika TANROADS.

Tofauti na Musa, Doto ameuziwa nyumba hiyo kwa jina la mtu mwingine lakini anaishi katika nyumba hiyo, namba 64 iliyopo Kinondoni Flats.

Habari kutoka TBA zinaonyesha jina la mtu mwingine (tunalihifadhi) kuwa ndiye aliyeuziwa nyumba hiyo mtu huyo alipata kupitia utaratibu wa Magufulikupeleka jina lake kwenye wakala wa majengo na kulazimisha apewe nyumba.

Alipoulizwa kwa njia ya simu, Doto alisema suala la ajira na nyumba waulizwe waliomwajiri na kumpa nyumba. Akakata simu.

Mfanyakazi mwingine alieleza Rai kwamba msichana mwingine (jina tunalihifadhi) akiwa na miezi minne tu kazini alipelekwa na Magufulikatika Wakala wa Majengo akilazimisha auziwe nyumba hata kabla ya kuthibitishwa kazini. Nyumba hiyo iko Block A, Ocean Road.

Hata hivyo, habari hizo zinaeleza kwamba msichana huyo ambaye hadi sasa anaishi na wazazi wake, ameipangisha nyumba hiyo kwa mfanyakazi mmoja wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na analipwa kwa dola za kimarekani.

“Kuuza nyumba za serikali sawa, lakini kweli katika mtindo huu? Sisi tunaoshiriki kuzikagua na kuziratibu tukiomba hatupati, lakini wengine wanaingia serikalini miezi miwili wanapata nyumba. Na wengine hata si wafanyakazi, wanapata, hii si sahihi, alilalamika mfanyakazi mmoja aliyeandikia Rai kwa njia ya barua pepe.

Hadi Machi mwaka huu Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) walishauza nyumba 8,288 ambazo hata hivyo zilitakiwa kuuzwa kwa watumishi wa serikali.

Katika mauzo hayo, Serikali ilitarajia kupata jumla ya shilingi 60,016,556,439.00. Hata hivyo hadi sasa Serikali imepata shilingi 22,684,108,115.08.

Kwa sasa, Serikali imebakiwa na nyumba 1,098 zinazosimamiwa na TBA. Kati ya hizo, nyumba 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa Serikali, nyumba 675 kama tied quarters, nyumba 111 zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40 zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama ofisi na nyingine 29 ni kama karakana na bohari.

SALVA RWEYEMAMU
RAI
Umeandika hoja ndefu lakini shida ni kuwa hizi ni opinions,siwezi pingana na wewe moja kwa moja lakini pia siwezi amini hoja yako moja kwa moja.Mi naamini kuwa kama kuna mtu ana tatizo na uuzwaji wa hizi nyumba angeenda kwa court.Kama meya wa ubungo alivyo enda kwa issue ya Bashite,,Hii issue ni ya kitambo sana hata kabla ya uchaguzi wa 2015.Kuendelea kumtuhumu mtu kwa opinions tu sio sawa rafiki.
 
Naa kweli wakienda kujifunza viubongo vya watu wale inaweza kutuingizia kipato.
Punda wanawekewa trafikilaaaiti!!

Lazima utalii ukue teh teh teh teh
Hayo matusi sasa,kwa hiyo chato wanaishi punda tu?
 
Mtoa mada uko kama NKAMIA,hamjui wananchi wanavyoteswa kwa
1)-Kuvunjiwa nyumba zao.
2)-Kukomeshwa kwa kutoza faini barabarani
3)-Kuongezwa kwa viwango vya faini na gharama za kulipia viwanja
4)-Kunyang'anywa viwanja kwa madai ya kutoendeleza wakati ela zimezidi kuwa hazionekani.
5)-Wanchi wamezidi kupata magonjwa ya moyo kwa kutojua hatima za kesho zao,kila siku jambo jipya la kudumaza vipato vyao.
5)-Matamko ya viongozi yasiyotia FARAJA badala yake chuki na HASIRA.
MEMA YEPI BANA ACHA NJAA NDUGU.
 
ukweli utatuweka huru,lugha za kutiana moyo penye hakuna hazina nafasi tena.Narudia ''KATA'',na ''ASIEFANYA KAZI ASILE''
 
ukweli utatuweka huru,lugha za kutiana moyo penye hakuna hazina nafasi tena.Narudia ''KATA'',na ''ASIEFANYA KAZI ASILE''
Lugha ya kuwa BOMBERDIER imekamatwa ilikuwa na ukweli kutoka kwa LISSU,mbona hamkukubali wakati inapigwa kutu hapo MONTREAL mpaka leo,na waliosema kweli mumewaita "si wazalendo"wakati nyie munaficha.
 
Hakuna alichofanya mimi sijaona,, yote ni mikakati ya awali
Mikakati inaweza kuwepo lakini nani wa kumfunga paka kengele? hicho tulikuwa tunakosa.Nadhani japo huwezi ona mengi lakini hata hili la elimu bure basi ulitazame kwa jicho la kizalendo
 
Eti ni opinion! Pumbaff! Mwizi ni mwizi tu fisadi na fisadi ni tu. CAG haandiki opinions anachunguza kwa kina kisha kuandika ripoti yake.

Usituletee ujinga wako wa lumumba humu eti hizi ni opinions. Mwizi aliyeiba leo ni mwizi na aliyeiba miaka 15 iliyopita naye ni mwizi. Yote haya kuhusu wizi wa huyo dikteta uchwara yamo kwenye ripoti za CAG.

Umeandika hoja ndefu lakini shida ni kuwa hizi ni opinions,siwezi pingana na wewe moja kwa moja lakini pia siwezi amini hoja yako moja kwa moja.Mi naamini kuwa kama kuna mtu ana tatizo na uuzwaji wa hizi nyumba angeenda kwa court.Kama meya wa ubungo alivyo enda kwa issue ya Bashite,,Hii issue ni ya kitambo sana hata kabla ya uchaguzi wa 2015.Kuendelea kumtuhumu mtu kwa opinions tu sio sawa rafiki.
 
Lugha ya kuwa BOMBERDIER imekamatwa ilikuwa na ukweli kutoka kwa LISSU,mbona hamkukubali wakati inapigwa kutu hapo MONTREAL mpaka leo,na waliosema kweli mumewaita "si wazalendo"wakati nyie munaficha.
Unaweza kuwa ukweli lakini namna ya kuuleta,,usitumie madhaifu serikali kutaka umaarufu.That is where the issue arises
 
Eti ni opinion! Pumbaff! Mwizi ni mwizi tu fisadi na fisadi ni tu. CAG haandiki opinions anachunguza kwa kina kisha kuandika ripoti yake.

Usituletee ujinga wako wa lumumba humu eti hizi ni opinions. Mwizi aliyeiba leo ni mwizi na aliyeiba miaka 15 iliyopita naye ni mwizi. Yote haya kuhusu wizi wa huyo dikteta uchwara yamo kwenye ripoti za CAG.
At last umeandika hiyo ripoti kaandika nani? CAG au gazeti la RAI? poor you.
 
Ukweli ungekuwa unaujua usingeandika huu upuuzi kuhusu huyo fisadi Mkuu.
We mahakama? ndio tatizo lenu CDM ,mnajifanya wajuvi wa kila kitu.Unaanzaje kumuita mtu fisadi wakati mahakama ndio ina haki hiyo?
 
Back
Top Bottom