Meli zetu hazifai kubeba abiria, ni vyuma chakavu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Meli zetu hazifai kubeba abiria, ni vyuma chakavu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Michael Amon, Jul 24, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Jul 24, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,670
  Likes Received: 607
  Trophy Points: 280
  TANZANIA sasa imekuwa nchi ya misiba na tunadiriki kusema kwamba mara nyingi misiba hiyo imekuwa ya kujitakia. Haipiti siku kabla vyombo vya habari havijatangaza habari za vifo vya mamia ya watu vinavyotokana na ajali barabarani katika kila kona ya nchi yetu. Ajali za vyombo vya majini, kama ilivyo kwa vyombo vya safari za anga na reli zimezidi kuongezeka na kujenga dhana miongoni mwa wananchi kuwa, siyo tu ajali zimekuwa sehemu ya utamaduni wetu, bali pia kwamba ajali hizo kamwe haziepukiki.

  Tumeshindwa kupata muarobaini wa kupunguza, kama siyo kukomesha ajali hizo zinazopoteza maisha ya Watanzania. Badala ya kufanya uamuzi mgumu wa kuchukua hatua stahiki dhidi ya vyanzo vya ajali hizo na kusimamia sheria za usafirishaji kwa kuhakikisha sheria hizo zinauma kila upande pasipo woga wala upendeleo, viongozi wetu wamebaki kuwa vinara wa kutoa rambirambi kwa wafiwa. Tunathubutu kusema kwamba vifo vingi vinavyotokana na ajali hizo vimetokea kwa sababu Serikali imeshindwa kutimiza wajibu wake.

  Juzi mchana utamaduni huo wa ajali ulijirudia baada ya miili ya abiria wapatao 50 kuopolewa wakiwa wamefariki dunia na wengine 137 kuokolewa wakiwa majeruhi baada ya meli ya Skagit iliyokuwa imebeba abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar kuzama karibu na Kisiwa cha Chumbe, kilomita 19 kutoka Bandari ya Malindi, mjini Zanzibar. Hata hivyo, kumekuwapo na mkanganyiko kuhusu idadi kamili ya watu waliokuwa katika meli hiyo, kwani jana mamlaka husika zilikuwa zikitoa kauli zilizokuwa zinatofautiana au zinakinzana.

  Hii ni ajali ya pili mbaya kutokea visiwani humo katika kipindi cha miezi 10 tu tangu ilipotokea ajali nyingine ya MV Spice Islander Septemba 2011 ambapo watu wapatao 240 walikufa na wengine zaidi ya 1,500 hawajulikani walipo hadi leo baada ya meli hiyo kuzama ikiwa safarini kuelekea Pemba ikitokea Bandari ya Malindi, Unguja na tume iliyoundwa na Rais Mohamed Shein kuchunguza ajali hiyo ilitoa ripoti iliyosema kuwa, meli hiyo ilikuwa imebeba mizigo na abiria kuliko uwezo wake.

  Hata hivyo, siyo mara ya kwanza kwa meli hiyo iliyozama juzi kukumbwa na misukosuko ikiwa imebeba abiria baharini. Mei mwaka huu, abiria wapatao 300 walinusurika kufa baada ya meli hiyo kushika moto katika eneo la Nungwi ulioanzia kwenye injini wakati ikielekea Unguja kutoka Pemba. Zipo taarifa kutoka shirika moja la kimataifa kuwa, meli hiyo ilinunuliwa mwaka 2011 kutoka Marekani, lakini wataalamu walionya mwaka 2006 kwamba meli hiyo ilikuwa haifai tena kubeba abiria.

  Jambo moja linalojitokeza hapa ni kwamba meli zinazosafirisha abiria katika maziwa na bahari zetu siyo salama na hazifai tena kwa sababu zimechakaa, hivyo kustahili tu kuuzwa kama vyuma chakavu. Inashangaza kuona serikali zetu katika pande zote mbili za Muungano hazithamini maisha na ustawi wa watu wake na hazioni umuhimu wa kununua meli zilizo salama kwa ajili ya usafiri wa wananchi.

  Hili linathibitishwa na ukweli kwamba MV Liemba iliyozama katika Ziwa Tanganyika miaka michache baada ya Uhuru halijapata meli nyingine hadi leo. Kama hiyo haitoshi, MV Bukoba iliyozama katika Ziwa Victoria mwaka 1996 na kuua watu 1,000 haijapata mbadala wake hadi leo, huku MV Victoria iliyoanza kutumika katika ziwa hilo tangu miaka ya 60 ikisubiriwa kuzama na kuua maelfu ya abiria wakati wowote kutokana na kuzeeka kupita kiasi. Ni jambo la ajabu kwamba Ziwa Nyasa limekosa meli kwa miongo mingi sasa na kuacha wananchi wakiweka maisha yao rehani kwa kutumia usafiri usio salama.

  Tunazishauri serikali zote mbili zitambue kwamba majuto ni mjukuu, kwa maana ya kuhakikisha kwamba vyombo vya usafiri vinakuwa salama badala ya kusubiri kutokea kwa ajali na kuwa wepesi wa kutoa rambirambi na hata kuamuru bendera zote nchini zipeperushwe nusu mlingoti.
   
 2. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,713
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  The silly government!
   
 3. paty

  paty JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,218
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Hii ni hatari ya sisi wenyewe kukubali kuwa dampo la vitu vya bei laisi vilivyokwisha thamani na vilivyo chini ya kiwango, ni hatari sana, ...ivi mamlaka husika huwa zinafanya kazi gani?

  Hizi tume zinazoundwa baada ya majanga huwa zinaishia wapi? Maana kila mwaka tatizo ni lile lile na wananchi wanazidi kupoteza maisha, inasikitisha sana, nadhani viongozi wanapaswa kuwajibika na wananchi tuache haraka zisizo kuwa na maana, kama usafiri ni hatarishi hakuna haja ya ku risk maisha yako
   
 4. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,447
  Likes Received: 606
  Trophy Points: 280
  ...na wengine zaidi ya 1,500 hawajulikani walipo!!!!!!
   
 5. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuna mambo maishani lazima uwe makini tu..hayataki ubabaishaji!..na miongoni mwao ni hili la 'Usafirishaji wa Abiria'..kiukweli usipokuwa makini hapa kila siku itakuwa Misiba tu!..Hakuna mbadala..tuache lipualipua..kama tunawatakia mema watu wetu tujitoe kikweli kikweli..bahati mbaya kwa nchi yangu Tanzania kila kitu hatuwezi..lol!
   
 6. bombu

  bombu JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,129
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Tatizo kubwa ni kuwa wamiliki wa vyombo vyenyewe ndo hao hao wanaoturushia rambirambi zao kupitia runingani, na kutuambia hizo ni ajali kama ajali zingine, eti ni ajali za kimaumbile. Inanishangaza sana kuona kuwa baada ya tukio moja mambo husahaulika na ratiba za ovyo ovyo huendelea, huku tukidhani kuwa hiyo ni bahati mbaya.

  Lol, tumebaki tukiziumiza keyboard zetu, ilhali mambo yanazidi kutuwia ugumu. Ingawa wakati mwingine jamani ajali twazisababisha sie abiria na mizigo yetu. Tu watu wabinafsi wenye kujijali, hakuna anayefumbua macho na kuutazama uhalisia wa mambo. Utakuta mtu yuko radhi asafiri akiwa amening'inia kwa madai kuwa ana haraka ya aendako.

  kweli tunatakiwa kufumbua macho na kuona thamani ya roho na nafsi zetu. Tujithaminishe kabla hatujapangwa pamoja na mizigo yetu. Ni kawaida kwa vyombo vyetu vya usafiri kujaza kupita ukomo wake, na hili ni tatizo kubwa kuliko yote.
   
 7. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,154
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  Wanasubiri kuunda tume watu wale pesa za kufanya kazi za tume na mapendekezo yake nayo yatawekwa kama yalivyowekwa yale ya Mv Spice maana Tanzania kwa tume hatuna mshindani na zote report zake hazifanyiwi kazi
  Tumebaki tunasema ajali haina kinga wakati tunaona kwa macho yetu kuwa hivi vyombo ni vichakavu havifai hata kubeba abiria kwa namna yoyote
   
 8. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,670
  Likes Received: 607
  Trophy Points: 280
  Usemayo ni kweli kabisa mkuu...Hakuna kinachoshindikana katika hii dunia na waswahili husema kinga ni bora kuliko tiba. Kwa mtazamo wangu nadhani kinga ya kwanza ya ajali kama hizi za uzembe ingepaswa kuwekwa na serikali kwa kuhakikisha kuwa vyombo vya majini vinavyoingia nchini kwetu ni mpya na zenye viwango vinavyokubalika kimataifa na sio kuruhusu nchi yetu kugeuzwa kama dampo la vyuma chakavu na machinjio ya watu

  Siwalaumu sana watanzania kwa kupanda usafiri huo kwa sababu kwanza kabisa usafiri wa majini ni usafiri wa gharama nafuu ambao hutumika na watu wengi hasa wa kipato cha chini...Ni watanzania wachache wenye uwezo wa kusafiri kwa ndege. Kama wakisema wasipande hizo meli kwa sababu zimechakaa unadhani watasafiri kwa njia gani wakati huo usafiri wa meli ndio wanaoutegemea ndio ambao pia wana uwezo wa kuumudu?
   
 9. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,154
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280

  Mkuu Young_Master nchi ya kitu kidogo kila kitu kinawezekana
  Kuanzia waziri mpaka mtu wa chini pale TRA anayetoa mzigo bandarini wanajua uhalisia wa vyombo vyetu ndani ya bahari
  Wanajua hiki chombo ni cha mwaka gani na kilipaswa kuwa wapi wakati huo
  Hakuna kwenye uafadhali sio kwenye ndege wala sio meli au vyombo vvya usafiri majini wala sio barabarani
  Na hii ni kutokana na kuwa na watu wasiojali wanapitisha na kukubali vyombo hivyo vitumike kuwasafirisha watu
  Angalia mabasi yanavyoua watu yakipata ajali kwa kuwa bodi zake ni kama karatasi hivyo likipata ajali ni kuwa bodi inakatika na kuhama kabisa
  Angalia vinoah vilivyoruhusiwa kubeba abiria ambavyo hata mbuzi akilitwanga bodi lake kwa pembe zake kisawa sawa analitoboa ila vimejaa barabarani kubeba abiria
  Kwa hapa Arusha kwa sasa angalia barabara ya Namanga wamezitoa zile 504 zilizokuwepo vinoah kwa sasa ndo vimejaa
  Angalia karatu na Babat kwa sasa
  Mkuu kila mahali ni pabaya hakuna kwenye usalama kabisa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #10
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,670
  Likes Received: 607
  Trophy Points: 280
  Usemayo ni kweli kabisa mkuu na hayo maeneo yote uliyoyataja nayafahamu na ni kweli yanaongoza kwa huo usafiri mbomvu wa vinoah na watu wanautumia sana huo usafiri wa noah kwa sababu ndio ndio usafiri wa haraka ukilinganisha na mabasi. Lakini nani alaumiwe kama sio serikali?
   
 11. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  sio tu kwamba hizi meli/boti hazistahili kuwepo majini kwa sababu ya ubovu wake bali pia zinakuaga over loaded..unakuta meli yenye uwezo wa kupakia abiria 200 unakuta zingine zina mpaka watu 350 hao wengine wanawekwa kihuni huni kwa hiyo sasa unakuta meli ikija kuzama wakicheki kwenye rekodi wanapewa idadi na information za watu ambao sio zote ni sahihi..kuna wengine nina uhakika wamekufa na wako majini mpaka sasa ambao hawakurekodiwa kwenye system...hilo ni tatizo la kiuongozi na serikali inabidi iwe makini kusimamia haya mashirika/kampunia husika
   
 12. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,154
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  So mkuu Young_Master sio kwamba wahusika hawaoni kinachoendelea
  Wanaona na wanajua kuwa vyombo fulani havifai kusafirisha abiria au vinabeba abiria kupita uwezo wake
  Ila nani wa kukemea iwapo kuanzia msimamizi, meneja, mkata ticket lao moja kuwa wanataka faida
  MV Bukoba, Mv Spice na hata hii iliyozama inasemekana ni kubeba abiria na mizigo kupita uwezo wake na ubovu mwingine ambao unajulikana kwa wote
  Ila nani amfunge paka kengele kusema kuwa umezidisha abiria washushe au hiki chombo hakiruhusiwi kuondoka bandarini kwa kuwa kimejaa kupita kiasi
  Kuanzia msimamizi hapo na wahusika wote washakunja chao mfukoni hawana haja nyie abiria mtajua wenyewe mkifika au msifike shauri yenu
  Mabasi yanaondoka stendi yanajulikana kabisa ni mabovu may be tyres zimeisha kabisa au kuna sehem imefungwa fungwa na kamba au mpira kwenye engine linaachiliwa na kubeba roho za watu hakuna anayejali abiria jiombee mwenyewe ufike salama na Mungu anajua kuwa nyie mnasafiri so ni lazima awafikishe salama
  Trafic wanaona na wanajua kabisa chombo ni kibovu ila kwa kuwa nae kashakunjiwa wala haoni
  Madereva wanaovertake maeneo hatari yenye milima na kona za hatari traffic wapo wala hawajali wao wakikusimamisha wakunjie 5000 yao wakati mnasalimiana basi nenda mheshimiwa safari njema kabisa
  lori limetoka mnadani limejaza mizigo na juu kabisa ya hiyo mizigo wanakalishwa akina mama ambao gari likiyumba tuu kidogo hawawezi hata kujitetea
  Wakikutana na polisi we jua tuu kukunja mkono wala kosa halitaonekana( sawa ni shida ya usafiri huko wanakotoka ila je usalama wa hao wasafiri uko wapi)
  likianguka na kuua hizo ni kudra za mwenyezi Mungu ajali haina kinga
  Tufike mahali tuseme basi na hizi ajali hao waliopewa dhamana waone kuwa maisha ya watu yanayopotea yana thamani kama yao ambao wanapanda V8 na VX na kupita nazo mtaani kwa mbwembwe
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,968
  Likes Received: 156
  Trophy Points: 160
  Wamekufa.
   
 14. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #14
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,670
  Likes Received: 607
  Trophy Points: 280
  Probably
   
 15. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 11,778
  Likes Received: 1,195
  Trophy Points: 280
  Nkicheki miaka ya MV Victoria, hata sipati hamu ya kupanda vyombo hivi vya kitz, practically primitive, we meli ya miaka ya 60, itakuwa na nini la kuifanya iendane na mazingira ya sasa?
   
 16. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #16
  Jul 26, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,670
  Likes Received: 607
  Trophy Points: 280
  nadhani hilo swali ingekuwa ni bora kama wangeulizwa hao waheshimiwa wanaopiga meza za bungeni kila siku halafu hatuoni wanachofanya zaidi ya kuangamiza maisha ya wananchi kwa uzembe wao kila kukicha.
   
Loading...