Meli yazama bahari ya Hindi, watamo wapotea

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,162
Meli moja ambayo bado haijatajwa na vyombo rasmi, imezama Jumamozi iliyopita wakati ikiwa njiani kutoka Dar es Salaam kuelekea Mafia. Abiria na wafanyakazi waliokuwemo kwenye meli hiyo inaelezwa kuwa ni 14 na hadi hivi sasa watu wanane wamepatikana wakia hao huko maeneo ya Makunduchi, Zanzibar.

Mwili wa mtu mmoja, anayeaminika kuwa ndiye alikuwa nahodha wa meli hiyo, umepatikana na kufanya watu watatu wasijulikane walipo. Watu hao wanahusisha askari magereza mmoja ambaye alikuwa anayasindikiza magari matatu ya Magereza yaliyokuwa yanasafirishwa na meli hiyo.

Pamoja na magari hayo, meli hiyo ilibeba pia shehena ya mafuta ya Tanesco yaliyokuwa yanapelekwa Mafia.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, tayari ametuma salamu za rambirambi kwa wafiwa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom