Meli ya mizigo yazama Tanga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,377
58,384
kuna meli ya mizigo inaitwa Sarobo imezama Tanga asubuhi hii ya leo ilikuwa inatoka Tanga kwenda Pemba..mabaharia saba walikuwa ndani ya hiyo meli wamepatikana salama.. Kama kuna mtu mwenye more details kuhusu hili tukio tupeane updates...

Sina hakika na hilo jina la meli/boti may be nimekosea spellings tutawiana radhi

source:JF

My take: Kama viongozi wetu wangekuwa wastaarabu wanegoa tamko la kuvikagua vyombo vyote vya majini na liseni zao..nashangaa hadi sasa hivi wapo kimya
 
Duu!
Ni aibu hadi kwa mataifa ya jirani!
Sumatra wana kazi gani hawa, au ni jina na ofisi tu!
Damu za Watz zitamezwa na bahari ya HiNDI HATA LINI JAMENI?
 
Thanks for update na tungoje kusikia chanzo cha ajali ni nini. Naamini kuna haja ya kufanya ukaguzi wa kina wa vyombo vya majini
 
Sasa naanza kuimkumbuka ile movie ya 2012.....majanga ya baharini na nchi kavu, na 2012 ndo inakaribia
 
Kweli huu mwaka nia wa SHETANI. Jana ajali zimeuwa Morogoro, Polisi kama kawaida yao wameuwa Geita, sasa tunaishi kiwasiwasi wasi tu maana kila kona majanga sijui tumekosa nini kwa nchi yetu hii maana huwezi kusema tumemkosea nini Mungu! Ewe JK na Serikali yako hizi roho za wasio na hatia zitawahukumu siku za mwisho!
 
Oh, hii imekaaje mkuu! Ina maana na ajali nazo zinasherehekea miaka 50!!?? ...au zimeamua kuonyesha ukweli wa mameno na gharama wanazodumbukiza kwenye kusherehekea huko!!?
tutaisha mwaka huu...hii miaka 50 ya uhuru tunatoana kafara tu...thanks for updates.
 
Kweli huu mwaka nia wa SHETANI. Jana ajali zimeuwa Morogoro, Polisi kama kawaida yao wameuwa Geita, sasa tunaishi kiwasiwasi wasi tu maana kila kona majanga sijui tumekosa nini kwa nchi yetu hii maana huwezi kusema tumemkosea nini Mungu! Ewe JK na Serikali yako hizi roho za wasio na hatia zitawahukumu siku za mwisho!

Hapo kwenye red Mkuu tumekosa viongozi wenye akili timamu.
 
Dah mbona inasikitisha hivi........majini na nchi kavu matatizo
Angani ndege zinashindwa kutua kisa umeme hakuna kila mahali matatizo!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom