Meli ya India yawasili Afrika Kusini na kile kirusi Baba lao

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,825
35,827
Mabibi na mabwana kutokea Afrika Kusini, kuna habari za meli kuwasili huko ikiwa na mzigo wa hatari na wa kutosha kutokea India:

IMG_20210505_085111_326.jpg



Huu umewasili kwenye meli. Tena bila shaka kabla ya kutoka India walipimwa dhidi ya kirusi hiki, mabaharia hawa.

Kwa hali hii kwenye madege kutakuwa je?

Kwa huu usafiri wa anga unaoendelea bado baina yetu na India, tusipoliita sasa koleo hili kwa jina lake, ipo hatari ya kuwa tunajipalia makaa kwa mikono yetu wenyewe.

Faida za mahusiano ya anga na India kwa sasa hailingani kabisa na hatari iliyo mbele.

Huu ndiyo ulio ukweli mchungu kweri kweri.
 
Covid 19 rafiki wa wabaguzi. Nchi haswa maskini zitatengwa sana sababu tu ya COVID
 
Covid 19 rafiki wa wabaguzi. Nchi haswa maskini zitatengwa sana sababu tu ya COVID

Atalaumiwa sana dobi. Kirusi cha India?

Eeh mola wetu ukipishilie mbali kama kimbunga Jobo.
 
Back
Top Bottom