Meli kubwa ya Jeshi la China yenye Hospitali inayotoa huduma za upimaji, upasuaji na kutibu magonjwa bure yawasili Dar

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Wadau habarini

Katika kuunga mkono jitihada za RC Makonda, jumla ya Madaktari Bingwa Na Wataalamu wa Afya 381 kutoka Jeshi la China watawasili nchini tarehe 20/11/2027 na kutoa huduma za matibabu bure ikiwemo upasuaji.

Wataalamu hao watakuja na Meli maalumu itakayotumika kutoa matibabu bure kwa wastani wa Wagonjwa 600 kwa Siku ikiwemo upasuaji.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaomba wakazi wa Jiji hilo pamoja na Mikoa ya jirani kuchangamkia fursa hiyo muhimu itakayodumu kwa muda wa siku saba kuanzia tarehe 20/11/2017.

Tutaendelea kuwapa mrejesho wa zoezi hilo.

Karibuni..
----

UPDATE >> 19 Novemba, 2017

Meli ya Hospitali kutoka China tayari imewasili katika Bandari ya Dar es Salaam leo ikiwa na madaktari bingwa na wafanyakazi 381 ambao watatoa huduma ya matibabu bure ndani ya meli hiyo kwa muda wa wiki moja kuanzia Jumatatu ya kesho (Novemba 20, 2017)..
 
Daaa.., wamuangalie sana huyu Jamaa asije ifanya DSM kama Jimbo la Catalonia, ana uwezo wa kuleta Madaktari toka Jeshi la China!!!
 
Taratbu naacha kumuita bashite, Makonda ananipa wakat mgumu sana mana nipo katkat na haitakiwi uwe vuguvugu, mana akikukera asubuh jion lazma atakufurahsha, huyu jamaa mi napenda uchapakaz wake sana, tatzo ni akianza show off za maneno ndo anaharibu. Yan asubuh unaita jina lile jion unaita hili.

By now,
i don't hate you, i don't love you. I like the work, i hate the acts.
Yote kwa yote tunahtaj maendeleo, Big up bro.
 
Wadau habarini.
Katika kuunga mkono jitihada za RC Makonda Jumla ya Madakari Bingwa Na Wataalamu wa Afya 381 kutoka Jeshi la China watawasili nchini tarehe 19/11/2027 na kutoa huduma za matibabu bure ikiwemo upasuaji.
Wataalamu hao watakuja na Meli maalumu itakayotumika kutoa matibabu bure kwa wastani wa Wagonjwa 600 kwa Siku ikiwemo upasuaji.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhesh Paulo Makonda amewaomba wakazi wa Jiji hilo pamoja na Mikoa ya jirani kuchangamkia fursa hiyo muhimu itakayodumu kwa muda wa siku saba kuanzia tarehe 19/11/2017

Tutaendelea kuwapa mrejesho wa zoezi hilo.
Karibuni

Akina shika?
 
Makonda atangaze huduma ya afya toka mamia ya madaktari wa kichina ndani meli maalum.

Wagonjwa watafanyiwa uchunguzi, upasuaji mdogo na mkubwa na kupewa daw na huduma itatolewa bure kwa kila mmoja.

Watatoa huduma kwa wagonjwa 600 kwa siku.

Wanainchi toka mikoani mtakaribishwa na utaratibu utatolewa wa kupata hiyo huduma kwa kila mmoja.
 
Makonda atangaze huduma ya afya toka mamia ya madaktari wa kichina ndani meli maalum.

Wagonjwa watafanyiwa uchunguzi, upasuaji mdogo na mkubwa na kupewa daw na huduma itatolewa bure kwa kila mmoja.

Watatoa huduma kwa wagonjwa 600 kwa siku.

Wanainchi toka mikoani mtakaribishwa na utaratibu utatolewa wa kupata hiyo huduma kwa kila mmoja.
May he. the Chinese doctors and all who made and will make this happen be BLESSED ABUNDANTLY
 
RC MAKONDA KUPOKEA MELI KUBWA YA JESHI LA CHINA YENYE HOSPITAL NDANI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA anataraji kupokea Meli kubwa ya kisasa kutoka Nchini China inayowasili Nchini November 19 kwaajili kutoa huduma za upimaji na Matibabu ya Magonjwa yote Bure kwa Wakazi wa Dar es Salaam kwa muda wa Siku Saba.

Meli hiyo kubwa ya aina yake ya Jeshi la Maji la China itawasili Bandari ya Dar es Salaam ikiwa na Madaktari Bingwa na Wataalamu wa Afya zaidi ya 380 ina uwezo wa kufanya upasuaji mkubwa na mdogo ndani ya meli kwa zaidi ya Watu 600 kwa siku.

RC MAKONDA amewatangazia wananchi kuchangamkia fursa hiyo ya huduma ya matibabu bila malipo kuanzia November 20 -25 ndani ya Meli.

MAKONDA amesema Meli hiyo itatoa matibabu kwa Magonjwa ya Figo, Saratani, Ini, Moyo, Macho, Sukari, Presha ambapo watakaopimwa na kugundulika kuwa na tatizo watapatiwa Dawa na matibabu Bure.

Aidha MAKONDA amesema huduma hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuokoa gharama za matibabu kwa Wananchi ikiwemo ile ya kusafirisha wagonjwa nje ya nchi kwakuwa ndani ya meli zitapatikana huduma zote ambazo hazipatikani kwenye hospital za Tanzania.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na aliekuwa Balozi wa China Nchini Tanzania aliyoitoa wakati wa Zoezi la upimaji wa Afya bure ambapo aliahidi kumuunga mkono RC MAKONDA katika kuboresha Sekta ya Afya.

Jambo jingine litakalifanywa na wataalamu hao ni kukarabati vifaa vyote vya hospital za Dar es salaam vitakavyokuwa na matatizo ikiwemo Ultrasound na Xray ili ziweze kufanyakazi upya ambapo pia madaktari hao watakuwa wakibadilishana uzoefu na utaalamu na madaktari wa Tanzania.

Mbali na hilo Madaktari hao watatembelea vituo vya kulelea watoto yatima kujionea namna serikali inahudumia watu Hawa wa kundi maalumu pamoja na siku ya moja ya kubadilishana utamaduni wa mavazi, vyakula na michezo.

RC MAKONDA amemwambia Mganga Mkuu wa Mkoa kuwaita Wagonjwa wote waliokuwa wamepangiwa kufanyiwa upasuaji tarehe za mbali kutokana na ufinyu wa huduma kupelekwa kufanyiwa huduma Bure.

Nae Kamanda wa Jeshi la Maji la China Meja Xing Song amesema zoezi hilo ni matunda ya ushiririkiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na China ambapo wamesema watazidi kushirikiana na
 
Back
Top Bottom