JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,458
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ameziagiza Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kuanza kutumia Bandari za nchi kavu zinazokidhi vigezo ili kupunguza msongamano wa magari bandarini.
Meli hiyo ‘Frontier Ace’ iliwasili jana Ijumaa Aprili 8, 2022 ikielezwa kuwa imewasili ikitokea Singapore kama kituo chake cha mwisho kabla ya kuwasili Dar baada ya safari ya siku 10.
Meli hiyo ilitengenezwa mwaka 2000 inatembea ikiwa na bendera ya Panama ina upana wa mita 33.2.
Baada ya kushusha mzigo Tanzania, inaelezwa kuwa magari 2,936 ni kwa ajili ya Nchi za DRC, Uganda, Zambia, Zimbabwe, Malawi na Afrika Kusini
Agosti 2021, bandari hiyo iliweka historia ya kupokea meli ya Tranquil Ace yenye urefu wa mita 199.95 na upana wa mita 32.2, ikiwa imebeba magari 3,743, ambapo asilimia 65 ya magari hayo ambayo ni 2,945 yalikuwa yakisafirishwa kwenye mataifa mengine wakati ni 798 yaliyobaki Tanzania.
Source: The Citizen