Melchizedek na utata unaomzunguka

Biblia haijataja kumuelezea sanaaa ndomaana akaingizwa ktk watu watatu ambao ndani ya biblia hawaonekani kua na wazazi.
Hapa una maanisha ya kuwa wazazi wao hawajulikani au hawakuwa na wazazi kinasaba kabisa ? Na kama ni kinasaba hili liliwezekana vipi ?
 
Habari za masiku wanajukwaa wote, leo ningependa tujadili watu mysterious kwenye vitabu vyetu vya dini kama ilivyo kawaida yetu. Hivyo twendeni pamoja ili tusolve mystery hii, kubwa ya yote tuongeze tu maarifa na kujibu maswali ambayo yameonekana magumu kwenye vitabu hivi.

Niweke rai mapema pamoja na kwamba inaongelea mtu wa kwenye imani zetu ila mada hii isijengwe kidini yaani kukashifiana bali ijikite kwenye mrengo wa kuelemishana. Karibuni

UTANGULIZI
Melchizidek anaongelewa kwa mara ya kwanza ndani ya Biblia kwenye kitabu cha mwanzo 14:18 ambapo baada ya Abraham kutokea vitani alikutana na Mfalme wa eneo la Salem (Jerusalem ya leo) ambapo alimbariki na Adam alimpa kikumi cha kila alichokuwa nacho wakati huo.

Kwahiyo kitabu cha mwanzo kinamueleza kama MFALME WA SALEM na kuhani wa Mungu YAHWEH

View attachment 1176929
AGANO JIPYA
Upande wa agano Jipya Melchizedek anaelezwa kuwa ana uhusiano ma Yesu.

Waebrania 5
6 kama asemavyo mahali pengine,Ndiwe kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki

Zaburi 110:4, Waebrania 5:10,6:20 zote zinaeleza kuwa Yesu ni kuhani kwa mfuatano na huyu melchizedek. Ikumbukwe Makuhani wengi wamepita hapo kati na Yesu ametokea kwenye uzao wa Abraham sasa iweje afananishwe na melchizedek na sio kuhani yeyote yule??

Je huyu melchizedek ni nani hasa?

UTATA ZAIDI
Utata zaidi unaibuka pale ambapo muandishi wa kitabu cha waebrania (ambaye mpaka leo hafahamiki ni nani) anaandika haya
Waebrania 7
3 hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.

Tunaambiwa huyu ''Jembe'' hakuwa na baba wala mama na anaishi milele hata sasa???

Ukisoma sura yote inamsifia mtu huyu wa ajabu (mysterious) na kusema licha ya ukuu wa Abraham kama Baba wa wayahudi ila haoni ndani kwa huyu Melchizedek!!

Book of Enoch
Muandishi wa kitabu hiki anajaribu kutupa mwanga kidogo kuhusu utata huu. Ukisoma Enoch 2 sura ya 71 inaeleza kuwa Kuhani Nir (Kaka yake Nuhu) alikuwa na mke ambaye hakulala naye toka alipoteuliwa na Mungu kuwa kuhani. Siku moja anagundua mke wake ana mimba, hivyo ukazuka ugomvi mkubwa mwishowe yule mama akapata presha akaanguka akafa, sasa cha ajabu walipotaka kuizika maiti haraka haraka ''kuua soo'' Wakashangaa mtoto ametoka tayari!!!. Yaani maiti imezaa!!!
Hivyo ikawa concluded kuwa kazaliwa bila baba wala mama.

Ikumbukwe alizaliwa kabla ya gharika, hivyo ili unabii utimie kuwa atakuwa kuhani wa makuhani wote ikabidi Malaika Gabriel amchukue na kumficha bustani ya Eden hivyo akapona gharika na akarudishwa baada ya gharika kupita.

HITIMISHO
Katika pekua pekua zangu sijakutana kabisa na maandiko yeyote kwenye biblia na pseudepigrapha (vilivyoachwa) ambacho kinagusia mwisho wake zaidi vyote vinasema anaishi milele ingawa havisemi wapi ama lini aliacha kuwa mfalme wa Salem.

Sasa wajuvi wa Historia na Dini mtusaidie je mtu huyu alikua nani hasa??

Pia kma alikuwa mkuu kuliko Abraham na amefananishwa na Yesu kwanini hajaongelewa sana kwenye Bible??

Je historia yake ni ipi??

Je mwisho wake ni upi hapa duniani? Au bado anaishi na sisi kwa sura tofauti?

Karibuni....

Hivi kumbe bado kuna watu wanaamini kwenye uwongo wa bibilia zile
 
Je hukuwahi kuuliza kwanini hajulikani ?

Kwetu sisi waislamu kuna elimu ya kuhakiki wa habari na mara nyingi kama mtu hajulikani jambo lake huwa halifnayiwi kazi,hii ni kwa uchache sana.
Niliuliza nikajibiwa kuwa aliandika consistently na maono ya mitume wengine hivyo yupo credible licha ya kwamba hajulikani..... Wengine wakadai Ni mtume paulo aliandika kwa kuangalia style ya uandishi na mtiririko. So wakakichukua

Sio hiko tu bali hta Wimbo ulio bora muandishi wake hatambuliki!!

Aisee

Labda niulize kma ikitokea kwenye Islam mwandishi hamumfahamu ila maneno yapo sawa na mafundishe ya mitume wengine je nayo mtayapuuza?? Au Jina ni muhimu kuliko content.
 
Kwahiyo hawakukwambia ni ipi kauli yenye nguvu kati ya hizo ?
Labda niulize kma ikitokea kwenye Islam mwandishi hamumfahamu ila maneno yapo sawa na mafundishe ya mitume wengine je nayo mtayapuuza?? Au Jina ni muhimu kuliko content.
Nayo hatuyachukui mpaka maandiko yawafikiane na mafundisho ya mtume wetu Muhammad amani ya Allah iwe juu yake.

Jina ni muhimu ili kujua wapi amechukua hicho alichokiandika,kwetu sisi kuwataja rijali ndio dini na lazima tuangalie wapi tunachukua dini yetu.
 
Habari za masiku wanajukwaa wote, leo ningependa tujadili watu mysterious kwenye vitabu vyetu vya dini kama ilivyo kawaida yetu. Hivyo twendeni pamoja ili tusolve mystery hii, kubwa ya yote tuongeze tu maarifa na kujibu maswali ambayo yameonekana magumu kwenye vitabu hivi.

Niweke rai mapema pamoja na kwamba inaongelea mtu wa kwenye imani zetu ila mada hii isijengwe kidini yaani kukashifiana bali ijikite kwenye mrengo wa kuelemishana. Karibuni

UTANGULIZI
Melchizidek anaongelewa kwa mara ya kwanza ndani ya Biblia kwenye kitabu cha mwanzo 14:18 ambapo baada ya Abraham kutokea vitani alikutana na Mfalme wa eneo la Salem (Jerusalem ya leo) ambapo alimbariki na Adam alimpa kikumi cha kila alichokuwa nacho wakati huo.

Kwahiyo kitabu cha mwanzo kinamueleza kama MFALME WA SALEM na kuhani wa Mungu YAHWEH

View attachment 1176929
AGANO JIPYA
Upande wa agano Jipya Melchizedek anaelezwa kuwa ana uhusiano ma Yesu.

Waebrania 5
6 kama asemavyo mahali pengine,Ndiwe kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki

Zaburi 110:4, Waebrania 5:10,6:20 zote zinaeleza kuwa Yesu ni kuhani kwa mfuatano na huyu melchizedek. Ikumbukwe Makuhani wengi wamepita hapo kati na Yesu ametokea kwenye uzao wa Abraham sasa iweje afananishwe na melchizedek na sio kuhani yeyote yule??

Je huyu melchizedek ni nani hasa?

UTATA ZAIDI
Utata zaidi unaibuka pale ambapo muandishi wa kitabu cha waebrania (ambaye mpaka leo hafahamiki ni nani) anaandika haya
Waebrania 7
3 hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.

Tunaambiwa huyu ''Jembe'' hakuwa na baba wala mama na anaishi milele hata sasa???

Ukisoma sura yote inamsifia mtu huyu wa ajabu (mysterious) na kusema licha ya ukuu wa Abraham kama Baba wa wayahudi ila haoni ndani kwa huyu Melchizedek!!

Book of Enoch
Muandishi wa kitabu hiki anajaribu kutupa mwanga kidogo kuhusu utata huu. Ukisoma Enoch 2 sura ya 71 inaeleza kuwa Kuhani Nir (Kaka yake Nuhu) alikuwa na mke ambaye hakulala naye toka alipoteuliwa na Mungu kuwa kuhani. Siku moja anagundua mke wake ana mimba, hivyo ukazuka ugomvi mkubwa mwishowe yule mama akapata presha akaanguka akafa, sasa cha ajabu walipotaka kuizika maiti haraka haraka ''kuua soo'' Wakashangaa mtoto ametoka tayari!!!. Yaani maiti imezaa!!!
Hivyo ikawa concluded kuwa kazaliwa bila baba wala mama.

Ikumbukwe alizaliwa kabla ya gharika, hivyo ili unabii utimie kuwa atakuwa kuhani wa makuhani wote ikabidi Malaika Gabriel amchukue na kumficha bustani ya Eden hivyo akapona gharika na akarudishwa baada ya gharika kupita.

HITIMISHO
Katika pekua pekua zangu sijakutana kabisa na maandiko yeyote kwenye biblia na pseudepigrapha (vilivyoachwa) ambacho kinagusia mwisho wake zaidi vyote vinasema anaishi milele ingawa havisemi wapi ama lini aliacha kuwa mfalme wa Salem.

Sasa wajuvi wa Historia na Dini mtusaidie je mtu huyu alikua nani hasa??

Pia kma alikuwa mkuu kuliko Abraham na amefananishwa na Yesu kwanini hajaongelewa sana kwenye Bible??

Je historia yake ni ipi??

Je mwisho wake ni upi hapa duniani? Au bado anaishi na sisi kwa sura tofauti?

Karibuni....

The fact remains that Melchizedek’s nationality, genealogy, and offspring are left undisclosed in the Scriptures, and that with good reason, for he could thus typify Jesus Christ, who by Jehovah’s sworn oath “has become a high priest according to the manner of Melchizedek forever.”— Heb 6:20

Melkizedeki ni aina (mfano / muwakilishi) ya Kristo, anayeonyesha huduma ya Bwana kabla yake.

Inawezekana kwamba Ibrahimu, baada ya vita vyake vya kuchosha, alikutana na kumpa heshima Bwana Yesu mwenyewe.
 
Je huu wimbo ulio bora mnaufanyia kazi ? Kama mnaufanyia kazi kwanini na kwa vigezo gani ?
Unafanyiwa kazi sababu unaongelea Upendo wa kristo kwa kanisa lake.

Wamebase kwenye content tu sawa na ww Zurri naweza amini mada zako ingawa sikujui kabisa maana na base kwa content

So bado hamna shida hta kma muandishi hafahamiki muhimu tu asiwe amepotosha au kukinzana na wenzie.
 
Wamebase kwenye content tu sawa na ww @Zurri naweza amini mada zako ingawa sikujui kabisa maana na base kwa content

Mnajuaje kama iko sawa yaani mizani yenu ya usawa ni ipi ?

Je katika hiyo nyimbo marejeo yake ni katika Injili au Torati au Zaburi ?
 
Niliuliza nikajibiwa kuwa aliandika consistently na maono ya mitume wengine hivyo yupo credible licha ya kwamba hajulikani..... Wengine wakadai Ni mtume paulo aliandika kwa kuangalia style ya uandishi na mtiririko. So wakakichukua

Sio hiko tu bali hta Wimbo ulio bora muandishi wake hatambuliki!!

Aisee

Labda niulize kma ikitokea kwenye Islam mwandishi hamumfahamu ila maneno yapo sawa na mafundishe ya mitume wengine je nayo mtayapuuza?? Au Jina ni muhimu kuliko content.
Mwandishi anatambulika sema wewe humtambui anaitwa mfalme Suleiman Mwana Wa Daudi
 
Unafanyiwa kazi sababu unaongelea Upendo wa kristo kwa kanisa lake.

Wamebase kwenye content tu sawa na ww Zurri naweza amini mada zako ingawa sikujui kabisa maana na base kwa content

So bado hamna shida hta kma muandishi hafahamiki muhimu tu asiwe amepotosha au kukinzana na wenzie.

If Melkizedeki is Jesus Christ then the next coming of Jesus will be the "Third coming" not the Second coming as it is preached, Bible scholars need to update their theology
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom