Elections 2010 Meja Jenerali Kitundu awaweka sawa wanajeshi - Msishabikie chama, pigeni kura kiraia

mimi sioni mgawanyiko wowote ktk jeshi letu!! Ila mashabiki wa chadema ndio wanahamu jeshi ligawanyike wakidhani wao chadema watafaidika na mgawanyiko huo!!! Sasa chadema mumepiga mahesabu vibaya kwani kwa hakika jeshi letu lina nidhamu ya hali ya juu na mgawanyo wa madaraka unafanyika kwa mujibu wa sheria na hapa kauli ya mkuu wa jkt sioni kama inagongana na ya mnadhimu mkuu wa jeshi (shimbo) kwani yeye shimbo aliongelea hali ya usalama wakati wa uchaguzi na huyu wa jkt amewaasa wanajeshi kutoshabikia chama wakati wakiwa wako kazini kijeshi!!

sasa huo mgawanyiko munao utafuta utokee ktk jeshi letu sijui mumeuonea wapi?
chadema wacheni uchimvi na kuwachonganisha maafisa wa jeshi letu! Huu sio ustaarabu wala si uzalendo kuwa na hamu jeshi letu lipatwe na msukusuko kwa faida zenu za kisiasa!!! Yaani munadhani jeshi likigawanyika ndio slaa atakuwa rais!! Munajidanganya!!!
 
Na kwa vile kauli hii imetolewa na afisa wa juu kuliko Shimbo.. for me thats settles it; kuna habari kuwa tayari ulishatolewa waraka na CDF (kabla ya gumzo la Shimbo) ambalo umetoa maelekezo kwa wakuu wa vikosi jinsi ya kuact. Wakuu wengi wa vikosi wanadokeza kuwa wanazingatia waraka huu unaowataka kuwa neutral na hawafuati maagizo kutoka kwenye mikutano ya waandishi wa habari

Wengi wanafahamu kuwa huo ndio mwenendo wa jeshi tangu mfumo wa vyama vingi vianze. Kwa hiyo huo waraka wa CDF ni kusisitiza utamaduni ambao tayari upo, and it is smart thing to do pamoja na kuwa it is nothing new. Na Makamanda wenye akili wanajua hilo. Na asakri wapiganaji ikiwa ni pamoja na wale wa vyeo vya chini wanajua kuwa order hawapokei kutoka kwenye media, kuna proper channels za kupokea orders.

Lakini swali ni kuwa, Jeshi litamfanya nini Shimbo? ataachwa hivi hivi tu pamoja na utovu wa nidhamu wa kiwango cha juu? amachafua sana sura ya jeshi na kupunguza imani ya wananchi kuhusu Jeshi. Watu wameanza kuwa na hofu kuwa huenda si Jeshi la wanachi bali ni Jeshi la Chama.
 
Nieleweke vizuri ndugu yangu,Hili siyo jambo la kisiasa,kutoa mfano wa uongozi wa kisiasa tena kwa muundo wa Muungano wa TZ,ni kujishusha hadhi Mkuu..

Kujishusha hadhi kivipi?? bado narudia kuwa Shimba hana backup wakati Kitundu anayo!
[/COLOR]
research..No right to speak.

Mkuu kwani hii inahitaji research ya aina gani ya rocket au sterm cell?, hivi unawakumbuka akina Doe, akina Sankara et al??

Kitundu ana Command ya kikosi ndani ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kama ilivyo kwa Meja Jenerali yeyote anayeongoza vikosi/jeshi la Anga,Maji etc as I said ealier..lakini hawa wote wanaripoti kwa Chief of Staff (Mnadhimu Mkuu) na Mkuu wa Majeshi Hayo yoote/vikosi vyote na ambao ndio viongozi wakuu wawili wa mwisho kabisa
.

Achana na hiyo habari ya nani anaripoti kwa nani, wale wanaokomand vikosi (Ma-brigedia, ma-Major Generals) ndie wenye nguvu sio wale wanaokaa pale UPNG especially mtu kama chief-of-staff!. Mkuu wa jeshi la anga ama jeshi la nchi kavu akikasirika ni dakika chache tu anaweza kwenda kum-roundup huyo Shimba pale UPNG! hawa sio watu wakudharauliwa hata kidogo ni wazee wa kazi!

Huu ndio mpangilio wa madaraka ya juu zaidi KIJESHI. Luteni Generali (Shimbo) yupo juu ya Shitundu WITH NO POLITICS..Ulichosema wewe ni kama (kwa mfano) kumlinganisha kamishna mkuu wa Jeshi la Polisi (utawala) Tanzania nzima ambaye yupo baada ya Inspekta mkuu wa polisi na Kamishna wa kanda maalumu wa polisi mkoa fulani,ambapo kimsingi huyu anaripoti kwake (wa utawala) + Inspekta!

Hivi unadhani sijui mpangilio wa GESHI letu??? mpangilio wa uongozi ninaufahamu kabla hata hiyo Wikipedia yako haijawa mtandaoni; Toka enzi za wanageshi wazalendo wa kweli wasiopenda kuchanganya mambo ya ajabu-ajabu: The great Sarakikyas, the Twalipos, Marwas, Msuguris, Kiaros, akina Black Mamba, the Kiwelus, the great Mayungas....

Tena kwa taarifa yako hicho kiti cha Chief- of- Staff katika Geshi letu kilikuwa kinakaliwa na ma-Brigedia generals na Major generals hawa hawa unaowadharau!. Tuna bahati tu ma-Brigedia general na ma-Major generals wetu ni watu wastaarabu, kwenye nchi nyingine kauli kama hizo za akina Shimba huwa zinachukuliwa kama opportunity ya kuanzisha masoo mengine:hand:

 
Luteni Jenerali ni Mkubwa kwa Ranks za Kijeshi kuliko Meja Jenerali. Suala la yeye kuongoza JKT ni dogo kwa JWTZ. Ukiangalia suala kuongoza kundi la Wanajeshi utakuwa unakiukimbia ukweli. Kwani kati ya Brigedia (anaongoza Brigedi) na Luteni Jenerali yupi mkubwa?

Suala la Makamu wa Rais wa JMT na Rais wa Zanzibar: wakiwa wote uwanjani ktk shere za uhuru nani kati yao anaanza kuondoka uwanjani?

Ndugu usipotoshe utaratibu wa majeshi, ni vizuri ukafuatilia kuliko kukisia.

Utaelewa siku nyingine!
 
Hii hainishangazi lakini inanirudisha nyuma sana. Wananchi wanapata shida; hakuna maji sehemu nyingi, hakuna chakula sehemu nyingi za nchi, uchumi umekuwa mbaya sikuzote, wanajeshi wengi wa renk za chini wana ndugu wana kufa muda huu naandika huko Muhimbili, wanafunzi wengi wanaotoka familia maskini hawawezi kwenda tena shule, ujambazi na mengineo mengi hatuwezi kuyaeleza leo. Wananchi watapata mwamko gani ili waweze kubadili viongozi nchini kwetu? Umaskini sio wa ulazima Tanzania na ninaomba sana kila Mtanzania ahimizwe Upigaji wa Kura. Uchaguzi ni moja wapo ya nafasi maalumu ya kubadili viongozi na sera ili nchi iende njia nyingine. Chama kinachoshinda ndicho kinauwezo mkubwa wa kutafuta soluhisho la matatizo ya nchi. NI MUHIMU KUPIGA KURA NA TUSIOGOPE JESHI AU KIONGOZI YEYOTE WA CCM. Kama kuna mtu yeyote anafikiri ni rahisi kuondoa viongozi kama Lowasa ni kitu rahisi. Upigaji kura mwingi ndio solution nyumbani. Amini Usiamini kuna viongozi serikalini, jeshini, na hata usalama wa taifa wanataka mabadiliko lakini hawawezi kusema hadharani. Tukipiga kura kwa wingi na CCM ikaiba WATAFANYA KILA NJIA KUITETEA NCHI YAO.
 
Kujishusha hadhi kivipi?? bado narudia kuwa Shimba hana backup wakati Kitundu anayo!
[/COLOR]


Mkuu kwani hii inahitaji research ya aina gani ya rocket au sterm cell?, hivi unawakumbuka akina Doe, akina Sankara et al??

.

Achana na hiyo habari ya nani anaripoti kwa nani, wale wanaokomand vikosi (Ma-brigedia, ma-Major Generals) ndie wenye nguvu sio wale wanaokaa pale UPNG especially mtu kama chief-of-staff!. Mkuu wa jeshi la anga ama jeshi la nchi kavu akikasirika ni dakika chache tu anaweza kwenda kum-roundup huyo Shimba pale UPNG! hawa sio watu wakudharauliwa hata kidogo ni wazee wa kazi!



Hivi unadhani sijui mpangilio wa GESHI letu??? mpangilio wa uongozi ninaufahamu kabla hata hiyo Wikipedia yako haijawa mtandaoni; Toka enzi za wanageshi wazalendo wa kweli wasiopenda kuchanganya mambo ya ajabu-ajabu: The great Sarakikyas, the Twalipos, Marwas, Msuguris, Kiaros, akina Black Mamba, the Kiwelus, the great Mayungas....

Tena kwa taarifa yako hicho kiti cha Chief- of- Staff katika Geshi letu kilikuwa kinakaliwa na ma-Brigedia generals na Major generals hawa hawa unaowadharau!. Tuna bahati tu ma-Brigedia general na ma-Major generals wetu ni watu wastaarabu, kwenye nchi nyingine kauli kama hizo za akina Shimba huwa zinachukuliwa kama opportunity ya kuanzisha masoo mengine:hand:


Is it?..............duh.............Aisee!
 
Na kwa vile kauli hii imetolewa na afisa wa juu kuliko Shimbo.. for me thats settles it; kuna habari kuwa tayari ulishatolewa waraka na CDF (kabla ya gumzo la Shimbo) ambalo umetoa maelekezo kwa wakuu wa vikosi jinsi ya kuact. Wakuu wengi wa vikosi wanadokeza kuwa wanazingatia waraka huu unaowataka kuwa neutral na hawafuati maagizo kutoka kwenye mikutano ya waandishi wa habari

Lieutenant General ni mkubwa kuliko Major General, hivyo Shimbo ni mkubwa kuliko Kitundu.
 
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limewataka wanajeshi wake, kutoshabikia chama chochote cha siasa na badala yake kuwasikiliza wagombea na kumchagua mtu anayejali maslahi ya nchi.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa jeshi hilo nchini, Meja Jenerali , Samwel Kitundu, alipokuwa akifungua Kituo cha Afya cha Makutopora kilichopo Manispaa Dodoma Mjini.


Alisema "Sisi hatuhusiki kwa namna yoyote kushabikia chama chochote cha siasa...siku ya uchaguzi inapofika tunayo nafasi ya kwenda kushiriki kupiga kura kama raia wengine, haya yapo wazi kwetu."

Meja Jenerali Kitundu alisisitiza kuwa asingependa kuona inatokea dosari yoyote kwa mwanajeshi kufanya jambo ambalo ni kinyume cha maagizo hayo.

"Kwa ufahamu wetu tuwe tumewa pima vilivyo (wagombea) kwa hiyo tunapokwenda katika kutimiza wajibu wetu tunakwenda kuchagua kile ambacho tunaamini kwamba kitakuwa kwa maslahi ya nchi yetu," alisema.

Hata hivyo, alisema ni ruksa kwa wanajeshi kwenda kusikiliza mikutano ya kampeni lakini wawe wao binafsi na sio kama jeshi.


Alisema wanapokwenda katika mikutano hiyo wahakikishe wamevaa nguo za kiraia na si sare za jeshi.

Kwa upande wake, Kaimu Mganga wa kituo hicho, Dk. Felister Abdallah, alisema kituo hicho kinakabiliwa na upungufu wa waganga, wauguzi na wataalam wa maabara.

Pia alisema kituo hicho kinakabiliwa na tatizo la usafiri hasa inapotokea wagonjwa kupelekwa katika hospitali za rufaa na hivyo kuomba kupatiwa gari la wagonjwa.

Alisema hivi sasa wamekuwa wakiwapeleka wagonjwa katika hospitali za rufaa kwa kutumia usafiri wa lori.

Naye Kamanda wa Kikosi cha Makutopora, Meja Kapteni Damian Sanga, alisema kuwa kikosi hicho cha 834 KJ, kimefanya ukarabati wa wodi mbili na kujenga wodi mpya ya watoto.

"Majengo hayo pamoja na ukarabati wa jengo moja la nyumba ya Pstaff ambao haujakamilika umefanywa kutokana na fedha za maendeleo zilizotumwa kikosini kwa mwaka 2009/2010," alisema.

Aliongeza kuwa fedha za maendeleo zilizotumwa kwa mwaka huo zilikuwa sh. milioni 98.5.

Aidha, alisema ukarabati wa jengo la utawala na kituo cha ushauri nasaha na upimaji VVU, umefanywa na kampuni ya Farm Access.

Akijibu changamoto hizo, Meja Jenerali, Kitundu, alisema ameyachukua mapungufu wa hayo na kwamba suala la upungufu watendaji muhimu katika kituo hicho ni jambo ambalo watalishughulikia mapema.

Kuhusu gari la wagonjwa, alisema tatizo hilo lipo katika vikosi vyao vingi kwamba kila mwaka watakapopata magari watapeleka katika vikosi ili kupunguza tatizo hilo.

Kituo hicho cha afya mbali ya kuhudumia wanajeshi na familia zao, kimekuwa kikihudumia pia wakazi wa vijiji vya Mchemwa, Veyula, Gawaye, Chihanga, Msalato, Kongogo, Tinai, Mbalawala, Chukikwi na Babayu.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

My Take:
Hivi kwanini Shimbo hakuweza kusema kitu chepesi kama hiki au hadi kuja na mikwara.

Kwenye red hapo juu, hivi kweli hiki cheo kiko JWTZ? Waandishi wetu sio makini sana!
 
BRAVO Kitundu, hawa ndio wanajeshi wanayoitakia mema nchi hii. Kauli yake ni nzito na inaonyesha nidhamu ya jeshi, na kwamba wapo tayari kulinda usalam wa watanzania chini ya Rais yeyote ajaje. BIG UP Kitundu!
 
....... Upigaji kura mwingi ndio solution nyumbani. Amini Usiamini kuna viongozi serikalini, jeshini, na hata usalama wa taifa wanataka mabadiliko lakini hawawezi kusema hadharani. Tukipiga kura kwa wingi na CCM ikaiba WATAFANYA KILA NJIA KUITETEA NCHI YAO.

Mkuu ulilose3ma ni kweli. Kuwa kwenye system haina maana kwamba wote ni wabovu kama hao viongozi wa juu wa cccm.
Wapo viongozi wengi sana ktk majeshi yetu (yote) na pia ktk usalama wa Taifa ambao ni wazalendo ... isipokuwa kwa taratibu za kazi zao hawawezi kuongea out of turn maana hawana mamlaka ya kusemea vyombo vyao. Lakini nina imani ikifikia hatua ya watu kutaka kuiingiza nchi ktk vurugu za kisiasa watatumia nafasi zao pale walipo kuinusuru nchi yao.
 
UYumzee ana busara as amesoma alama za nyakati akaona asije temwa na Slaa.
Slaa unaweza mkumbuka kwenye ufalme wako
 
Back
Top Bottom