Meja Jenerali Kitundu awaweka sawa wanajeshi - Msishabikie chama, pigeni kura kiraia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Meja Jenerali Kitundu awaweka sawa wanajeshi - Msishabikie chama, pigeni kura kiraia

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 10, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 10, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limewataka wanajeshi wake, kutoshabikia chama chochote cha siasa na badala yake kuwasikiliza wagombea na kumchagua mtu anayejali maslahi ya nchi.

  Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa jeshi hilo nchini, Meja Jenerali , Samwel Kitundu, alipokuwa akifungua Kituo cha Afya cha Makutopora kilichopo Manispaa Dodoma Mjini.


  Alisema "Sisi hatuhusiki kwa namna yoyote kushabikia chama chochote cha siasa...siku ya uchaguzi inapofika tunayo nafasi ya kwenda kushiriki kupiga kura kama raia wengine, haya yapo wazi kwetu."

  Meja Jenerali Kitundu alisisitiza kuwa asingependa kuona inatokea dosari yoyote kwa mwanajeshi kufanya jambo ambalo ni kinyume cha maagizo hayo.

  "Kwa ufahamu wetu tuwe tumewa pima vilivyo (wagombea) kwa hiyo tunapokwenda katika kutimiza wajibu wetu tunakwenda kuchagua kile ambacho tunaamini kwamba kitakuwa kwa maslahi ya nchi yetu," alisema.

  Hata hivyo, alisema ni ruksa kwa wanajeshi kwenda kusikiliza mikutano ya kampeni lakini wawe wao binafsi na sio kama jeshi.


  Alisema wanapokwenda katika mikutano hiyo wahakikishe wamevaa nguo za kiraia na si sare za jeshi.

  Kwa upande wake, Kaimu Mganga wa kituo hicho, Dk. Felister Abdallah, alisema kituo hicho kinakabiliwa na upungufu wa waganga, wauguzi na wataalam wa maabara.

  Pia alisema kituo hicho kinakabiliwa na tatizo la usafiri hasa inapotokea wagonjwa kupelekwa katika hospitali za rufaa na hivyo kuomba kupatiwa gari la wagonjwa.

  Alisema hivi sasa wamekuwa wakiwapeleka wagonjwa katika hospitali za rufaa kwa kutumia usafiri wa lori.

  Naye Kamanda wa Kikosi cha Makutopora, Meja Kapteni Damian Sanga, alisema kuwa kikosi hicho cha 834 KJ, kimefanya ukarabati wa wodi mbili na kujenga wodi mpya ya watoto.

  "Majengo hayo pamoja na ukarabati wa jengo moja la nyumba ya Pstaff ambao haujakamilika umefanywa kutokana na fedha za maendeleo zilizotumwa kikosini kwa mwaka 2009/2010," alisema.

  Aliongeza kuwa fedha za maendeleo zilizotumwa kwa mwaka huo zilikuwa sh. milioni 98.5.

  Aidha, alisema ukarabati wa jengo la utawala na kituo cha ushauri nasaha na upimaji VVU, umefanywa na kampuni ya Farm Access.

  Akijibu changamoto hizo, Meja Jenerali, Kitundu, alisema ameyachukua mapungufu wa hayo na kwamba suala la upungufu watendaji muhimu katika kituo hicho ni jambo ambalo watalishughulikia mapema.

  Kuhusu gari la wagonjwa, alisema tatizo hilo lipo katika vikosi vyao vingi kwamba kila mwaka watakapopata magari watapeleka katika vikosi ili kupunguza tatizo hilo.

  Kituo hicho cha afya mbali ya kuhudumia wanajeshi na familia zao, kimekuwa kikihudumia pia wakazi wa vijiji vya Mchemwa, Veyula, Gawaye, Chihanga, Msalato, Kongogo, Tinai, Mbalawala, Chukikwi na Babayu.

  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

  My Take:
  Hivi kwanini Shimbo hakuweza kusema kitu chepesi kama hiki au hadi kuja na mikwara.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Shukrani kwa taarifa nzuri kuwa jeshi lote halina viongozi mafisadi kama Shimbo.

  Shimbo na wengineo wana wasiwasi na Chadema na haswa Dr. Slaa kuwa atawafikisha kwenye tanuru ya haki kwa dhuluma kubwa walizotufanyia na ndiyo maana wanatutishia tusifanye maamuzi ya busara kwenye chaguzi hii. Hawataki kujibu hoja ya Meremeta, Kagoda Military radar, n.k

  Hata hivyo Mwenyezi Mungu yupo pamoja nasi
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  hapo ndipo inapoonyesha mgawanyiko ndani ya Jeshi, wengine wako kimaslahi ya taifa zaidi nadhani hawa hawako kwenye hiyo mitandao, lakini wengine wako tayari kuvunja katiba ya nchi kwa maslahi binafsi
   
 4. M

  Masauni JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 5. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mzee Mjj Gen. Shimbo anajua anachofanya. Si bahati mbaya au kwa kukosea
   
 6. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Very nice. Tuoine ccm hapa watasemaje!!! Maana walimshabikia afande wao aliye tisha wapiga kura.
   
 7. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Huyu MGeneral tayari ameshahesabiwa! huyu ni mzalendo, sina la kuongeza
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Oct 10, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Na kwa vile kauli hii imetolewa na afisa wa juu kuliko Shimbo.. for me thats settles it; kuna habari kuwa tayari ulishatolewa waraka na CDF (kabla ya gumzo la Shimbo) ambalo umetoa maelekezo kwa wakuu wa vikosi jinsi ya kuact. Wakuu wengi wa vikosi wanadokeza kuwa wanazingatia waraka huu unaowataka kuwa neutral na hawafuati maagizo kutoka kwenye mikutano ya waandishi wa habari
   
 9. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Si kwamba watu wote serikalini au jeshini hawana uelewa wa matatizo yetu kama taifa, la hasha, wengi wanaelewa vyema kuwa taifa lina tatizo mahali fulani na wengi wanajua kuwa tatizo ni mfumo uliopo.

  Mjj nakushukuru sana kwa kutuletea hii hapa, binafsi yangu nisingeiona kwa sababu nimesusa kununu magazeti ya IPP media kwa kuwa yanapendelea mafisadi. naamini huo utakuwa mchango wangu mkubwa kwa taifa langu.

  Viongozo kama hao, tunatakiwa kunote down majina yao kwa ajili ya kuwawezesha kulitumikia vyema taifa lao siku itakapofika.

  Aluta Continuor, mapambano bado yanaendelea.

  Respect.
   
 10. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aliyoyaongea huyu Mkuu wa JKT ndiyo Watanzania wengi tungependa kuyasikia toka kwa Wakuu wa majeshi, lakini wasiwasi wangu huyu mafisadi wameshammulika kama wataweza kuiba kura hapo October 31 na kurudi madarakani basi huyu Mkuu "atastaafishwa kwa manufaa ya mafisadi"
   
 11. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Mambo haya ndo nilikuwa nataka kuyasikia..meja jenerali kitundu wewe ni mzalendo na kuna Siku utakuja kuvikwa nishani kwa maneno yako haya.mungu akupe maisha marefu san a
   
 12. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Kwa kuwa hii imesemwa na kuhakikiwa na wewe basi na iwe Kama bwana atakavyo na kutuwezesha kufanya mabadiliko tar 31.... Huyu kweli ndo meja na amepikwa kuwa mwanajeshi
   
 13. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Of course sitegemei kama Shimbo atakuwa mjinga kiasi hicho akaweka kwenye makaratasi habari za utata kama zile. Akifanya hivyo atakuwa anaanda kamba ya kujifunga mwenyewe na credibility yake. Ubaya ni kuwa wanasiasa wa sasa nao watapita tu kama walivyo wengine wote. Ataufichia wapi uso wake akiitengeneza kashfa isiyo hata na sababu
   
 14. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #14
  Oct 10, 2010
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Lieutenant General (Cheo cha Shimbo) ni cheo cha juu zaidi ya Major General alichonancho Kitundu..cheo hicho ni kikubwa jeshini na anayekuwepo huwa ni mmoja tu na kazi yake kubwa ni Overall admnistration ndani ya Jeshi zima (Chief of staff in other words),lakini ma-major generals huwa ni wengi kiasi upto five ambao wanaongoza vikoso kama JKT,ANGA,MAJI etc..na mtu wa mwisho baada ya hapo ni General i.e Mwamunyange..Just Corrections! Thanks
   
 15. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu mimi napingana nawewe! Kitundu ni mkubwa kwa Shimbo kwa sababu yeye anaongoza jeshi linaloitwa JKT, wakati Shimbo ni mtu wa utawala tu. Cheo cha Shimbo ni kama vile makamu wa Raisi wa JMT kwa Rais wa ZNZ. Wakati kiprotokali makamu wa Rais wa JMT anaonekana ni mkubwa lakini kiukweli hana nchi anayoongoza!

  Kwa kuongezea tu, kama bifu likitimka Kitundu atakuwa na backup ya jeshi lake wakati Shimbo atajikuta hana wa kumlinda zaidi ya wale mabodyguads wake tu....
   
 16. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Kwenye majeshi ambayo maofisa wanakosa nidhamu na kutofuata taratibu,General anaweza akawa hana commanding authority kama Colonel. Jeshi lolote uhai wake upo kwenye nidhamu na kufuata sheria. Vinginevyo ni kutengeneza matatizo maana ni rahisi askari kuvunja taratibu za kufuata chain of command.Askari wana upeo wa kuelewa. Si busara kuwatoa nje ya line yao ya kazi ili kulinda maslahi binafsi. Tukumbuke matatizo kama yale ya Ivory Coast, Zaire na sehemu nyingi za Afrika yalitengenezwa na wanajeshi waliotaka kutoa favors kwa wanasiasa fulani bila kufuata haki wala sheria.
   
 17. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Luteni Jenerali ni Mkubwa kwa Ranks za Kijeshi kuliko Meja Jenerali. Suala la yeye kuongoza JKT ni dogo kwa JWTZ. Ukiangalia suala kuongoza kundi la Wanajeshi utakuwa unakiukimbia ukweli. Kwani kati ya Brigedia (anaongoza Brigedi) na Luteni Jenerali yupi mkubwa?

  Suala la Makamu wa Rais wa JMT na Rais wa Zanzibar: wakiwa wote uwanjani ktk shere za uhuru nani kati yao anaanza kuondoka uwanjani?

  Ndugu usipotoshe utaratibu wa majeshi, ni vizuri ukafuatilia kuliko kukisia.
   
 18. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #18
  Oct 10, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu Mwanakijiji whats up! Mbona hii kauli anaongelea wanajeshi wake (kauli ya internal to jeshi)! na Ile ya Shimbo anaongelea suala la usalama wa nchi (public) to my understanding these are different topic all together.

  Kauli hizo hakuna inayoipinga nyingine au ku-isupport nyingine different issues... tujaribu kuondoa miwani yetu ya ushabiki wakati tukisoma haya mambo.

  Ni miwani hii ilituambia CCJ ni moto wa kuotea mbali!
   
 19. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mpige shule mtaalamu wetu!
   
 20. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2010
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Nieleweke vizuri ndugu yangu,Hili siyo jambo la kisiasa,kutoa mfano wa uongozi wa kisiasa tena kwa muundo wa Muungano wa TZ,ni kujishusha hadhi Mkuu..No research..No right to speak. Kitundu ana Command ya kikosi ndani ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kama ilivyo kwa Meja Jenerali yeyote anayeongoza vikosi/jeshi la Anga,Maji etc as I said ealier..lakini hawa wote wanaripoti kwa Chief of Staff (Mnadhimu Mkuu) na Mkuu wa Majeshi Hayo yoote/vikosi vyote na ambao ndio viongozi wakuu wawili wa mwisho kabisa,Huu ndio mpangilio wa madaraka ya juu zaidi KIJESHI. Luteni Generali (Shimbo) yupo juu ya Shitundu WITH NO POLITICS..Ulichosema wewe ni kama (kwa mfano) kumlinganisha kamishna mkuu wa Jeshi la Polisi (utawala) Tanzania nzima ambaye yupo baada ya Inspekta mkuu wa polisi na Kamishna wa kanda maalumu wa polisi mkoa fulani,ambapo kimsingi huyu anaripoti kwake (wa utawala) + Inspekta! ..Nenda Wikipedia huko utapata shule zaidi,hiki nikupacho ni just a normal understanding BUT MORE PRECISE. Mind u,TZ is using British army commission style which is also adopted in the Commonwealth countries.

  MY CONTRIBUTION ON TOPIC: Mungu ambariki kitundu kwa moyo wake wa kizalendo. AMeonyesha uwezo mkubwa kama kiongozi wa jeshi ambalo kimsingi halipaswi kuingiliana moja kwa moja na politcs,though Politics is the KING inawagusa moja kwa moja wao binafsi,familia na ndugu kwa ujumla..so mmoja mmoja kama raia ana haki ya kujiandikisha na kupiga kura kama mtanzania yeyote..lakini si kufanya siasa ndani ya jeshi kama anavyotaka kuitumbukiza Lt Gen Shimbo coz ilishafutwa kitambo,wenzie wakati wanaondoka alikuwa wapi?..Nawatakia kila la kheri wanajeshi wote na Mungu awaguse mmoja mmoja ili tufanye uchaguzi kwa amani na mabadiliko pamoja na maendeleo yaonekane katika nchi yetu. Alamsiki
   
Loading...