At Calvary
JF-Expert Member
- Aug 22, 2018
- 4,513
- 3,552
Sasa wewe unataka tu mishahara ipande. Ikipanda halafu haulipwi hio hela kuna haja gani..!Kwakuwa hakuna aijuae kesho kwa maana leo unaweza kuwa mzima na kesho ukatangulia mbele za haki au kupata ulemavu wa Kudumu, n.k, ni sahihi kuishi kwa kutegemea matakwa au fadhila za binadamu mwenzako hasa kwa mambo sensitive ya ktaifa kama hili la haki na masilahi ya watumishi wa umma?
Swala la mishahara ya watumishi na mambo mengine katika nchi, kwanini tuyaache yategemee utashi binafsi wa Raisi?
Je, kwa bahati mbaya mwakani tukawa na Raisi mwingine kwasababu yoyote ile kulingana na katiba yetu, na Mei Mosi Raisi huyo akaamu kutongeeza mishahara kwasababu yoyote atayoitoa, watumishi watapaswa tena kusubiri miaka saba ndio masilahi yao yaangaliwe?
Kama ambavyo leo hii Magufuli hayupo, nani ana uhakika mwakani Mama Samia atakuwepo au yeye mwenyewe atakuwepo?
Ukweli ni kwamba, anaweza asiwepo Mama Samia na hata makamu wake au wanaweza kuwepo lakini wote wssiwe fit kukalia hicho kiti.
Kama utadhani mimi nina mawazo mabaya, basi walioandika katiba yetu watakuwa na mawazo mabaya zaidi.
Wakati umefika, mambo ya msingi katika nchi yasiwe ni matakwa binafsi ya Raisi vinginevyo nchi hii na watu wake wataendelea tu kupiga mark time miaka nenda miaka rudi.
Embu kwanza tuboreshe miundombi u.