Mei mosi: Sina imani tena na vyama vya wafanyakazi

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,598
3,644
Mambo yafuatayo yamenifanya nione Meimosi hii nisiisherekee kwa kukosa imani na vyama vya wafanyakazi.

1. Serikali imevitia kapuni, havina nguvu ya kuishurutisha Serikali kuboresha maslahi ya watumishi.

2. Vyama kushindwa kuwatetea watumishi waliotumbuliwa kwa vyeti feki japo walitumikia nchi hii zaidi ya miaka 35-40 wengi walibakiza miezi au mwaka mmoja kustaafu.

3. Watumishi wanaosumbuliwa na Serikali kila siku, vyama hivyo havina msaada wowote wa kisheria. Vimekuwa navyo ni kandamizi kwa watumishi hao.

Mtumishi amebaki anapambana kivyake kutetea maslahi yake.

SWALI: Hivi hela za watumishi mnazokata kila mwezi zinatumika kuwatoa vitambi na kutengenezea ma t-shirt ya meimosi tu? Kwanini mnashindwa kuwapa watumishi msaada wa kisheria kupitia hela zao hizo?

PENDEKEZO:
Ni ujinga na upumbavu kwa mtumishi kuendelea kukatwa fedha zake kwenye hivyo vyama ambavyo havimsaidii kwa lolote.
 
Nakubaliana nawe ni utumwa na ujambazi unaofanywa na hivi vyama vya Wafanyakazi kuchukua pesa zao kila mwezi wakati vyama hivyo havina msaada wowote kwa Wafanyakazi kwa miaka chungu nzima sasa. Wakati umefika sasa Wafanyakazi kazi kuvishinikiza vyama hivyo au kudai makato ya kila mwezi yanayokwenda kwenye vyama hivyo yasimamishwe mara moja.
 
Sisi huku tumejitoa kabisa kwenye hivyo vyama, tuliwaandikia barua wasitishe makato wakajifanya hawasikii, tukamtafuta mwanasheria tukampa barua zetu, navyokwambia walishasitisha kutukata pesa zetu.
Hivyo vyama hamna lolote
 
Vyama haviwezi kutetea wanachama waliovunja sheria za ajira Kwa kuwa walifoji vyeti vyao ambalo ni kosa kisheria

Serikali ingewaacha bila kuwatumbua ingalikuwa imevunja sheria ya ajira Na kanuni zake

Vyama vya wafanyalazi vinawatetea walioonewa kazini watumishi ambao hawajavunja sheria isipokuwa wameonewa Na mwajiri Wao

Hongera JPM kuturudishia utawala wa sheria Tanzania uliokuwa umekufa kifo cha kimya kimya huku tukiwa Na bunge lisilojua wajibu wake Kwa miaka mingi.
 
Na Waalimu wanapaswa kufanya hivi kwa chama chao CWT
 
Mambo yafuatayo yamenifanya nione meimosi hii nisiisherekee kwa kukosa imani na vyama vya wafanyakazi.
1. Serikali imevitia kapuni, havina nguvu ya kuishurutisha serikali kuboresha maslahi ya watumishi.
2. Vyama kushindwa kuwatetea watumishi waliotumbuliwa kwa vyeti feki japo walitumikia nchi hii zaidi ya miaka 35-40 wengi walibakiza miezi au mwaka mmoja kustaafu
3. Watumishi wanaosumbuliwa na serikali kila siku, vyama hivyo havina msaada wowote wa kisheria. Vimekuwa navyo ni kandamizi kwa watumishi hao.
Mtumishi amebaki anapambana kivyake kutetea maslahi yake.
SWALI: Hivi hela za watumishi mnazokata kila mwezi zinatumika kuwatoa vitambi na kutengenezea ma t-shirt ya meimosi tu? Kwanini mnashindwa kuwapa watumishi msaada wa kisheria kupitia hela zao hizo?.
PENDEKEZO:
Ni ujinga na upumbavu kwa mtumishi kuendelea kukatwa fedha zake kwenye hivyo vyama ambavyo havimsaidii kwa lolote.
Well said
 
Vululuvululu! Wakumwamini sasa ni mungu tu ichi imekamatika hii CWT haina hata habari zaidi ya kugawa tishert na kofia Fanya yako tuu. Achana na sirikaliiiii
 
Vyama haviwezi kutetea wanachama waliovunja sheria za ajira Kwa kuwa walifoji vyeti vyao ambalo ni kosa kisheria

Serikali ingewaacha bila kuwatumbua ingalikuwa imevunja sheria ya ajira Na kanuni zake

Vyama vya wafanyalazi vinawatetea walioonewa kazini watumishi ambao hawajavunja sheria isipokuwa wameonewa Na mwajiri Wao

Hongera JPM kuturudishia utawala wa sheria Tanzania uliokuwa umekufa kifo cha kimya kimya huku tukiwa Na bunge lisilojua wajibu wake Kwa miaka mingi.
Namaanisha mkubwa, wapo watu walionewa Waka struggle wenyewe kupata haki yao.
Mishahara yao ya miezi mitatu iliyosimamishwa hawajalipwa hadi leo, hivi hapo kuna chama cha wafanyakazi au wanyonyaji tu?
 
Sisi huku tumejitoa kabisa kwenye hivyo vyama, tuliwaandikia barua wasitishe makato wakajifanya hawasikii, tukamtafuta mwanasheria tukampa barua zetu, navyokwambia walishasitisha kutukata pesa zetu.
Hivyo vyama hamna lolote
safi saana mi nimefanya hivyo
 
Mambo yafuatayo yamenifanya nione meimosi hii nisiisherekee kwa kukosa imani na vyama vya wafanyakazi.
1. Serikali imevitia kapuni, havina nguvu ya kuishurutisha serikali kuboresha maslahi ya watumishi.
2. Vyama kushindwa kuwatetea watumishi waliotumbuliwa kwa vyeti feki japo walitumikia nchi hii zaidi ya miaka 35-40 wengi walibakiza miezi au mwaka mmoja kustaafu
3. Watumishi wanaosumbuliwa na serikali kila siku, vyama hivyo havina msaada wowote wa kisheria. Vimekuwa navyo ni kandamizi kwa watumishi hao.
Mtumishi amebaki anapambana kivyake kutetea maslahi yake.
SWALI: Hivi hela za watumishi mnazokata kila mwezi zinatumika kuwatoa vitambi na kutengenezea ma t-shirt ya meimosi tu? Kwanini mnashindwa kuwapa watumishi msaada wa kisheria kupitia hela zao hizo?.
PENDEKEZO:
Ni ujinga na upumbavu kwa mtumishi kuendelea kukatwa fedha zake kwenye hivyo vyama ambavyo havimsaidii kwa lolote.
Ila tukumbuke nao niwafanyakazi na wanaangalia matumbo yao ,
 
Mi nisaidieni hapa. Mfanyakazi A anakatwa 2% ya mshahara wake ambayo ni Tshs 300,000 na Mfanyakazi B anakatwa 2% ya mshahara wake ambayo ni Tshs 40,000! Km chama ni kimoja na huduma za chama ni zile zile kwa wanachama wake wote, huo utofauti unakujaje? Kifupi kwa nini michango ya wafanyakazi kwa vyama usiwe fixed amount? Mf. Elfu 10 nchi nzima.
 
Huu ni wizi wa mchana kweupe
 
Back
Top Bottom