Mei Mosi 2021 kurejesha furaha ya watumishi na wahitimu? Rais Samia ni tumaini jipya

Halafu asipofanya hayo tayari anakuwa adui wenu siyo?

Kuongoza nchi iliyo jaa wajinga wengi ni Kazi Sana.
 
Tatizo alilolitengeneza mwendazake ni kubwa Sana, sijui SSH ataanzia wapi. Kuna wafanyakazi kwa miaka 6 hawajapanda daraja.malimbikizo lukuki. Tusubiri.
 
Niungane na Tundu Lissu kuwatahadharisha wenzangu kuwa tusishangilie kupitililiza, hizi shangwe kila kona ni njema, lakini tusishangalie kupilitiliza.

Nakumbuka wakati wa Hayati Rais wetu dk Magufuli, walipotolewa wenye vyeti feki tukashangalia, wakatolewa wafanyakazi hewa tukashangalia, baadae vyeti vikaungwa na NIDA tukashangalia.

Yote hii tulidhani sasa mfupa uliomshinda Fisi umeenda kupata majibu yake. Tukaambiwa kuna bodi ya mishahara imeundwa itafanya kazi haraka kuweka mishahara sawa tukashangilia pia.

Baadae kidogo kidogo tukasikia makato ya bodi yamepanda kutoka 8%-15% ndio tukaanza kidogo kuamka, mwishowe kikaja kikotoo, halafu mwaka wa kwanza ukapita bila nyongeza, mwaka wa pili, mwaka watatu mpaka ukafikika mwaka wa Saba, Waliojariwa mwaka 2014 wakaishia na mshahara ule ule wa JK Kikwete.

Nayasema haya ndugu zangu kwakuwa msema kweli ni mpenzi wa Mungu nimeona kila kona watu wakishangilia.

Kwa wafanyakazi wenzangu niwasihi Mei Mosi hii itatoa mwanga kuwa HUYU NDIE YULE AJAYE, AU TUMTAZAMIE MWINGINE

Muwe na siku njema!
 
Pressure ni kubwa kuna mtu hakulala kwa miaka sita lakini bado muda huo wote haukutosha kuibadilisha Tanzania. Kwa maoni yangu nadhani kwa sasa jambo kubwa sio kuongeza mshahara, dunia nzima watu wanapunguziwa mishahara kwasababu ya Covid-19 cha msingi tunaomba ajira kwa vijana wetu through goverment employments from projects or direct employments and from investors, kama wamekomalia watu wajiajiri basi wahakikishe fungu la mikopo rafiki kwa vijana na kina mama linaongezwa maradufu, hapo angalao kila mtu atapata share ya nchi japo kidogo.
 
Pressure ni kubwa kuna mtu hakulala kwa miaka sita lakini bado muda huo wote haukutosha kuibadilisha Tanzania.... kwa maoni yangu nadhani kwa sasa jambo kubwa sio kuongeza mshahara, dunia nzima watu wanapunguziwa mishahara kwasababu ya Covid-19 cha msingi tunaomba ajira kwa vijana wetu through goverment employments from projects or direct employments and from investors, kama wamekomalia watu wajiajiri basi wahakikishe fungu la mikopo rafiki kwa vijana na kina mama linaongezwa maradufu, hapo angalao kila mtu atapata share ya nchi japo kidogo.
Unasemaje wewe? ni nani huyo hakulala kwa miaka sita? unajua masaibu yaliyowapata wafanyakazi wewe?
 
unasemaje wewe? ni nani huyo hakulala kwa miaka sita? unajua masaibu yaliyowapata wafanyakazi wewe?
Nayajua kwakua nami ni mfanyakazi ila je nawewe unaya feel masahibu wnayoyapata waliokosa ajira ? au ndio kusema mwamba ngoma huvutia kwake
 
Nayajua kwakua nami ni mfanyakazi ila je nawewe unaya feel masahibu wnayoyapata waliokosa ajira ? au ndio kusema mwamba ngoma huvutia kwake
Aliyesimamisha ajira ndio huyo hyo alisimamisha wafanayakazi kupanda madaraja na nyongeza ya mshahara, ndio maana nasema tusubiri Mei mosi pengine Nchi ikarudi katika mstari ule ule.
 
Furaha ya watumishi na wahitimu vyuo mbalimbali itarejea siku chache zijazo yaani Mei Mosi. Watumishi walio wengi wanaishi kwa ⅓ ya mshahara baada ya kuingia kwenye mikopo ili kuinua maisha yao.

Tunatarajia kusikia mambo haya kutoka kwa Rais:
  • Mishahara kupanda
  • Kupanda madaraja
  • Kupanda vyeo
  • Kubadilishiwa muundo kwa waliojiendeleza
  • Kuruhusu uhamisho hasa wa kubadilishana
  • Kutoa ajira mpya
  • Kuondoa kikokotoo kipya
  • Kurekebisha fao la kujitoa na kukosa ajira
  • Kupunguza riba ya HESLB

Hatutegemei kuona TUCTA wakiimba nyimbo za kuabudu bila ujumbe wa maslahi ya wafanyakazi

Pia soma
Mtamkataa kalibuni tu
 
Covid -19 ni shida,majirani wanakopeshwa mikopo sababu ya c-19.
 
Mishahara ya Watumishi wa Umma ipo chini sana(hasa ya walimu), HESLB ni jibu jingine pia.
Ni ile ile ya enzi za JMK wakati sukari ikiuzwa 1400 kwa kilo leo 2800 kwa kilo. Bidhaa nyingine vivyo hivyo. Kwa kweli mtumishi wa TZ anaishi kimsukule sukule !!
 
Mishahara ya Watumishi wa Umma ipo chini sana(hasa ya walimu), HESLB ni jibu jingine pia.
Hasa ya walimu..

Unaijua mishahara ya PS na wale wa masijala?

Walimu mnamshahara mzuri sanaa..

Tena mwalimu wa certificate kwasasa anatofautiana elfu 5 na bwanashamba wa certificate na nurse wa certificate.

Kila jambo ni walimu na afya, MBONA SERIKALI INA WATUMISHI WENGI SANAA??

#YNWA
 
Furaha ya watumishi na wahitimu vyuo mbalimbali itarejea siku chache zijazo yaani Mei Mosi. Watumishi walio wengi wanaishi kwa ⅓ ya mshahara baada ya kuingia kwenye mikopo ili kuinua maisha yao.

Tunatarajia kusikia mambo haya kutoka kwa Rais:
  • Mishahara kupanda
  • Kupanda madaraja
  • Kupanda vyeo
  • Kubadilishiwa muundo kwa waliojiendeleza
  • Kuruhusu uhamisho hasa wa kubadilishana
  • Kutoa ajira mpya
  • Kuondoa kikokotoo kipya
  • Kurekebisha fao la kujitoa na kukosa ajira
  • Kupunguza riba ya HESLB

Hatutegemei kuona TUCTA wakiimba nyimbo za kuabudu bila ujumbe wa maslahi ya wafanyakazi

Pia soma
Mei 1 itutazame nasisi wavuvi ziwa tanganyika uvinza kata ya kalya tumevurugwa na utawala uliopita
 
Back
Top Bottom